TUACHE PROPAGANDA JUU YA UHAI WA WATANGANYIKA.
Hakuna Taifa linalotuonea wala kutuingilia mambo yetu ya ndani kinyume na Sheria za Kimataifa.
Yanayotupata leo yanatokana zaidi na ujinga wetu wenyewe, ukatili wetu wenyewe, na kushindwa kuwajibika kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi.
Tumeacha misingi ya utawala wa sheria na kujigeuza kuwa miungu watu wasioguswa na uwajibikaji.
Hatuwezi kuua, kutesa, kushambulia na kupoteza maelfu ya watu halafu tukajificha nyuma ya neno “sovereignty.” Huo siyo ulinzi wa mamlaka ya Taifa; huo ni upotoshaji wa dhana ya sovereignty chini ya Sheria za Kimataifa.
Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa (UN Charter), Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR), Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR), Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (African Charter on Human and Peoples’ Rights), pamoja na kanuni ya Responsibility to Protect (R2P), Mataifa yana wajibu wa kulinda uhai, utu, uhuru na usalama wa wananchi wake.
Sovereignty katika sheria za kimataifa siyo leseni ya Serikali kufanya ukatili dhidi ya watu wake bila kuwajibishwa. Sovereignty ina mipaka ya kisheria na kiutu iliyowekwa na mikataba ya kimataifa, sheria za haki za binadamu, na wajibu wa Mataifa kulinda wananchi dhidi ya mauaji, mateso, upotezwaji wa watu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Pale ambapo Taifa linashindwa au linakataa kulinda haki za msingi za wananchi wake, jumuiya ya kimataifa kupitia taasisi zake halali inaweza kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za kimataifa ili kuzuia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Ndiyo maana hatua mbalimbali zinazochukuliwa na baadhi ya Mataifa ya Ulaya, Marekani, na taasisi za kimataifa kuhusu maafa ya Oktoba 29 dhidi ya Watanganyika ikiwemo mauaji, upotezwaji wa watu, mateso, na vitendo vinavyokiuka misingi ya haki za binadamu zinaweza kuwa na msingi ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa na wajibu wa kimataifa wa kulinda utu wa binadamu.
Tusipokuwa tayari kujiwajibisha wenyewe, tutajikuta tunawajibishwa na jumuiya ya kimataifa.
Ukweli, Haki, Utawala wa Sheria na Uwajibikaji ndiyo msingi pekee wa kulinasua Taifa letu kutoka katika mkwamo huu.
BAK MWABUKUSI
SHAMBANI BUSOKELO
@HildaNewton21@daviddjumbe Nimecheka UFM wamejiunga na DW saa Saba kusikiliza habari za mchana ilipofika taarifa ya MAFWELE wamekatiza taarifa wameweka muziki