Nitapambana niwezavyo kuhakikisha tunabadili mfumo na sera za uendeshaji wa jeshi la polisi.Vyeo vya kupeana kindugu na kujuana unaenda kukoma,Fikiria mtoto wa mahita kaingia juzi huko ni inspector wakati kuna watu ni wasomi kuliko huyu kiumbe mwaka wa 20 Sasa bado ni macoplo.
Mdude Nyagali, CHADEMA youth leader & victim of kidnapping & torture by intelligence and security operatives for his criticism of Magufuli Dictatorship, is one of many political prisoners in Tanzania today. President Samia’s fine phrases should be judged against this ugly reality
Mdude Nyagali, kiongozi wa CHADEMA Songwe, alitekwa nyara na kuteswa na wanaUsalama wa Taifa kwa kupinga na kukosoa udikteta wa Magufuli. Rais Samia anaimba kuhusu maridhiano lakini Mdude bado ni mmoja wa wafungwa wengi wa kisiasa wa utawala huu. Zilongwa mbali na zitendwa mbali!
IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record: 1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote. 2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.
3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku. 4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.
5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi. 6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba.
Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar.
Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.
7) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo. 8) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi!
9) Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio. Lakini polisi hawakuwa na interest ya kunihoji zaidi ya kupiga mabomu mikutano yangu ya hadhara.
10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa.
IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania wote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma!
Wawekezaji na Demokrasia ni sawa na mtoto na mbeleko! Ikikatika mbeleko, mtoto huanguka! Ukiminya Demokrasia, wawekezaji hukimbia! Huwezi kumnyima pumzi mama mjamzito ukategemea kuwa mtoto aliye tumboni akaendelea kuishi! Miujiza ya aina hiyo bado haijatendeka katika uso wa dunia
Tulijua CCM wanachotaka kufanya kuhusu katiba mpya! Ndiyo maana #KatibaMpyaMovement ikaasisiwa ili kupambana non stop kudai katiba..
Niliwaonya kuwa hawa UVCCM wanatumwa tu nyuma yao ni maagizo ya chama chao! Jana mmesikia.
Ikibidi nguvu zitatumika kudai katiba mpya! SIMPLE
Unadhani hawamjui huyu mhuni aliyetoa bastola hadharani? Wanamjua vizuri sana. Wameamua kumlinda ili wamtumie siku wakimhitajia.
#Tanzania una MFUMO OVU sana.