Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche leo Juni 20, 2026 amesimikwa kuwa Chifu wa Wangoni Mkoa wa Ruvuma.
Heche amesimikwa kuwa Chifu wakati akiwa anaendelea na ziara za chama hicho katika Mkoa wa Ruvuma chini ya operesheni inayojulikana kama #KatibaMpya na #FreeTunduLissu, ambapo ameshiriki tukio la kiutamaduni lililofanyika kwa Wazee wa Kabila la Wangoni.
Katika tukio hilo lililofanyika Songea Mjini, Wazee wa Kimila wa Kingoni wamemtambua na kumvika vazi la U-Chief kama ishara ya heshima, wakimtangaza kuwa Chifu wa Wangoni wa Mkoa wa Ruvuma.
Wazee hao wamesema hatua hiyo ni kutambua mchango wake katika masuala ya ujenzi wa demokrasia na utetezi wa haki za wananchi. Heche amepongeza utamaduni huo, akisema unadhihirisha mshikamano na heshima ya jamii ya Wangoni kwa Viongozi wanaowasikiliza Wananchi.
Tukio hilo limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa chama na Wananchi wa eneo hilo.
#MillardAyoUPDATES
Nowdays uki-mess tu na raia, kila mtu anakuombea baya likukute na wote wanakua upande wa adui yako.
Imagine leo waafrica wengi wanashabikia Mexico na wanataka Mzulu ashenyetwe!!
Taarifa: Ili kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Lissu na struggles zake gerezani, nimeamua kumuiga style yake mpya ya nywele…Sitachana wala kunyoa nywele zangu mpaka atoke jela akiwa HURU✌🏾✌🏾
#LiMwenyekiti#KatibaMpya#FREELISSU
CHADEMA sasa hivi si chama cha siasa tu, ni imani iliyozama mioyoni mwa watu! Baada ya kushiba nondo za maana kutoka kwa viongozi, wananchi wenyewe wamemwaga upendo kwa kuchangia kiasi cha TZS 5,992,255 kidogo kidogo (Tone kwa Tone), kisha burudani ya ngoma za ukombozi ikafuata. CCM ili ipate vibe kama hili, ni lazima imwage mabilioni kusomba wasanii ili kuvuta watu. #PeoplesPower #KatibaMpya #FreeTunduLissu
KAHAMA — SHINYANGA.
Wananchi wameamua kwa uwezo na nguvu zao wenyewe kuchangia harakati za kisiasa za CHADEMA. Wananchi wanasema CHADEMA itaendeshwa kwa gharama za UMMA. TONE TONE tumepata kiasi cha TZS 2,700,700. Changia TONE lako kupitia 0744446969 – CHADEMA HQ
KAHAMA – Shinyanga. Makamu Mwenyekiti CHADEMA @HecheJohn. Homeboy is cooking. Watu ni wengi kama mchanga. Massive, overflowing crowd. This is a clear demonstration of political might—unmatched and irreplaceable. IGA UFE, JARIBU UFILISIKE. 🔥#katibampya#freetundulissu
Unaamka asubuhi unapita mtandaoni unakutana na interview ya Mzee Warioba, Unatabasamu huku machozi yakikulenga lenga kwa imani kwamba kumbe bado kuna watu wenye mapenzi ya dhati kabisa na Tanganyika yetu.
Thank you, Tata Warioba. 🫂
Taarifa kwa umma.
Tunalaani kwa nguvu zote serikali dhalimu kuzuia tume ya haki za binadamu ya bunge la ulaya kuingia nchini kuona ukweli kuhusu hali ya hali za binadamu.
Kama tume yenu ya Chande imechunguza na mnaamini ilichosema, kwanini mnaogopa kuruhusu watu huru kuja kuchunguza?
"Lissu si mnavyofikiria, yuko tayari kufia jela [...] Alisema acheni nikae jela, sijavunja hata rekodi ya Mandela. Hata nikifia jela msiache kukipigania hiki tunachokiamini." - Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Boniface Jacob, amesema kuwa chama pekee chenye uwezo wa kuwasemea Wananchi na kutetea maslahi yao ni CHADEMA.
Jacob ameyasema hayo leo Mei 8, 2026, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Jijini Arusha, ambapo amesema kuwa kipindi ambacho Chama hicho kilifungiwa kwa mwaka mmoja, Wananchi wengi walipitia wakati mgumu kutokana na kukosa sauti ya kuwasemea.
“Sisi CHADEMA tulifungiwa kwa mwaka mmoja, na ndani ya kipindi hicho hakuna mtu aliyeona cheche, kwa sababu msemaji rasmi wa Wananchi anayezungumzia shida za Watanzania ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),” amesema Boniface Jacob.
#MillardAyoUPDATES
#HABARI Marekani imemwekea vikwazo vya kiuchumi rais wa zamani wa DR Congo, Joseph Kabila, ikimtuhumu kufadhili na kuunga mkono waasi wa AFC/M23 wanaopigana mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na kuwashawishi wanajeshi wa serikali kuasi ili kudhoofisha utawala wa sasa.
Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Washington kuwawajibisha wote wanaochochea machafuko nchini Congo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Marekani, mali zote za Kabila zilizopo Marekani zimefungiwa huku raia na kampuni za Marekani zikizuiwa kufanya biashara naye au taasisi zozote anazomiliki kwa kiasi kikubwa.
Marekani imesema vikwazo hivyo vinalenga kumbana kisiasa na kiuchumi ili aache kuhusishwa na jitihada za kuyumbisha serikali ya Kinshasa.
Hatua hiyo inakuja wakati Kabila tayari anakabiliwa na hukumu ya kifo ya mahakama ya kijeshi ya Congo kwa tuhuma za uhaini na uhalifu wa kivita, huku Marekani ikisisitiza kuwa inaendelea kulinda makubaliano ya amani ya Congo na Rwanda yaliyosainiwa mwishoni mwa mwaka 2025. #EastAfricaTV
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, amewasha moto jijini Arusha kwa kukosoa vikali mwenendo wa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akidai kuwa uendeshaji wake unakiuka misingi ya uadilifu na matakwa ya kisheria.
Akizungumza leo, Aprili 30, 2026, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanasheria, Mwabukusi ametoa changamoto kwa mamlaka husika kurekebisha mfumo wa utawala ikiwa kuna hofu ya ushindani wa kidemokrasia badala ya kutumia sheria kuminya wapinzani.
Mwabukusi ameeleza kuwa chama hicho tayari kimefikisha malalamiko yake rasmi kwa mamlaka husika kuhusu mazingira ya kesi hiyo, akisisitiza kuwa haki na uadilifu ndivyo vinapaswa kuongoza mahakama na si shinikizo la kisiasa. Katika kauli yake iliyojaa msisitizo, Rais huyo wa TLS amesema kuwa ikiwa uwepo wa viongozi kama Tundu Lissu unaleta usumbufu wa kisiasa kwa watawala, basi ni vyema mfumo wa vyama vingi ukafutwa nchini na kubaki na chombo kimoja kuliko kuendelea na mchakato unaoonekana kukiuka taratibu za kisheria.
Aidha, kiongozi huyo wa wanasheria nchini ameweka msimamo wa dhati kuhusu uhuru wa TLS, akitoa onyo kali kwa watu au taasisi zinazotoa misaada kwa chama hicho kwa lengo la kutaka kudhibiti msimamo wao au kuwanunua viongozi. Mwabukusi amesisitiza kuwa TLS haitayumba katika kutetea haki za wananchi na utawala wa sheria, na amewataka wadau wanaotoa misaada kwa masharti ya kutaka kunyamazisha sauti ya chama hicho kuchukua misaada yao kwani TLS haiko sokoni kwa ajili ya kuuzwa.
Alimalizia kwa kutoa wito wa kuwepo kwa heshima kati ya TLS, Serikali, na wadau wengine wa maendeleo, akibainisha kuwa jukumu lao kuu ni kuwa sauti ya wasio na sauti na kutetea wananchi bila woga wala upendeleo.
Mwabukusi amesisitiza kuwa wanasheria nchini wana wajibu wa kuhakikisha kuwa sheria hazitumiki kama silaha ya kukandamiza watu, bali kama chombo cha kutoa haki sawa kwa wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.