Tumeelekezwa kuwa na upendo kwa watu. Hakuna sheria katika Dini inaelekeza kupigana bila sababu zenye tija. Hata Mtumeﷺ amewanasihi wazazi wasiwapige watoto hata wanyama. Vipi kwa binadamu wengine? Sio katika utaratibu wa Dini. Anayeamua kufanya hayo ni yeye mwenyewe asijinasibishe na Dini. Ni sawa na mtu anayefanya ugaidi kwa kivuli cha Uislamu, makosa hayo.