Hao Mawaziri Walezi wanatumia fungu gani la bajeti kugharamia majukumu yao ya ulezi wa mikoa na mwaka 2026/27 limetengwa kiasi gani?
Kama tayari kuna Madiwani, Wabunge, Mameya, Wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa wenye majukumu ya kusimamia maendeleo ya wananchi, Waziri Mlezi anaongezea nini?
Waziri Mlezi ana mamlaka gani ya ziada ambayo Mkuu wa Mkoa au viongozi waliochaguliwa hawana?
Anaenda mkoani kufanya jambo gani ambalo Madiwani, Wabunge na Mameya hawawezi kulifanya?
Huyo Waziri Mlezi anawajibika kwa nani kuhusu matokeo ya ulezi wa mkoa?
Kama tatizo ni utekelezaji wa miradi, kwa nini jukumu hilo lisimamiwe kupitia mifumo iliyopo ya Serikali za Mitaa mpaka ngazi ya Mikoa na viongozi waliopo?
Waziri Mlezi akigundua tatizo mkoani kwake ana mamlaka ya kulitatua au kazi yake ni kutoa taarifa kwa mamlaka nyingine?
Kuna performance indicators zipi za kupima kama Waziri Mlezi amefanikiwa au ameshindwa?
Mfumo huu umeanzishwa mwaka gani na kwa sheria, kanuni au uamuzi gani wa Katiba?
Na mwisho, gharama zote za mfumo huu yaani safari, posho, ulinzi, magari na vikao kwa mwaka mmoja ni kiasi gani?