Ushirikishwaji wa vijana katika mambo yanayowahusu ni hatua muhimu katika kutafuta suluhisho la changamoto zao. - Pirosca Mvanda
Sikiliza zaidi mjadala huu kupitia YouTube channel: https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu#CivicTech#YouthParticipation
Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa.
Je vijana wanatumiaje haki hii kikatiba?
Jumamosi iliyopita tuliendesha mjadala kwa kushirikiana na @humanrightstz sikiliza sauti za vijana
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Bado kuna changamoto kubwa tunayopitia kama Taifa ni Ilani za Vyama kutoendana na Dira ya Taifa.
Kutokuwepo kwa maono ya muda mrefu hupelekea kushindwa kutimiza vipaumbele na hili linaenda kuwagusa pia vijana
Yusuph Rajab
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Vijana wanahitaji mazingira wezeshi na kupatiwa ujuzi utakaowakomboa na changamoto ya ukosefu wa ajira.
Pirosca Mvanda, Akizungumza kwenye mjadala
Fuatilia: https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Mahitaji makubwa ya vijana
1. Mitaala bora ya elimu
2. Upatikanaji wa ajira
3. Sera wezeshi.
Ni muhimu serikali ikaangalia namna ya kutatua changamoto hizi kwa ustawi bora wa taifa.
Pirosca Mvanda, akizungumza https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Wanasiasa wengi huwatumia vijana kipindi cha uchaguzi kwa kuwa wana nguvu na ushawishi baada ya kuingia madarakani hawaweki msukumo tena kwa vijana wanaendelea na mambo yao.
Mtazamo na uwajibikaji wa viongozi huwa ni tofauti
Sada Nyenga
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Kipindi cha uchaguzi Vijana wengi huangalia fursa ya kuwa karibu na wanasiasa wakiwa na lengo la kupewa nafasi mbalimbali za uongozi lakini si wote wanafanikiwa.
Sada Nyenga
Fuatilia mjadala https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Katiba ni msingi wa sheria zote na ikiwa kuna sheria yeyote inakinzana na katiba inakuwa batili.
Wakili Yusuph Rajab
https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania inatoa uhuru wa kupata taarifa.
Hii inatoa nafasi kwa vijana na wananchi wote kufuatilia ahadi walizotoa viongozi kipindi cha kampeni.
Wakili Yusuph Rajab
Fuatilia mjadala: https://t.co/3ZaRVHpTkW
Vijana tunapaswa kuwapima viongozi tunaowapa nafasi
Je, wanawajibika ipasavyo kwa ahadi waliozotoa? ili tusirudie makosa ya kuchagua katika chaguzi zijazo
Pirosca Mvanda
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Kijana ana haki wa kupata, kufuatilia na kutoa taarifa.
Kwa msingi huu kijana ana wajibu wa kuhoji ahadi zote zilizoahidiwa na wanasiasa ambao amewapa ridhaa ya kuongoza.
Sada Nyenga
Fuatilia: https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Ongezeko la siasa za ushabiki zinapelekea vijana kuendelea kutumika na wanasiasa tunashindwa kufuatilia sera nzuri ili tuchague chama sahihi.
Fuatilia mjadala huu: https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Vijana wengi bado tuna dhana kuwa siasa haituhusu na hii inapelekea kushindwa kufahamu haki zetu.
Hili linapelekea wanasiasa kututumia tu kipindi cha uchaguzi na baada ya hapo hutuacha - Wakili Yusuph Rajabu.
Fuatilia mjadala: https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Vijana wana maoni yao wanataka kusikika.
Changamoto za ukosefu wa ajira, haki zao za msingi, kwa kiasi kikubwa ahadi za vijana zimesaulika.
Pirosca Mvanda, akizungumza muda huu
Fuatilia mjadala huu: https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Ahadi za Vijana toka uchaguzi mkuu sio tu zimesahaulika bali hata Vijana wenyewe bado hawapewi kipaumbele
Pirosca Luvanda, Kijana Kiongozi akizungumza kwenye mjadala muda huu https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Ahadi za Vijana baada ya uchaguzi, Je zimeshaulika?
Ni mjadala wetu leo utakaruka hewani kuanzia saa 4:00 Asubuhi hii.
Usikose kufuatilia, ukiwa na swali usisite kutuandikia
YouTube Live: https://t.co/3ZaRVHpTkW
#ElimikaWikiendi#HojaZetu
Ni mjadala unaobeba sauti za vijana wengi.
Baada ya Uchaguzi: Je, Ahadi za Vijana zimesahaulika?
Ungana nasi ifikapo saa 4:00 Asubuhi.
Cc @HojaZetu https://t.co/B0l41bvUqq
#ElimikaWikiendi#HojaZetu#CivicTech