NCHI HII IMEPIGANA NA KUSHINDA KILA AINA YA UBAGUZI
Ameandika Ndugu George Rugambwa, akiwa safarini Dongobesh, Manyara.
Jumatano tarehe 18 mwezi Oktoba mwaka 1961, waliibuka wabaguzi watano ndani ya lililokuwa Bunge la Tanganyika. Ukumbi wa Bunge ulikuwa Karimjee Dar es Salaam. Ukumbi huu Serikali ilipewa na familia ya Karimjee ili utumike kwa shughuli za Bunge, wakati Serikali mpya chini ya Mwalimu Nyerere hapo akiwa Waziri Mkuu ikijipanga kujenga Bunge lake.
Nchi ilikuwa bado haijawa Jamhuri hivyo Mkuu wa Nchi alikuwa bado Malkia wa Uingereza. Mkuu wa Serikali Serikali (Waziri Mkuu) alikuwa Mwalimu Nyerere. Sasa siku hiyo asubuhi likazuka jambo Bungeni, baadhi ya Wabunge Watanganyika weusi walikuwa wanataka Wabunge wenye asili ya Bara Asia na Uzungu waachie ngazi hata kama mababu zao walizaliwa Tanganyika.
Tafakari ya Mwalimu ikampa mwanga kuwa ubaguzi ule kama utashinda basi hautaishia na Ubunge. Utasambaa kama saratani na mwisho pasingekuwapo na taifa. Wakiwa katika mjadala, Mwalimu akasimama na kueleza kuwa wanachotaka kufanya wabunge wanaounga mkono hoja ile ni dhambi kubwa na watakuwa Hitler wadogo (little hitlers) kwa ubaguzi. Akaongeza, ubaguzi ule hautaishia na rangi ya ngozi bali utakuja udini, jinsia na kila aina na mwisho hatutakuwa na nchi. Akasema kwamba Bunge lipige kura, wanaounga mkono hoja kuwa Wabunge wasio Watanganyika weusi wajiuzulu waseme ndio, wasiounga mkono waseme hapana. Demokrasia iamue.
Baada ya hoja ile ya Mwalimu, Bunge likapumzika na kurejea saa kumi na mbili jioni. Kabla ya kupiga kura baadhi wa Wabunge wakapewa nafasi kuchangia hoja akiwemo Meya wa Dar es Salaam, Sheikh Amri Abedi, ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigoma. Sheikh Abeid akaiponda ile hoja ya kibaguzi, akaiita ya kishenzi. Huu ulikuwa msaada mzuri kwa Mwalimu kwani Sheikh Abeid aliheshimika sana kwa kuwa mtu wa msimamo.
Ilipofika majira ya saa moja usiku, Wabunge wote wakawa wamerejea Bungeni. Spika wa Bunge Mheshimiwa Abdulkarim Karimjee akasimama na kuwahoji Wabunge. Asilimia kubwa wakapinga hoja ile ya kutaka kubagua wabunge wasio na ngozi nyeusi na hicho kikawa kifo cha hoja ya kuwataka wajiuzulu. Huenda leo nchi hii ingekuwa nyingine kama tusingeshindwa mtihani ule wa kutugawa.
Kwa Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchi hii imeshinda wabaguzi wa kila aina. Wabaguzi wa kidini, kirangi ya ngozi, kijinsia, kikabila, kikanda na kadhalika. Naandika ujumbe huu na kipande cha historia yetu kukutia moyo unapokutana na wabaguzi wa aina mbalimbali katika kazi yako ya kutumikia nchi yetu. Wabaguzi wengi huwa hawasemi wazi wazi bali hutafuta sababu tofauti tofauti hata za kutengeneza. Soldier on, Madam President. Endelea kututumikia. Tutashinda katika yote.
Ndugu zangu wasomaji, najua mnajiuliza majina ya wabunge vinara walioongoza ile hoja ya kibaguzi kwenye Bunge pale Karimjee. Historia imewaandika kama wabaguzi waliotaka kuigawa nchi ikiwa ndio kwanza inaanza kusimama. Majina yao ni;
1. Christopher Tumbo
2. Aron Msindai
3. Said Mtaki
4. John Mwakangale
5. Richard Wambura
Financial literacy ni muhimu sana kuanza kufundishwa kuanzia shule za msingi. Just imagine kijana ana make deal anapata 1 Billion Tsh , ananunua G Wagon 700M na so other liabilities. Mwingine , the same amount of money ananua hisa/bond , let’s say appreciation yake ni 12% kwa mwaka + compounding interest. Baada ya Miaka 5 , G Wagon itakuwa imeshuka value kwa asilimia 60% up to 70 % wakati huo aliyefanya investment itakuwa na ongezeko la the same 60 /70 % or more , mmoja pesa yake ilikuwa inaongezeka na mwingine alikuwa anazunguka na gari kuishusha thamani maeneo ya Masaki na Mlimani City.
Haya mawazo yamekuwa serious this morning , kwani kuna siku nilinunua kuku nimchinje , mambo yakawa mengi nikasema nitamchinja siku moja, nikamuacha , sasa akataga, akatotoa na vifaranga , sasa sio kuku mmoja tena , wkt natafakari nikaona chupa ya perfume kwenye dustbin , nikasema unajua hii perfume thamani yake that day ningenunua kuku 33. Anyway naaminI ktk maisha bora na mazuri , lakini our obstacles sometimes ni ktk FINANCIAL LITERACY. Tufikirie Pamoja. Nafikiri Reforms Zinahitajika pia zaidi ktk mindset zetu.
IGP , Polisi Wako Kahama Wana Mpango Mbaya Dhidi Yetu Leo , Mkutano Wetu Umetangazwa Wiki Nzima Na Sasa Wameleta Barua Asubuhi Hii Kuzuia Eneo Tulilopo Na Kuzingira Eneo Hilo Na Kuzima Muziki Na Kuanza Kutishia Viongozi Wetu. Tafadhali Epusha Madhara Dhidi Ya Uhuni Wa Namna Hii. Nakutakia Siku Njema.
UZI!! Kama ishawahi kukuta hii situation kwenye shughuli yako ongeza bidii na usiwe comfortable zaidi
Nikiwa ofisini nimekaa nawaza namna gani bora ya kuboresha service kwa ukubwa napokea simu
"☎️ Hello naongea na ofisi ya JOH CABINET?"
Mimi: Ndio mpendwa karibu
Jamaa: Asante samahani mimi natokea mkoa wa Arusha kuna vitu nilikuwa nahitaji kutoka kwako nimepewa sifa zako na kuona bidhaa kwa rafiki yangu nimevutiwa kufanya kazi na wewe
Sasa nahitaji sehemu mpya nnayohamia vitu vyangu vyote vitoke kwako najua ww ni muaminifu utafanya hilo
Mimi: umefika boss
Baada ya muda akaorodhesha bidhaa zake na kuomba utaratibu wa malipu punde meseji ya muamala imethibitishwa QJ42...Umepokea..
Jamaa: kaka sijawahi kukuona ila naamini utafanya kilichobora nakutakia kazi njema. Deal Close
Hii kwangu ilinipa na nguvu kuona mtu anaweza kukuamini kupitia marafiki zake na wateja ni wale wale unavomfanyia kilicho bora basi inakuwa nafasi yako nzuri
Nawashukuru wale wote mnaorecommend JOH CABINET kwa watu wenu wa karibu Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki na kuwainua kwenye kazi za mikono yenu
Namba zetu za simu ☎️: 0710444391
📍Tunapatikana Chang'ombe Temeke,Dar es salaam.
NB: Zipo bidhaa ambazo zipo tayar pia tunafanya kazi kulingana na chaguo la mteja anavyotaka kwa bei nafuu na Ubora wa hali ya juu pia ushauri wa kitaalamu ni bure kabisa🙏.