Mkuu wa Mkoa anawezaje kuwa mjinga wa kiwango hiki? Fikiria unaishi katika mkoa ambao RC wake anatengeneza taarifa na kuisambaza katika mitandao ya kijamii kinyume na sheria ya makosa ya mtandao
Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 16: Kutoa Taarifa za Uongo mtandaoni adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Tunajua, Tanzania hawa watawala wapo juu ya sheria za nchi yetu, lakini kwa makosa haya, Albert Chalamila angetakiwa kushtakiwa na akipatwa na hatia afungwe au atulipe faini au vyote kwa pamoja.
Katika nchi ambazo zimestaarabika, Albert Chalamila hawezi kuwa Mkuu wa Mkoa katika Jiji ambalo ni mahususi kimkakati katika uchumi wa Taifa. Ni mtu mwenye uwezo mdogo na hafifu kiuongozi. Hatoshi.
Gavana wa Cairo, Khaled Abdel-Aal Abdel-Hafez au Gavana wa Casablanca, Mohamed M’hidia. Huwakuti wanasambaza vitu vya kipumbavu katika makundi ya WhatsApp kama anavyofanya Albert Chalamila.
Brigedia Mtikila, MMM.
The United States is committed to supporting free and fair elections, including the upcoming elections across Africa. We will not hesitate to consider consequences – including visa restrictions – for those who undermine democracy.