TANZIA: Mkuu wa Jeshi la Polisi. IGP Camillus M. Wambura anasikitika kutangaza kifo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Ndwanga Datistan Nsagaje na Konstebo Emmiliana Charles wa Wilaya ya Kipolisi Chalinze vilivyotokea kwa ajali ya gari eneo la Mavi ya Ng'ombe Kijiji cha Mboga, Kata ya Lugoba, Tarafa ya Msoga Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani tarehe 05.03.2023.
Pia anatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa.
Taratibu za Mazishi zinaendelea kati ya Jeshi la Polisi na Wanafamilia.
"Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiweโ
#KitengeUpdates