Huwezi kusema uko ktk chama cha siasa cha upinzani lakini unajizuia kumuunga mkono Lissu aliyeyatoa maisha yake kwa ajili ya mapambano hayo.
Wengine wanapoteza muda na pesa za Watanzania.
Ni muhimu wananchi na wanachama wa vyama vya siasa, ikiwemo vyama vyenye wafuasi wengi kama CHADEMA, kuelewa kuwa nguvu ya mabadiliko pia inategemea uwezo wetu wa kuchangia na kujitolea kifedha kwa shughuli za pamoja. Kwa uhalisia, tuna uwezo mkubwa wa kuchangisha fedha ikiwa tutakuwa na nidhamu ktk wajibu huu.
Tatizo kubwa tulilonalo si ukosefu wa fedha pekee, bali ni changamoto ya mtazamo (mindset) na vipaumbele vyetu. Tunaweza kuchangisha mamilioni ya shilingi kwa sherehe na shughuli za kifahari, lakini tunashindwa kuchangia kiasi kidogo kwa ajili ya kusaidia wakati mwingine wagonjwa au kuimarisha harakati za haki na maendeleo.
Hili linaonyesha wazi kuwa changamoto yetu kubwa ni fikra zetu zaidi kuliko hata masuala ya kikatiba. Tukibadilisha mtazamo wetu, tutaweza kujenga nguvu ya pamoja inayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.
Tunaomba kuwe na moyo wa kujitolea kifedha kwa wote wanaotaka kuona haki, maendeleo na demokrasia ya kweli nchini. Inaumiza na kutesa nafsi sana kuomba pesa kwa jamii ambayo inapaswa kujua kuwa kuendesha vyama vya siasa kama CHADEMA ni wajibu wao. Hapa , usiandike Mh tuko pamoja. Changa pesa Mangi !!
“Kumekuwa na majaribio na vitisho kutoka kwa watawala kunizuia nisiongee. Kuna wakati niliambiwa nizime simu yangu, nisiitumie mpaka (wao) watakapo niambia. Nikawauliza, kwa sheria gani? Kuna wakati nilikaribishwa mahali fulani, nikapigiwa simu na watawala, wakasemam mzee usiendee kwenye huo mkutano. Kwanini? Hauna manufaa. Nikawauliza, nani anaamua hayo manufaa? Nikakataa. Wakawafuata watu walio karibu na mimi ili wanishawishi nisiende, nikakataa pia. Mnakumbuka nilifanya mahojiano hapa na Jamhuri? Wakatoa summary, wakasema watachapisha mahojiano yote, neno kwa neno. Baadae Jamhuri wakanieleza wamezuiwa wasitoe yale mahojiano. Kuna viongozi wanaogopa kuzungumza na mimi, wanatuma ujumbe kupitia mbali huko. Marafiki zangu wanaogopa wakisema nitatekwa au kupewa sumu. Nawaeleza mimi ni mali ya Mungu, ndiye atakayeamua lini ananihitaji.”
— Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania.
#FreeTunduLissu hoja zake za kutetea watanzania ndio zimemuweka Gerezani mpaka leo.
Kama mlikuwa hamtaki ushindani wa HOJA mngefuta vyama vingi tuwasikilizage nyie tuu.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa nitakuwa Uyole Jumapili hii pamoja na Viongozi wengine wa ngazi mbalimbali za chama…Ni mkutano wa hadhara na Wananchi wote wa Mbeya Mjini njooni tuendelee tulipoishia…✌🏾✌🏾
#LiMwenyekiti#NyasaMpya#FREELISSU
Siku 34 zimepita tangu kesi ya Uhaini inayomkabili Mhe.
@TunduALissu isimame, hii ni baada ya ombi la mapitio lililofunguliwa na Jamhuri katika mahakama ya rufaa, ambayo halijapangiwa tarehe hadi leo.
WHO TO LEAD THE PROCESS OUT OF THIS DEADLOCK?
It is extremely dangerous to discuss the 29 October 2025 incident as if it were an isolated event. It is part of a continuing pattern of attacks against fundamental rights the right to life, freedom of expression, freedom of identity, and freedom of association. When discussing how best to address the current democratic challenges, we must honestly and independently examine everything that happened before, during, and after the elections.
A critical part of the solution is establishing the whereabouts of the hundreds of our fellow citizens who were abducted, disappeared, or unlawfully detained.
Justice, Truth, and Accountability require answering essential questions: who, how, where, who did what, and why before, during, and after the elections massacre and enforced disappearances.
There are no shortcuts, because half truths are often worse than outright lies.
We must be ready to pursue solutions grounded in justice, truth, and accountability.
BAK MWABUKUSI.
KONGOLE POLISI NA VYOMBO VYA USALAMA KENYA KUKAMATA WATEJAJI HAWA.
Taarifa hii inasambaa toka jana.Watekaji waliokamatwa mmoja ni Mtanzania na Waliyemteka walikuwa wakimwambia wanamleta Tanzania.
Nilitaraji mpaka muda huu tuwe tumejuwa Polisi wetu na vyombo vyetu vya usalama vimefanya au vinatarajia kufanya nini kuwasiliana na wenzetu kwani kwa zaidi ya miaka 11 wao wabaendelea na uchunguzi.
Labda Polisi wetu wako kuandaa kinachoitwa eti ibada ya toba na kusameheana ya madhehebu kitaifa? au wako kuandaa ulinzi wa mechi ya Yanga na Simba?
Kukamatwa kwa wakora hawa kutafungua mwanya wa kumjua mtekaji mkuu wa wanaharakati watanganyika na anakopeleka mateka na ndugu zetu.
HAKI,UKWELI NA UWAJIBIKAJI VITALIPONYA TAIFA.
BAK MWABUKUSI.