Rafiki wa Nyerere aliyesoma civil engineering,akasimamia harusi ya Idd Amin kama best man na mshindi wa tuzo ya Nobel huyu ni Yasser Arafat.1973 tulikuwa nchi ya kwanza Afrika kuruhusu PLO ya Palestina ifungue ubalozi wao hapa.Tukio hili liliwafanya Waisrael waondoke hapa nchini.
Hapa ndipo Mwalimu Nyerere alipozaliwa na eneo hili nililosimama ndipo Kondo la Uzazi(Placenta)ya mama yake ilipofukiwa chini.Safari iliyoanza kijiji cha Mwitongo Butiama,ilifika tamati kwa Mwalimu kuandika jina lake kwenye historia ya dunia ambalo kamwe halitafutika,tunamkumbuka
Chifu Nyerere Burito,baba yake Mwalimu alikuwa na wake 22,hakujua kusoma wala kuandika,hakuwa na dini,akatawala kwa miaka 30 na akaishi miaka 82.Wazungu walimshawishi awe Mkristu,akakubaliana nao kwa mambo mengi ila swala la mkristu kuwa na mke 1 akaligomea,wakashindwa kuelewana.
Mwinyi alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani,yalitokea Mauaji ya vikongwe mikoa ya Mwanza na Shinyanga kwa imani za kishirikina. Waziri mkuu Kawawa akaitisha kikao cha maafisa usalama,Wakuu wa mikoa hiyo na Mwinyi,wakaanzisha “Operesheni Mauaji” ili kubaini wote waliofanya mauaji.
“Tanzania ni ya Watanzania na Watanzania ni Wote. Hakuna mtu mwenye haki ya Kusema Mimi Ndiyo watu wala hakuna Mtanzania mwenye haki ya kusema ninajua linalowafaa Watanzania na wengine lazima wafuate” J. K Nyerere
Mwalimu alikubali mchango na mila za waislam ktk kudai uhuru.Alienda nyumbani kwa Mzee Jumbe Tambaza kukutana na wazee huku mkristu pekee akiwa ni yeye.Wakamsomea dua kisha wakamchinja mbuzi kama sadaka, wakamwambia Mwalimu apite juu yake.Kisha wakesema Gavana Twinning amekwisha.
Kabla Nyerere hajang’atuka nafasi yake ya uwaziri mkuu aliwaita mawaziri wake wakazungumza jambo hilo kwa saa 4, wakajua ni jambo litakalo chukua muda mrefu.Lakini siku iliyofuata Mwalimu alimuita Kawawa akamwambia ”Rashidi wewe ndiye Waziri mkuu,chukua kiti”. Rashidi alishituka
Huu ulikuwa Mkutano Mkuu wa CCM mwaka 1987. Ukitazama vizuri utagundua kuwa wakati huo hakukuwa na Masuala ya kuvaa sare za chama, watu walikuwa wanavaa nguo zao za kawaida kabisa. Je unafahamu majina ya watu hawa wanne walioketi mstari wa mbele?
Barcelona ilikuwa inapiga picha na watoto kwa ajili ya Calender ya UNICEF. Mwaka 2007, Messi akiwa na Miaka 20 akapangiwa kupiga picha na mtoto wa miezi 4 ambaye ni Lamine Yamal. Wakati huo hakuna alijua kuwa wangekuja kukutana ukubwani. Jumapili wanakutana fainali ya World Cup
Japan inaongozwa na mfalme ambaye ukoo wake umetawala kwa miaka 2600+. Mfalme wa sasa hana mtoto wa kiume na hawaruhusu mwanamke kutawala. Hivyo atakapofariki, mdogo wake wa kiume mwenye miaka 60 atarithi, kisha atakuja mpwa wake mwenye miaka 19 sasa. Wanaume kwenye ukoo wanaisha
FIFA imesema wachezaji wote wa timu itakayo shinda kombe la dunia watapewa Pete ya dhahabu pamoja na medali. Hii ni mara ya kwanza kwa washindi wa World Cup kupewa pete hizi. Utaratibu wa Pete huwa upo zaidi kwenye michezo ya Marekani. Hii itakuwa njia mpya ya washindi kujigamba
Martin Chegere aliyekuwa TO form 4 na Form 6, Best Student UDSM na Professor mwenye umri mdogo akiwa na miaka 39 tu, amefanya mahojiano na Gooluck wa Azam TV akasema yeye hakuwahi kuweka malengo ya kuwa TO, bali alikuwa anatumia muda vizuri na alijifunza hilo akiwa Maua Seminary
Kwa sasa uki like Whatsapp status ya mtu, utaona mipira ya football ikidunda namna hii. Kampuni ya Meta imeamua kufanya mabadiliko haya kwa ajili ya tukio kubwa la fainali ya kombe la dunia itakayo pigwa hapo kesho.
Declan Rice amekuwa mchezaji wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza EPL, kuifungia England goli kwenye michuano hii ya World Cup. Hii ndiyo maana halisi ya kuvaa kitambaa cha Captain mkononi, pia ametoa assist kwa goli la pili la Uingereza.
Donald Trump Rais wa USA, Mfalme na Malkia wa Spain, Rais wa Mexico, Waziri Mkuu wa Canada, Waziri Mkuu wa Spain na Rais wa FIFA ni baadhi tu ya viongozi waliopo ndani ya uwanja wa MetLife jijini New York wakitazama fainali ya World Cup 2026.
Fainali ya World Cup 2022 inaendelea kuwa miongoni mwa fainali bora katika historia ya football, mpaka dakika ya 90 tulikuwa tumeshuhudia magoli 4 na mpira ulienda dakika 120. Ile ilikuwa mechi ya aina yake, hatukuwadai chochote wachezaji.
Hatimaye Football imeshinda na dunia nzima imefurahi. Hawa Argentina hawakutakiwa hata kufika hii fainali. Hawa walipaswa kuaga mashindano hatua ya 16 bora kwenye ile mechi dhidi ya Misri. Hongera Spain kwa kuleta utulivu wa dunia.
Brazil na Italy zinaendelea kuwa nchi mbili pekee kuwahi kushinda kombe la dunia mara 2 mfululizo. Messi ameshindwa kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa World Cup na Argentina imeshindwa kutetea ubingwa wake. Usiku unaisha kwa Spain kuwa bingwa na dunia imefurahi.
Argentina imekuwa timu ya kwanza katika historia ya Football kushindwa kupiga shuti hata moja lililolenga goli kwenye dakika 90 za mechi ya fainali ya World Cup. Hawa jamaa walitaka kubeba kombe la dunia kihuni sana.
Kikosi cha Argentina kimejaa wahuni sana, tena World Cup hii wamecheza kwa fujo mnoo. Jana wameonesha udhaifu mkubwa na tabia ambazo sio za wanamichezo. Baada ya kuzidiwa uwanjani na kufungwa, wakaanzisha fujo. Hawa walipaswa wakutane na ile Spain ya kina Sergio Ramos na Puyol.