TSh 500k sio mtaji wa kuleta utajiri.
Lazima uelewe kwamba, Return kwa mtaji mdogo mara nyingi Haipo kwenye hisa.
Haipo kwenye UTT.
Haipo kwenye bond.
Bali ipo kwenye kuongeza uwezo wako wa kuzalisha pesa. Kwa sababu asset yenye return kubwa kuliko zote ni wewe mwenyewe na kipaji
Yaani unakuta kijana ana TSh 500k. Badala ya kujifunza skill mpya au kuongeza kipato chake yeye Anahangaika kutafuta investment itakayomfanya awe Tajiri.
Lazima uelewe kwamba, Return kubwa zaidi kwa kijana mwenye mtaji mdogo mara nyingi haipo kwenye hisa.
Haipo kwenye UTT.
Uzi👇
Akili za Karatasi
Kilosa Mjini Kiwanja Cha 50 kwa 50 ni 2M , Kinatosha Kujenga Room 10 za Kupanga zenye Jiko, Choo na Jiko , Kodi ya Hicho Chumba Ni 100k, Tuseme Ukajenga Room 10 Gharama Ni 22M kwa Hesabu zinazoaminika ,
Ukichukua Hati Ya Hii Nyumba Ukienda Bank Hamna , Hamna Wanakupa 25M, Riba Asilimia 18 , Unaenda kujenga Tena Room 10 kama Hizi hizi ndani Ya Miaka 2 Ushalipa Riba Na Deni Lote 😁 ukirudia Mara 10 👊👊
Issue ni 20M ya kwanza
HAKUNA KITU KINAMALIZA SANA PESA KIMYA KIMYA KAMA TABIA YA KULA OVYO!
Kula kula sana si tabia ndogo. Ni shimo la kimya kimya linalomeza hela yako..
Kuna kipindi nilikuwa natamani maisha yangu yasonge mbele…
→Nilikuwa na ndoto kubwa kichwani.
→Natamani niwe na hela ndefuu...
→Natamani nijenge kitu changu.
→Natamani niishi vizuri.
→Natamani nijibadilike kabisa na kuwa bora.
Lakini kila siku, hela ilikuwa inapotea bila hata mimi kuona inakwenda wapi.
Sio kwa sababu nilikuwa napata pesa nyingi.
Bali kwa sababu nilikuwa na tabia ambazo zilikuwa zinakula hela yangu taratibu.
Na moja ya tabia kubwa kabisa ilikuwa kula kula sana.
Ilikua kila nikihisi stress, nakula.
Nikihisi kuchoka, nakula.
Nikihisi kuchoka kiakili, bado nakula.
Nikikosa comfort, chakula kilikuwa njia yangu ya haraka ya kujituliza.
Na mbaya zaidi nilikuwa nafanya hivi huku bado nina ndoto za makubwa kichwani.
Nilikuwa nataka kubadilika…
lakini tabia zangu za kila siku zilikuwa zinanipinga na kunirudisha nyuma.
Kila siku ilikuwa inaonekana kama kitu kidogo tu:
Mara chipsi kidogo,
Soda kidogo,
Mmmmhhh snack kidogo,
Fast food kidogo,
Napata kamsemo kichwani mwangu “acha nijitreat kidogo tu leo.”
Lakini hizo “kidogo kidogo” za kila siku zikawa zinamaliza hela yangu taratibu.
Hapo ndipo nilianza kuelewa kitu kikubwa:
Hela haimalizwi mara moja tu.
Mara nyingi hufa kwa matone madogo madogo.
Na matone hayo kwa upande wangu yalikuwa cravings, emotional eating, na ile tabia ya kutafuta raha ya muda mfupi.
Nilikuwa si tu nakula nikiwa na njaa.
Nilikuwa nakula ili nihisi poa.
Nakula ili niisahau stress.
Nakula ili nijipe faraja.
Nakula ili nijisikie nimepumzika.
Lakini baada ya hapo, ukweli ulikuwa mmoja:
Tumbo linashiba huku mfuko unazidi kuwa mtupu.
Siku moja nikakaa nikajiuliza kwa uaminifu kabisa:
“Kwa nini hela yangu haidumu, kwani nakosea wapi?”
Jibu lilikuwa wazi.
Sio kwa sababu ya matumizi makubwa sana.
Ilikuwa ni tabia ndogo ndogo za kila siku ambazo zilikuwa zinaiba future yangu kimya kimya.
Ndipo nikagundua kwamba tatizo halikuwa chakula pekee...
Bali tatizo lilikuwa mentality ya kukimbilia comfort kila nikihisi kitu.
Mara ukiumia, unakula.
Ukiboreka, unakula.
Ukichoka, unakula.
Ukijipa moyo, bado unakula.
Na hapo ndipo maisha yako yanapoanza kuishiwa nguvu ya kusonga mbele.
Kwa sababu ukishindwa kudhibiti tamaa ndogo ndogo, itakuwa ngumu sana kwako kushika hela kubwa.
Ndio maana nilianza kujirekebisha.
Sikuacha tu kula kabisa.
Nilianza na kujiuliza.
Kabla sijatumia hela nilikuwa nauliza:
→Hii ni njaa kweli, au ni mood yangu tu?
→Hii inanijenga, au inanipa faraja ya dakika tano?
→Hii ni matumizi, au ni kujituliza kwa gharama ya kesho yangu?
Swali hilo dogo lilianza kubadilisha kila kitu.
Na polepole nikaanza kuona hela kama kitu cha kujenga future,
sio ya kutuliza boredom.
Nikaanza kuwa makini zaidi.
Nikaanza kudhibiti cravings.
Nikaanza kuacha maamuzi ya haraka yasiyo na maana.
Na hapo ndipo nilijifunza somo moja kubwa:
Watu wengi hawakosi hela kwa sababu hawajui kuipata.
Wanakosa hela kwa sababu hawajui kuishikilia ibaki mikononi mwao.
Na kuishika huanza kwenye tabia ndogo ndogo.
Chakula.
Matumizi.
Self control.
Uvumilivu.
Discipline.
Bila kusahau kupanga bajeti.
Kwa kifupi,
Ndoto zako kuhusu pesa zinaweza kuwa kubwa sana lakini kama kila siku unaiachia hela yako iende kwenye cravings za muda mfupi basi utabaki unatazama maisha ya watu wengine yakisonga mbele na wewe ukibali kuwa pale pale.
Mimi nilianza kuona tofauti siku nilipoacha kuishi kwa hisia kila dakika.
Na hapo ndipo hela ilianza kupata maana mpya katika maisha yangu.
Ili kugunda hili wewe anza na kutrack matumizi yako ya kila siku utanipa majibu.
Kwa siku nilikua nakera mpaka 50k!
Kwa mwezi hiyo ilikua ni 1.5M na hapo kukera nimemaanisha matuzi yasio na lazima.
Hivi unadhani hiyo 1.5M ningewekeza mapema kwenye hisa za CRDB ningekua wapi saa hivi??
Hapo najaribu kukuelewesha mambo kwa mifano ili unielewe vizuri zaidi! Anyway unajua nini unatakiwa kufanya. Bye.
Shukrani sana kwa Mentor wangu wa maswala ya kifedha @The_mesha24 kwa kunifungua macho kuhusu hili🙏
Ukiona maisha yanakupiga kila upande…
Kiakili umechoka, kifedha umebanwa, na hata mwili hauna nguvu kama zamani…
Basi usikimbie huu uzi.
Kuna kitu nilikuja kugundua kipindi kigumu nilichopitia…
Na kinaweza kubadilisha kabisa namna unavyojiangalia wewe mwenyewe na maisha yako.
Thread🧵⤵️