Wanajeshi wa jeshi la wananchi kukubali POLEPOLE kupotezwa kama kuku ni USALITI kwa Polepole na wananchi wote kwa ujumla.
Hapo nyuma tulikuwa tunapotezwa sisi wakina sativa, walikuwa wanazusha story kuwa tumefumaniwa na wake za watu itakuwa visa vya mapenzi ndiomaana nilitekwa.
Ikaja wakatekwa wakina SOKA na viongozi wa CHADEMA kila kona ya nchi wakasema “Chadema wanajiteka” ili wapate misaada kwa wazungu.
Ikaja Father Kitima (Kiongozi wa KATOLIKI) Akavamiwa na kupigwa nusu ya kumuua ni kwa neema ya Mungu akapona, wamekaa kimya uvamizi ule mpaka kesho jeshi la polisi hawana ripoti juu ya uvamizi ule.
Sasa wamemteka BALOZI MSTAAFU POLEPOLE ambae aliwahi kuwa kiongozi wenu mlipoenda kutoa msaada kama taifa kwenye nchi aliyokuwa anatumika kama BALOZI “MALAWI”—jeshi limekaa kimya na mtekaji anajulikana kuwa ni Afisa wa jeshi “MAFWELE”.
Haya yote yanatokea sio kipindi cha miaka kumi, hapana haya yote ni ndani ya miezi 12 tuu, nchi inanuka damu. Leo kwenye familia 10 lazima ukute familia moja imefikiwa na utekaji.
Wakati wanajeshi wetu wa JWTZ mpo bize kulinda taifa letu kwenye mipaka yetu lisivamiwe na maadui huku ndani WANANCHI mnaowalinda wanapotezwa kama KUKU.
Hatuna msaada wowote zaidi yenu JWTZ (Jeshi la wananchi) tunawaomba mtusaidie kupambana na hawa WAKOLONI WEUSI watatumaliza. Sisi hatuna mafunzo ya kujilinda, ndiomaana tunalipa Kodi tuwalipe mshahara nyie mtulinde.
Kwasasa huko mipakani mnakotulinda bora muondoke, adui yupo ndani tayari anatumaliza. Na mfano mzuri ni aliekuwa kiongozi wenu leo tunaenda siku ya pili hatujui alipo.
TUSAIDIENI WANANCHI WENU.🙏🏿
TUTAKUWEPO🫵🏾😎