Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kenya anayemaliza muda wake nchini, Mhe. Isaac Njenga, Ikulu Dar es Salaam, tarehe 17 Desemba, 2025.
#PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan hii leo Disemba 17, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba katika Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam.
#MillardAyoUPDATES
KIKAO KAZI CHA MAAFISA MAENDELEO YA VIJANA: KUWEKA MSINGI MPYA WA MUSTAKABALI WA VIJANA TANZANIA
Katika kipindi ambacho dunia inashuhudia mabadiliko makubwa ya kijamii, kiuchumi na kiteknolojia, vijana wameendelea kuwa kundi lenye nguvu kubwa lakini pia lenye changamoto nyingi. Kwa kutambua umuhimu huo, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imeandaa Kikao Kazi cha Maafisa Maendeleo ya Vijana wa Mikoa na Halmashauri, kinachofanyika tarehe 17–18 Disemba 2025 katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.Dodoma
Kikao hiki kimewakutanisha Maafisa Maendeleo ya Vijana kutoka ngazi mbalimbali kwa lengo la kutafakari kwa kina hali ya vijana nchini, nafasi zao katika maendeleo ya taifa, changamoto wanazokutana nazo pamoja na hatua za kimkakati zinazopaswa kuchukuliwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania ina umeme wa kutosha hatua ambayo imechangiwa na kukamilika kwa Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme ukiwemo Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ambao pekee unazalisha Megawati 2115.
Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo Julai 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia katika vituo vya Kinyerezi I, Kinyerezi I Extension na Kinyerezi II ambapo amesema licha ya kazi kubwa inayofanywa na TANESCO yapo baadhi ya maeneo yalikua na changamoto ya upatikanaji wa umeme lakini mpaka sasa yameendelea kuimarika.
Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko amefafanua kuwa ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme unaendana na mahitaji ya ongezeko la watu TANESCO inatarajia kuongeza uzalishaji umeme katika Kituo cha Kinyerezi III kutoka megawati 600 katika mpango wa awali hadi kufika Megawati 1000 mpango wa sasa.
‘’Nataka niseme mbele yenu ndugu zangu, Mhe. Rais Samia ndio Kinara wa kufanya haya yote yafanikiwe amefanya uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Nishati na ndio maana kwenye bajeti iliyopita Wizara hii imepata Shilingi Trilioni 2.3 kikubwa anataka wananchi wapate umeme wa uhakika,’’ alisema Dkt Biteko.
Aidha, Naibu Waziri Mkuu pia ametumia nafasi hiyo kuipongeza TANESCO kwa maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika ya kuwahudumia wateja hasa kwa uharaka wao wa kukabiliana na dharula zozote za umeme zinazojitokeza.
‘’Kuna maboresho makubwa yamefanyika katika kuwahudumia wananchi naona jitihada kubwa zinafanyika, mmekuwa na uharaka wa kushughulikia changamoto za umeme lakini pia niwapongeze kwa kuimarisha Kituo cha miito ya simu sasa wananchi wanahudumiwa bila gharama yoyote,’’ alisisitiza Dkt. Biteko.
Vilevile, Dkt. Biteko ametembelea Kituo cha Kupokea Gesi Asilia Kinyerezi kwa ajili ya kukagua miundombinu ya kusafirisha gesi na kuwataka kuongeza uzalishaji wa gesi ili kusaidia kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme.
Daraja la Magufuli KIGONGO-BUSISI Lenye zaidi ya km 3 litachochea ukuaji wa uchumi kwa mikoa ya kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla mawasiliano yatakuwa rahisi zaidi baina ya wananchi #sisinitanzania#drssh#mslac#matokeochanya#nchiyangukwanza
MWENGE WA UHURU WAZINDUA NEEMA YA MAJI TANDAHIMBA – VIJIJI 5 KUFAIDIKA.
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tandahimba umetenga Shilingi 452,500,000 kwa ajili ya kuchimba visima vitano vya maji safi na salama katika vijiji vya Mivanga, Lyenje, Dinduma, Mchangani na Michenjele, kwa lengo la kuondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba, Falaura Kikusa alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya Programu Maalumu ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inayolenga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama.
“Mradi huu ni mkakati maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kupunguza adha ya maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hii muhimu. Utekelezaji wake ulianza Mei 2024 na unatarajiwa kukamilika Juni 2025 kutokana na changamoto mbalimbali, licha ya mpango wa awali kumalizika Disemba 2024,” alisema Kikusa.
Kikusa alieleza kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 76, ambapo miundombinu ya maji ikiwemo usimikaji wa matanki ya lita 10,000 imekamilika katika vijiji viwili vya Mivanga na Lyenje, huku usimikaji wa pampu na mifumo ya nishati ya jua ukiwa umefanyika katika vijiji vya Mivanga, Lyenje, Dinduma na Mchangani.
Kwa mujibu wa Kikusa, gharama ya kisima kimoja ni Shilingi 90,500,000 na hadi sasa Shilingi 124,106,686.40 kati ya fedha zilizotengwa tayari zimelipwa. Fedha hizo zinatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo mpango wa Lipa kwa Matokeo, Mfuko wa Taifa wa Maji na michango ya wadau wa maendeleo.
Aidha, alisema mradi huo umetoa ajira za muda mfupi kwa wananchi wa maeneo husika wakiwemo mafundi, wapishi, na madereva, huku pia ukichochea maendeleo ya kilimo na kusaidia kupunguza magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara.
Katika kijiji cha Mivanga, kisima kimoja kina uwezo wa kuzalisha maji lita 372,000 kwa siku. Wananchi wa vijiji hivyo wametoa maeneo ya ujenzi wa visima hivyo bila fidia, yenye thamani ya takriban Shilingi 2,500,000.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed ameishukuru serikali kupitia RUWASA kwa kutekeleza mradi huo muhimu na kusisitiza kuwa umeleta afueni kubwa kwa wananchi waliokuwa wanatumia gharama kubwa na muda mwingi kutafuta maji.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kujali ustawi wa wananchi wa Tandahimba na kuwataka wakazi wa vijiji walionufaika na mradi huo kushirikiana na serikali kuutunza ili udumu kwa muda mrefu.
Mkazi wa kijiji cha Mivanga, Bi. Asha Seleman alisema mradi huo umesaidia kupunguza gharama za maisha kwa wakazi wa kijiji hicho kwani hapo awali walikuwa wananunua ndoo moja ya maji ya lita 20 kwa Shilingi 1,000.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH
@manj_cassano@1Maliga Vijana tungepata muda wa kujadili maendeleo kama ivi na pale kwenye changamoto tuseme na tutoe way forward ingekuwa ni afya sana kuliko kutumika kisiasa kudharirisha mamlaka ya nchi
@1Maliga Changamoto ya vijana mnatumika kisiasa sana mmekuwa watupu kichwani kufanya ivi kwako kunakupa faida gani mzee ebu badili fikra acha kutumia hisia kwenye kuwaza tumia akili japo kidogo then utajua unachofanya ni sahihi au kosa #sisindowajenziwatanzaniayetu