Jeshi la Magereza limekanusha vikali madai ya kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa kusukumwa na Askari July 30,2025 katika Mahakama ya Kisutu ambapo limesema Lissu alikuwa akielekezwa na kuongozwa kutoka katika chumba cha Mahakama tayari kwa safari ya kurudi gerezani baada ya kuonesha dalili za kukaidi.
Taarifa iliyotolewa leo August 02,2025 na Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi imesema โJeshi la Magereza Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizosambazwa na Mawakili wa, Tundu Antiphas Lissu, kufuatia tukio la July 30, 2025, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutuโ
โTukio hili lilitokea baada ya Mhe. Hakimu anayesikiliza shauri hilo kuahirisha shauri husika na kutoka nje ya chumba cha Mahalama, ikumbukwe kuwa Jeshi la Magereza ni chombo cha Ulinzi na Usalama chenye jukumu la msingi la kuhakikisha usalama wa Mahabusu na Wafungwa wote walio chini ya himaya yake wakiwa ndani au nje ya maeneo ya magerezaโ
โHii inajumuisha kuwalinda dhidi ya madhara yoyote yanayoweza kutokca nje au kusababishwa na wao wenyewe, vitendo vyote vya kiusalama vinavyochukuliwa na Askari Mahakamani au maeneo mengine vinalenga kutimiza wajibu huu wa kisheriaโ
#MillardAyoUPDATES