Nimeambiwa Gen Z wamechakaza Ma Bus ya Mwendokasi huko barabarani.
Kituo kilichopona ni Argentina na Manzese.
Sauti zinazosikika ni,
"HATUMTAKI SAMIA, SAMIA MUST GO".
Naambiwa barabarani kulikuwa hakukaliki leo.
Wananchi wamechoka sana kusubiri, kwasasa wako tayari kwa lolote.
MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI.
Juzi RPC wa Mkoa wa Mbeya alitangaza kupitia vyombo vya Habari kwamba Jeshi hilo limewauwa watuhumiwa watatu wakati wakijaribu kuwakimbia Polisi.
Watuhumiwa hao ni Marwa Nyahende, Edward Kayuni na Websta Mwantebele lakin ukweli ni kwamba hao Watuhumiwa hawajauwawa kwasababu ya tukio la kutekwa Shyrose Mahande bali RPC wa Mbeya kaamua kupindisha ukweli makusudi.
Hao Watuhumiwa watatu ambao wameuwawa walikuwa miongoni mwa watu ambao wanaunda kikosi cha Watu wasiojulikana Mkoani Mbeya na wanafanyakazi chini ya Ofisa wa Polisi ambae anaitwa Shabani na RPC wa Mbeya anafahamu kuhusu jambo hili.
Hao watuhumiwa watatu walikuwa waajiriwa wa Serikali kwenye JWTZ na JKT ila kwa nyakati tofauti walifukuzwa kwasababu ya utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wana Familia za marehemu hao anasema kwamba aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, RPC wa Mbeya Benjamin Kuzaga na Coplo Shabani waliwapa hao Watuhumiwa kazi ya kumteka Mdude Nyagali na waliahidi kuwapatia Shilingi milioni 100 baada ya kufanikisha kazi hiyo.
Lakin baada ya kufanikisha kazi hiyo Coplo Shabani aliwapatia shilingi milioni 20 tofauti na makubaliano yao kisha akawaambia pesa nyingine angewapatia baada ya wiki lakin hakufanya ivo.
Baada ya hapo akina Marwa walianza kudai pesa zao kwa nguvu, Shabani akawa anawazungusha mwisho alianza kuwatisha kuwa atapoteza kama wakiendelea kumdai pesa izo, wakamwambia kabla hajawapoteza watatoka hadharani waseme ukweli kuhusu namna Jeshi la Polisi yani RPC, Shabani na wao walivohusika kwenye tukio la Kutekwa Mdude.
Mwanafamilia huyo anasema kwamba juzi kati Coplo Shabani alimpigia simu mmoja wa watuhumiwa hao akamwambia awambie wenzie kwamba wakutane ili aweze kuwapatia kiasi cha pesa kilichobaki ambayo ni shilingi milioni 80 lakin pia kuna kazi nyingine anataka kuwapa wanapaswa kwenda kufanya na kuikamilisha kabla Oktoba 1 ndipo Mtuhumiwa huyo akawapigia wenzake kuwajulisha kwamba wanatakiwa kwenda kukutana na Shabani ili akawape pesa iliyobaki na kuwapa mchongo mwingine.
Lakin tangu walipoenda kuonana na Shabani zilipita siku tatu simu zao zikawa hazipatikani, familia ikadhani huenda wameenda kwenye hiyo kazi ambao Shabani alikuwa amewaitia hadi pale Familia ilipokuja kuona kwenye mitandao ya kijamii kwamba wameuwawa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kutekwa Shyrose.
Sasa turudi miezi kadhaa baada ya tukio la Mdude kutekwa kuna majina sita ya wahusika ambayo yalikuwa yanatajwa sana kwa nyakati tofauti miongoni mwa hayo ni pamoja na hao watuhumiwa watatu ambao RPC wa Mbeya anasema Wamewauwa.
Lakin pia ukiangalia plate number ya hiyo Carina T802 BEY ambayo tulionyeshwa juzi na RPC wa Mbeya kuwa ilikuwa ikitumiwa na Watuhumiwa hao then tukirudi miezi kadhaa nyuma kuna picha ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa imepaki kituo cha Polisi Chunya kuna msamaria mwema kutoka Jeshi la Polisi alitupenyezea kwamba gari hiyo ndo ilitumika kumteka Mdude sasa ukilinganisha plate number ya hiyo Noan na hii Carina ya juzi ni hiyo hiyo moja.
Lakin jambo jingine baada ya Shabani kufanikisha tukio la kutekwa Mdude sasa hivi kapandishwa cheo kutoka kuwa Coplo na sasa ni Special Sergeant
Halafu kapandishwa cheo kinyume kabisa na utaratibu wa Jeshi la Polisi ambapo kawaida Mtumishi yoyote wa Jeshi hilo anapaswa kupandishwa cheo baada ya miaka mitatu Sasa yeye ndani ya miaka mitatu kapandishwa kuwa Coplo na hapo hapo kapandishwa kuwa Special Sergeant means kahongwa cheo ili aendelee kutuumiza.
Kwa mantiki hii RPC wa Mbeya na Shabani wamewauwa hao watuhumiwa watatu ili kufuta ushaidi wa tukio la kutekwa Mdude kwasababu hao watu walitishia kwamba watatoka hadharani kusema ukweli so wakawawahi.
Huyu Mwanafamilia aliyenipa hii taarifa anasema kwamba kwa maelezo ya ndugu yake ambae alihusika kumteka Mdude ni kwamba Mdude bado yupo hai na kwamba Shabani ndo anajua wapi walipomficha Mdude.
Mwisho nawaambia watu ambao huwa wanatumwa kuteka/kupoteza watu Ukiua kwa upanga, utakufa kwa upanga.
Hili taifa litakombolewa 29.10.
Tutakuwa na Tanzania mpya ambayo itazingatia HAKI kwanza. HAKI ndio italeta AMANI & UPENDO.
GEN Z tumepewa hii nafasi haiji kutokea tena. Kila mtu awajibike kwa nafasi yake tutashinda.
Sababu za KUANDAMANA kuidai Tanzania mpya TUNAZO.
Uwezo wa kuandama kuidai Tanzania mpya TUNAO.
Uzuri ni kwamba Sisi tupo Wengi kuliko wao. Namba haidanganyi.
REPOST 200
#SiriNiNamba
#OKTOBATUNATOKA
#TUPOWENGI
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Tarehe 28, October wakianza Kuonyesha Magari yao ya WASHA-WASHA wanafahamu Kabisaa Baadhi ya NYUMBU hwatoenda kwenye Vituo vya Kupigia Kura. itakua imekula kwao.
Mana yake Mwaka 2025 utahesabika kua hauna UCHAGUZI.
Aliepanga Maandamano tarehe 29 October alikua na Akili Sanaa
Zikiwa zimebaki siku 39 tuwe na MAANDAMANO ya kitaifa kukomboa NCHI yetu kutoka mikononi mwa WAKOLONI WEUSI, hizi ndio ishara za ushindi.
1. TLS (CHAMA CHA MAWAKILI) kimeitisha Maandamano ya amani ya siku 2, kupinga kitendo cha Jeshi la polisi kumdhalilisha wakili mwenzao msomi Mahinyila akiwa eneo la MAHAKAMA.
Maandamano ya TLS yakiitishwa ni takwa la LAZIMA kwa kila wakili Tanzania, hapa hadi mawakili wa serikali (WAKINA KATUGA) haya maandamano yanawahusu. Ole wako uingie MITINI, wanayo LOKOO YAO.
2. Wafuasi wa CHADEMA hawa ni wazee wa “NO REFORMS NO ELECTION” —mpaka sasa hii NO REFORMS imeshakufa, masisiemu yameshupaza shingo, kwahiyo tunabaki na NO ELECTION. Mpaka sasa chama haakijasema kitu kuelekea “NO ELECTION”.
Bila shaka viongozi wanafanya TIMMING kama ya kumchinja KOBE. Hawa wakitoa TAMKO kuelekea NO ELECTION lazima nchi nzima itasikia na itafauata maelekezo. Ni swala la muda.
3. WAUMINI WA UFUFUO NA UZIMA. Press ya mwisho ya Askofu Gwajima alitoa kauli kuhusu maaandamano na alionyesha wazi kutuunga mkono tunaohamasisha maandamano. Bila shaka kabla ya 29.10 nae na kanisa lake lenye waumini zaidi ya milioni 3 nchi nzima watakuja na tamko ambalo litaenda kuinganisha taifa kuelekea maandamano yetu ya 29.10.
4. KANISA KATOLIKI. Kanisa KATOLIKI wao walishatoa waraka wao wa PASAKA walisema “KABLA YA UCHAGUZI YAFANYIKE MABORESHO YA SHERIA” serikali imeshupaza shingo na imewapuuzia kama kanisa. Wameendelea kushauri na kukemea ujeuri wa VIONGOZI wetu wa serikali kila siku ila wanapuuzwa.
Hawa nao wanawezaa kuwa na suprise package siku yeyote tujiandae. Kumbuka hili kanisa ni kubwa kuliko TAIFA LA TANZANIA. Walianza kuwepo wao hata kabla ya Tanganyika. Wakiongea hawa ni dunia imeongea.
5. ASASI ZA KIRAIA NA UMOJA WA MATAIFA. Hawa tayari waliunga mkono “NO REFORM NO ELECTION” kwahiyo wao wapo na wananchi. Lolote likitokea walishatoa ushauri ambao ni takwa la WANANCHI.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎