@azamtvtz Sawa ila kwenye huduma hii ya antena kuna changamoto moja, pindi ndege inapopita matangazo huwa yanakatika. Lifanyieni utafiti na kupata ufumbuzi.
Hongereni watani wa jadi Simba na Yanga kwa ushindi katika michezo yenu ya CAF (Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho) wikiendi hii. Ahadi ya hamasa kwa kila goli bado iko pale pale. Endeleeni kutuwakilisha vyema. Nawatakia kheri.
Wishing you all a happy, peaceful, and joyous Eid al-Fitr. The sighting of a new moon marks the end of our 30 days in fasting and prayers, but calls us for a continuous commitment to compassion, the spirit of sacrifice, generosity, gratitude, and a life of prayer. Eid Mubarak.
Hongereni Simba kwa ushindi wenu dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Upinzani wenu wa jadi uwanjani ni burudani inayowaleta pamoja mamilioni ya Watanzania katika kila kona ya nchi yetu, kwa namna ya kipekee. #KariakooDerby
Nawatakia Waislamu wote Mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Katika mwezi huu wa ibada na toba tuendelee kuiombea nchi yetu amani, upendo, mshikamano, utulivu na haki; nguzo zenye kuleta ustawi zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu. Ramadhan Kareem.
Ramadan Kareem to all brothers and sisters in Islam, in Tanzania and around the world. I wish you a month full of forgiveness, peace and understanding. May Allah accept your fasting and prayers, and shower His blessings upon you. Ameen.
Leo ni miaka miwili tangu tuondokewe na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Mwenyezi Mungu aendelee kumpa pumziko jema na aendelee kuwatia nguvu wanafamilia wote. Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kumuenzi kwa kuendeleza mazuri aliyoyaanzisha.
I convey my heartfelt condolences to President @LAZARUSCHAKWERA and the People of Malawi after Tropical Cyclone Freddy ripped through southern Malawi. Tanzania stands with you during this difficult time and prays for the departed souls, and wishes the injured speedy recovery.