Awamu hii imekuwa na nguvu kubwa kusukuma Kilimo Agenda ya 10/30 hususani kwa Vijana ikiongozwa na Mhe.@HusseinBashe .
Sijaona Mradi wa BBT ukihamasisha Vijana kujiunga kwenye Ushirika.
Kwa Maoni yangu japokuwa muda unaelekea ukingoni: Tukiwa na Vyama vya Ushirika vya Vijana kwa kila Wilaya, tutatengeneza mbinu na myanya ya kumwezesha kijana.
Na Vyama hivi viwe Mchanganyiko (Multipurpose) na viwe powered na Vyama Vikuu na Vyama vya AMCOS.
Gregory, mmoja wa wanufaika wa ufadhili wetu, alitumia sehemu ya posho yake kuanzisha biashara. Leo, kampuni yake inazalisha zaidi ya TZS 450M kwa mwaka na imeajiri watu zaidi ya kumi.
Vijana wakiwezeshwa, wanaweza.
//
Gregory, one of the beneficiaries of our scholarship program, used part of his stipend to start a business. Today, his company generates over TZS 450M annually and has employed ten people.
When young people are empowered, they succeed.
Miaka Mitatu kwenye Biashara ya Kilimo kama Startup, nimejifunza startups zinahitaji vitu vitatu tu:
1. Wateja
2. Taarifa Sahihi
3. Mtaji
Mengine ni kelele zisizo na msaada wowote
@19SaintLaurent @GregorySimeo@SokoineU Great initiative!
An Agribusiness Fund is key to driving Agritech & Foodtech innovation. Pairing funding with startup support will boost growth, market access & sustainability.
I’ll reach out to explore this further
What about nurturing Agritech and Foodtech Startups to scale, expand exports, and drive sustainable growth?
Combining this with funding would be a game-changer! 🔥
@fikirism@GregorySimeo@SokoineU
We as Sokoine Agrienterprises Plc we want to establish an Agribusiness Fund to boost investment in Agritech and Foodtech Startups in Tanzania. @SokoineU@tadbtz
Soon, i will be writing on how tunaweza kuintegrate #ArtificialInteligence into #FoodSystems in order to improve the food sector in #Tanzania , depicting how to and analysing readiness of the country. To follow along, you need to have #chakulafasta platforms.
Hongera sana Mhe.@HusseinBashe , kwa hatua hii.
Naamini kwamba Benki hii inaenda kukuza Usharika. Hususani kuvutia Vijana kuingia kwenye Ushirika.
Na sisi kama Vijana tunawekeza nguvu, Uwezo, teknolojia Ili kuleta mabadiliko kwenye Sekta ya Ushirika, Bali kama wanachama husika.
Jana 26.07.2024 Rasmi tumezindua bodi ya kwanza ya National Cooperative Bank - Benki ya Ushirika na huu ndio umekua mkutano wa mwisho wa wanahisa wa Kilimanjaro Cooperative Bank.
Mwaka 2019, Wizara ya Kilimo ilikutana na Mwenyekiti wa Bodi na Viongozi wa KCBL na Tanzania Federation of Cooperative Union TFC kujadili namna gani tunaweza kuwa na benki ya ushirika ya kitaifa.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu na kwakuwa mchakato wa kuanzisha benki ya kitaifa ya Ushirika ulishindikana kwa zaidi ya miaka 9 tuliamua kuanza safari hiyo ngumu kwanza kufanya mabadiliko Kilimanjaro Cooperative Bank na Tandahimba Cooperative Bank
Benki zote hizi 2 zilikua zinapata hasara na zilikua hatarini kufutiwa leseni na BOT. Tulifanya mabadiliko KCBL kutoka loss making ya mwaka 2020 ya zaidi ya Milioni 600, leo imekua ni taasisi inayotengeneza faida ya bilioni moja na nusu kwa mwaka kabla ya kodi.
Tuliamua kama Serikali, kuanza mchakato wa kuanzisha Benki ya Ushirika ya Kitaifa tukitakiwa kuwa na mtaji sio chini ya Bilioni 20
Tuliingia makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati na benki ya CRDB na kuwaomba wawabadilishie madeni yao waliyokua wakiwadai KCBL na Tandahimba Cooperative Bank kuwa Equity na tukabadili Menejimenti na leo benki hizi 2 zimeunganishwa na kuanza safari ya kuanzisha Benki ya Ushirika ya Taifa. Tumeshapata approval ya BOT na Vyama vya Ushirika, SACCOS na Watu Binafsi tayari wamenunua hisa zenye thamani ya karibu Bilioni 24 kama mtaji wa kuanzisha benki hiyo.
Benki hii haitokuwa tu benki ya kuweka na kutoa, bali itakua chombo cha kufanya makubaliano baina ya vyama vikuu vya ushirika na wakulima kuwa na makubaliano ya kimkakati na taasisi za fedha ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa vyama vya ushirika na wakulima. Hii itawapa wana ushirika na wakulima kuwa na chombo chao cha fedha watakachoweza kufanya nacho biashara bila kuathiri maslahi ya ushirika na wakulima.
Nimefarijika sana kuwa hii ndoto hatimaye inaenda kutimia baada ya safari ndefu sana.