Ukijua kudeal na Wajinga wajinga
Umeyaelewa Maisha😀
Maisha si tu kuhusu Pesa au Mafanikio. Ni kuhusu kujifunza kuishi na aina tofauti za Watu bila kupoteza Amani, Heshima, au mwelekeo wako.
Ndugu zangu Mimi Nalala Ila nawakumbusha kuwa
Kuna Umri ukifika Hata Mtu akuite Mbuzi unaitikia tu "Meee" Alafu
unaendelea na Maisha yako.
Ukomavu si kujua kujibu kila kitu, Bali kujua ni Vitu gani havistahili Jibu kabisa. Maana;-
Amani ya Moyo ni Bora Sana kuliko Ushindi.
Ndugu zangu Mimi Nalala Ila nawakumbusha kuwa
Kuna Umri ukifika Hata Mtu akuite Mbuzi unaitikia tu "Meee" Alafu
unaendelea na Maisha yako.
Ukomavu si kujua kujibu kila kitu, Bali kujua ni Vitu gani havistahili Jibu kabisa. Maana;-
Amani ya Moyo ni Bora Sana kuliko Ushindi.
Mafanikio ya Mtu hayategemei Maoni,Chuki,Wivu au kibali cha Watu wengine.Kubali kwamba kila Mtu ana Safari yake
Mafanikio ya Mtu mwingine hayahitaji Ruhusa yako,na Baraka za Mungu hazitolewi kwa kura za Watu
Watu watafanikiwa tu iwe unawapenda au huwapendi
Mungu si Mjomba wako.
Maisha ni Fumbo gumu kulitatua;
Yule unaemuona Tajiri mkubwa, huenda Hana Mtoto na alitoa kizazi.
Yule unayemuona kwenye V8 barabarani huenda anawahi matibabu ya Figo na Moyo muhimbili.
Yule Tajiri mwenye Magari,na Kitanda cha Gharama,huenda analala chini kwa kutimiza kafara🧵👇
Mafanikio hayaridhiki na juhudi za kawaida,yanataka kiwango cha kujitoa kinachovuka mipaka ya starehe.
Kufanikiwa kunahitaji kujitoa kupita kiasi,kunahitaji maumivu,gharama,na nidhamu. Hakuna “discount”.📌
Kwa kifupi tunasema;—
"Mafanikio Yanataka Damu Wewe
Unamwaga Jasho"😅
“May all bad energy sent to me be turned into cash” 💰
“Nataka Dunia inikaribishe kwa shinikizo na mimi nijibu kwa mafanikio.”✌️
Hakuna kilicho na ladha kama mafanikio yanayotokana na kupuuzwa.
Kila aliyekudharau siku ukianza kuingiza pesa anageuka Darasa.📌
Sio lazima uwe mbaya ili ukutane na Ubaya.Wakati mwingine unachohitaji tu ni kuwa bora.
INAWEZEKANA wewe huna shida na Mtu ila Watu wanashida na wewe jitahidi uwe Unasali sana huku Mtaani ni kubaya
Si kila vita inapiganwa kwa nguvu, zingine ni za Roho,Akili,Tabia,na za Ukimya📌
Leo huoni majibu, lakini muda unayaweka wazi. Ukweli hujitokeza, Watu hujifunua, na makosa huonekana bila kelele. Muda haupendelei — unatoa Haki.
Jifunze Kuvipa Vitu Muda,Muda Umebeba Majibu Ya Kila Kitu Kwenye Maisha.Muda Ukifika Utaongea.⏱️
“SISI wengine ni wagumu kusahau, so muwe makini na vitu mnavyotufanyia.”
Matendo ni mbegu. Ukipanda vizuri, utavuna Heshima. Ukipanda vibaya, utavuna Ubaya.
Watu wagumu kusahau mara nyingi hujenga mipaka imara. Sio kwamba wanapenda kinyongo, bali wanajilinda.
Mafanikio huweza kubadilisha mienendo ya mawasiliano kati ya Watu.
Mafanikio yakija, mitazamo ya Watu hubadilika.
Ukweli ni kwamba mara nyingi Mtu akifanikiwa, Watu huanza kuhisi amejitenga.
Sema njia zetu ni ngumu vizuizi ni vingi sana hamna Dili tunafanya kwa wepesi lakini Mungu ni mwema tutafika, ile Ndoto ya kumiliki ka-V8 iko palepale na papa God ata Bless.🤲
Maisha ni magumu, Safari si Rahisi, lakini Imani + Juhudi + Uvumilivu = tutafika.✊
Kila Mwanadamu hupitia Nyakat ngumu.Nyakat ambazo Machozi yanakua Lugha pekee kuelezea Maumivu unayopitia,na kmya kinakua Rafiki wa karibu kulko Watu.Nyakati ngumu zinafka bla kualikwa,Znakufundisha Uvumilivu, zinakuvua Marafik wa Uongo,na kukuonesha Nguvu uliokua huijui juu yako
Pesa si kitu cha kwanza kuliko Afya.
Unaweza kuwa na Utajiri mkubwa,lakini kama Afya yako ni mbaya huwezi kufurahia Maisha wala kutumia hiyo Pesa vizuri.Afya ndiyo msingi wa Maisha
"Wakati Unatafuta Pesa Tafuta Na
Afya,Usipofanya Hivyo Wewe na Pesa Mtashirikiana KUITAFUTA AFYA."
"Tunapitia magumu Mpaka tunaamini Waliokufa wamepumzika"
Wakati mwingine Maisha yanakua na Mateso,Presha na Mapambano makubwa sana,kiasi kwamba Mtu alie Hai anaweza kufikiria kua walioKufa wamepata Pumziko,kwasababu hawapiti tena ktk Shida,Mawazo na Mapambano ya Dunia
Hustler✊
"Ndugu zako wanavyoishi na wewe ukiwa Hauna Pesa, ndio hivyo watakavyoishi na Wanao ukiwa umekufa."
Hali yako ya sasa inapima uhalisia wa Upendo wa ndugu zako. Na kile wanachokuonyesha leo kinaweza kuwa picha ya namna watakavyotendea kizazi chako kesho.
Jitume kufanya Kazi, lakini tumia pia Akili, Maarifa na Mipango mizuri ili Juhudi zako zizae Matunda badala ya kuishia kukuchosha tu.
Akili ndiyo Dira ya Juhudi. Bila Akili, Juhudi zinaweza kukuumiza na kukuchosha tu.
“Juhudi bila Akili 🧠 ni kuutesa Mwili wako”📌
Haujaumbwa Kumfurahisha Kila Mtu Usijitwike Mzigo Usio Kuhusu
Amani yako ya ndani ni muhimu kuliko kukubalika na kila Mtu
Watu Sahihi watakuheshimu kwa ulivyo,si kwa unavyowaridhisha
Usipoteze Maisha yako ukitafuta Approval ya kila Mtu.Jenga Maisha yanayokupa Maana wewe kwanza.