Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka vijana wanaofanya kazi katika sekta ya ujenzi hawatakiwi kufukuzwa kazi kiholela hasa kwa makosa yasiyo ya uaminifu na uzembe.
Waziri Ulega ameyasema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa miundombinu inayojengwa chini ya wizara yake jijini Dar wa Salaam jana.
Ulega alisema amepata malalamiko kutoka kwa baadhi ya vijana wanaodai kuwa wamefukuzwa kazi kwa sababu ya kuwa mstari wa mbele kudai haki za ajira.
“ Ndugu zangu hii tabia ya kufukuza watu kwa sababu ndogondogo ikiwemo kupishana au watu kudai zao haifai. Si tabia ya Kitanzania.
“Watanzania tunafahamika duniani kwa mazungumzo. Tunafahamika kwa kutaniana na kupendana. Kama mtu kathibitika ni mbadhirifu, mdokozi au mvivu hapo siwezi kutetea. Lakini mengine tuzungumze tu,” alisema.
Ulega alisema masuala madogo kama ya uonevu kazini ndiyo matokeo yake hufanya watu kuwa na hasira na serikali zao lakini kwa mambo ambayo yanazungumzika kabisa.
Katika ziara yake hiyo, Ulega alitoa wito kwa wakandarasi ambao hawajakamilisha ujenzi wa barabada kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba kuharakisha kwani serikali haitasita kuvunja mkataba ikibidi
#MillardAyoUPDATES
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amekagua ujenzi wa Madaraja ya dharura Lindi na kuridhishwa na maendeleo yaliyofikia zaidi ya asilimia 88 katika maeneo ya Somanga, Njia Nne na Matandu.
Amesema kukamilika kwake kutamaliza kero za mvua ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikikatiza usafiri kuelekea Lindi, Mtwara na Ruvuma, akimshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuidhinisha fedha za dharura kufanikisha mradi huo.
Ulega ameeleza kuwa Wakandarasi wanafanya kazi usiku na mchana ili Madaraja na barabara za maungio yakamilike ifikapo Desemba 24, 2025 huku baadhi ya madaraja makuu yakifikia zaidi ya asilimia 86 hadi 90.
Viongozi wa Kilwa na TANROADS wamesema maandalizi makubwa yamekamilika na Wananchi wataanza kupita mara mvua zitakapoanza, huku ujenzi wa nguzo na boriti za chuma ukiwa umekamilika kwa kiasi kikubwa.
#MillardAyoUPDATES
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa, amewaomba wakuu wa wilaya nchini kusimamia kwa karibu zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wa awali na msingi ili mwanzoni mwa Januari 2026 waanze masomo kwa wakati
https://t.co/EazC1CUtNE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa katika Jamii kumekuwa na malalamiko makubwa juu ya maadili ya Viongozi wa Umma na ameagiza kuwa Viongozi wote wanaolalamikiwa na Wananchi waitwe wahojiwe ikiwemo yeye mwenywe juu ya tuhuma zinazowakabili.
Ridhiwani ameyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Utumishi wa Umma ambapo amesisitiza kuwa ni vyema taarifa za Watumishi wa Umma zikawa wazi na Viongozi wenye tuhuma wahojiwe na amesema hata yeye aitwe ahojiwe juu ya tuhuma za umiliki wa kituo cha mafuta cha Lake ili ukweli ujulikane na wenye uthibitisho wajitokeze wauseme na ukweli utakapo julikana uwekwe hadharani ili kuweza kuisadia Serikali.
“Nyie wenyewe mnaona maandamano kwa mafano yaliyotokea juzi hapa malalamiko makubwa yalikuwa juu ya maadili ya Viongozi wa Serikali, Tunalalamikiwa Viongozi, kuna mtu mmoja anaitwa Ali Ether ana vituo vyake vya mafuta vya Lake zadi ya 92 vimechomwa vile kwa sababu vinasemwa ni vya Ridhiwani kaniambia sasa fikiria mtu vituo vyake vya mafuta vinachomwa kwa sababu tu wanahisi fulani ndio anamiliki, sasa nyinyi tuiteni anzeni na mimi Waziri wenu.”---Amesema Waziri wa Utumishi Ridhiwani Kikwete.
#MillardAyoUPDATES
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba atembelea majirani zake wakati akielekea kwenye shuguli za Kiserikali
Ujirani mwema hujenga imani na kuimarisha ukaribu na kuelewana kati ya watu.
#MillardAyoUPDATES
When you organize goons to destroy the country but suddenly remember that Canada is nice this time of year. Maria Sarungi, now hiding in Canada after sponsoring chaos, while her minions remain in Nairobi.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuwa Serikali kupitia Jeshi la Magereza limezuia Viongozi wa Chama hicho kumtembelea na kumuona Mwenyekiti wake ambaye ni Tundu Antipas Lissu katika Gereza la Ukonga.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi CHADEMA, Brenda Rupia imeeleza yafuatayo “katika siku za karibuni, Viongozi wa Chama akiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema na Katibu Mkuu John Mnyika wamezuiwa kuingia Gereza la Ukonga kumwona Mwenyekiti Lissu”
“Leo Novemba 30, 2025, Mhe. Mnyika alipofika gerezani akaambiwa na Askari wa Magereza kuwa kuna maelekezo ya kutoruhusu Kiongozi yoyote wa CHADEMA kuonana Mhe. Lissu, hatua hii inaashiria zuio lisilo la kawaida linalokiuka haki za msingi za Mahabusu akiwa Gerezani la kutembelewa na kuonwa na Ndugu na Jamaa zake”
“CHADEMA inachukulia hatua hii kama uvunjaji wa haki za msingi za wafungwa na mahabusu na matumizi ya vyombo vya dola kuwanyanyasa wanasiasa wa upinzani, Chama kinataka Jeshi la Magereza litoe maelezo kwanini wanazuia Mhe. Lissu asionane na viongozi wenzake, Wadau wa ndani na nje ya nchi kufuatilia mwenendo huu hatari kwa mustakabali wa demokrasia na maisha ya Mhe. Lissu, CHADEMA itachukua hatua za kisheria, kisiasa na kidiplomasia kuhakikisha haki za Mhe. Lissu na viongozi wa chama hazikiukwi”
#MillardAyoUPDATES
Kituo Kikubwa cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (East Africa Commercial and Logistic Center) kilichopo Ubungo, Dar es salaam kimeendeleza amshaamsha na kutengeneza mipango ya ushindi kwenye dunia ya Wafanyabiashara Nchini Tanzania na sasa kimekuja na Maonesho makubwa ya kibiashara ya mwisho wa mwaka.
Lengo ni kuongeza fursa za kibiashara na kusukuma mbele uchumi wa Wafanyabiashara Wakubwa kwa Wadogo ambapo Maonesho haya yatafanyika kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 7, 2025.
Zaidi ya Wafanyabiashara 200 wanatarajiwa kushiriki na kupeleka bidhaa mbalimbali zenye bei maalum, punguzo kubwa na promosheni zenye kuvutia mamia ya Wanunuzi ambapo Afisa Uhusiano wa kituo hicho, Sabrina Komba ameiambia Ayo TV kuwa maonesho hayo yataleta fursa za mtandao wa kibiashara (networking), kuongeza mauzo, pamoja na kuonesha bidhaa mpya sokoni.
#MillardAyoUPDATES
📍 Chemba
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir amewasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa VETA za Wilaya.
Mhe. Wanu Ameir ameelezwa kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26 tayari Wilaya hiyo imeshapokea Shilingi bilioni 1.83 kwa ajili ya sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu.
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kuwa baada ya kukamilika kwa asilimia 100 kwa ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), Serikali imehamishia nguvu kubwa katika ujenzi wa njia za kusafirisha Umeme ili kuunganisha Mikoa mbalimbali Nchini pamoja na Mataifa jirani.
Hayo ameyabainisha leo Wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wakati wa ziara ya kukagua uzalishaji wa Umeme katika Bwawa hilo ambapo Waziri Ndejembi amesema hatua inayofuata sasa ni kuhakikisha nishati inayozalishwa inawafikia Wananchi kwa ufanisi.
Amebainisha kuwa ujenzi wa njia hizo za kusafirisha Umeme ni kipaumbele cha Serikali ili kuongeza upatikanaji wa Umeme wa uhakika na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya mijini na vijijini.
Waziri Ndejembi aliongeza kuwa kukamilika kwa miundombinu hiyo kutaiwezesha Tanzania kuuza Umeme kwa Nchi jirani, hatua itakayoongeza mapato na kuifanya Nchi kuwa kitovu cha usambazaji nishati katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Lazaro Twange amesema kwa sasa hakuna tena Changamoto ya Umeme ila Lazima tukubali marekebisho madogo madogo na maingizo mapya ya Wateja wapya na miradi ambayo itahitaji Umeme.
#MillardAyoUPDATES