#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 67
Mhe. Lissu : Sasa uasi maana yake nini? Naomba nimsomee tafsiri kutoka kamusi kuu ya kiswahili toleo la 3 ni kitendo cha kuwaondoa madarakani na pia nakusomea Kamusi ya Baraza la Kiswahili la Zanzibar inasema tendo la kuvunja sheria, kanuni au amri.
Kamusi ya kiswahili sanifu imetolewa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam na hii inasema tolea la 2002 inasema uasi hali ya uvunjaji wa kanuni, sheria au amri.
Sasa swali je wewe unafahamu maana tofauti ya hizi zilizopo kwenye kamusi?
George: HIZO TAFSIRI ZIPO VIZURI NAKUBALI.
Mhe. Lissu : Je kuna sheria inayohusu mikutano ya hadhara?
George: Ipo hiyo sheria.
Mhe. Lissu : Je mtu akivunja sheria ya mikutano ya hadhara atakuwa amefanya uasi? Je mtu akifanya mkutano wa hadhara bila kibali? Bila kutoa taarifa polisi
George: haliwi kosa la uhaini.
Mhe. Lissu: Mtu akifanya maandamano bila kutoa taarifa polisi ni kosa la uhaini?
George: Sio kosa la uhaini.
Mhe. Lissu : Hilo neno uasi ni kuvunja sheria?
George: Ni kuvunja sheria za Uchaguzi.
Mhe. Lissu : Safi umekuja vizuri. Twende kwenye Sheria za Uchaguzi.
Anafungua sasa sheria zake za Uchaguzi. Ninayo hapa Sheria ya Uchaguzi wa Rais wabunge na madiwani ya mwaka 2024
Sheria na. 1. Nataka nimuelekeze shahidi sura ya 7 inayozungumzia makosa na adhau yani makosa ya Uchaguzi.
Sasa wambie majaji kosa la kwanza ni kosa gani?
George anasoma -; Makosa yanayohusu uandikishaji wa wapiga kura.
Hili ni kosa la uhaini nitakuuliza yote ili nikienda kunyongwa niseme hakuna swali niliacha kuuliza. Anasema hapa Lissu.
Kosa la Pili ni nini? Kutumia wadhifa kushawishi wasiombe kuteuliwa.
Anasoma makosa yote hapa George kwenye hii sheria. Amefika kosa la saba. Hajasema bado kosa la kuzuia uchaguzi hadi sasa amefika la 10. Anasoma makosa yote 25 yaliyopo kwenye hiyo sheria.
Mhe. Lissu : Sasa katika yote uliyosoma kwenye sheria hiyo kuna kosa la kuzuia uchaguzi Mkuu?
George: Lipo kwenye makosa mengineyo.
Mhe. Lissu : Hebu yaseme.
George anasoma hayo makosa mengineyo sheria inasema makosa mengineyo maana yake ni kusema uongo na adhabu yake ni kulipa faini elfu 50.
Watu wanacheka ๐๐๐๐
Mhe. Lissu : kwahiyo katika orodha ya makosa yote ya Uchaguzi hakuna kosa la kuzuia Uchaguzi ni kweli?
George: Kwa niliyoyasoma hakuna hilo kosa lakini sehemu nyingine linaweza kuwepo.
Mhe. Lissu : Hayo mengine baki nayo mwenyewe mimi nimekupa sheria.
Mhe. Lissu Mtu hawezi kwenda kunyongwa bila mapambano hilo nakuahidi. Sasa twende.
Atakinukisha vibaya sana tena sana. Ulisema hivyo?
George: NI SAHIHI.
Mhe. Lissu Kwenye maelezo yako uliyanukuu hayo maneno "Wanasema msimamo huu unaashiria uasi, tutakwenda kukinukisha sana sana" Je katika maelezo yako yote ulifafanua maana ya maneno TUTAKINUKISHA VIBAYA SANA AU TUTAKINUKISHA SANASANA?
George : sikutafsiri neno moja moja.
Mhe. Lissu : Unafikiri ni rahisi kunyonga mtu.
Haya maneno kwenye hati ya mashitaka kuna mahali hayo maneno tutakinukisha yametafsiriwa?
George: Kwa neno moja moja hayajatafsiriwa.
Mhe. Lissu: Sasa twende kwenye Kiswahili sanifu tukaone maana ya neno KUKINUKISHA anamfungulia KAMUSI hapa.
Tuangalie sasa maana ya neno KIKUNUKISHA. Ni sahihi neno Kukinukisha linatokana na neno NUKA AU NUKIA?
George: NI SAHIHI.
Mhe. Lissu: Kamusi inasema tokwa na harufu mbaya au vunda na Nukia ni toa harufu nzuri. Kamusi nyingine ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam inasema Nuka ni toa harufu mbaya kwasababu ya kuoza. Nukia toa harufu nzuri kama vile marashi.
Sasa kama tulisema tutakinukisha sanasana maana yake kinuke vibaya kitoe harufu mbaya sana si kweli?
George: Kwa unayosoma kwenye kamusi ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Na vilevile kukinukisha kinukie ni kukifanya kitoe harufu nzuri sana?
George: Kwa vile ulisema vibaya basi ni kinuke sio kunukia.
Mhe. Lissu : Je na kukinukisha sana sana ni inaweza kuwa kinukie vizuri sana?
George: Hiyo haiwezekani.
Part 68 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 66
Mhe. Lissu : Matukio ya tarehe 07/04 ulisema Andrew Churu alitoka Makao Makuu ya polisi Dodoma na kuja Dar es Salaam kukuletea vifaa kadhaa na maelezo ya shahidi P?
George: NI KWELI VYOTE ALIKUJA NAVYO. NILIPOKEA.
Mhe. Lissu: Ulimuelekeza akabidhi vitu hivyo kwa Peter Malugala.
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Ulimwambia pia aandike maelezo yake yeye Mwenyewe?
George: Nilisema aandike maelezo.
Mhe. Lissu: Ulisema maelekezo yaandikwe na nani?
George: Sikujali nilisema tu aandike maelezo.
Mhe. Lissu : Kwahiyo hukujali kama anaaandika mwenyewe?
George: Yes sikujali.
Mhe. Lissu : Andrew Churu alijiandikia Mwenyewe?
George: Sikusoma maelezo yake.
Mhe. Lissu : Alijiandikia na kujionya mwenyewe?
George: Mimi sikusoma kiukweli.
Mhe. Lissu: Kesi ya ugaidi husomi mashahidi?
George: Mahamba ndio alisoma hilo sio mimi.
Mhe. Lissu : Baada ya kuwa umeletewa memory card na maelezo ya P ulisema umefahamu kuwa ile video ilikuwa picha halisi?
George: Yes ni kweli nilisema hivyo.
Mhe. Lissu : Je wakati unafikia hiyo conclusion je ulikuwa umeshapata taarifa ya kitaalamu ya Kaaya ambae ni mtaalamu wa forensic?
George: Nilikuwa sijapata hiyo taarifa kabisa.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji kulikuwa na sababu gani ya wewe ulishajua hiyo video ya kweli kwanini ulimpa Kaaya aende akachunguze hiyo video wakati ulishajua ni halisia?
Grorge: Sababu ya meta data lakini kuona kwa macho huwezi kugundua kama video ni halisi. ๐
Mhe. Lissu : Umeiwasilisha hiyo video hapa mahakamani?
George: Sijaiwasilisha mimi kiukweli, niliiona ile siku.
Mhe. Lissu : Kwahiyo kama uliona wewe na majaji wameshaona?
George: Watakuja kuiona huko mbele.
Mhe. Lissu : Je wewe sasa umeleta?
George: Sijaleta.
Mhe. Lissu : Je umesoma report ya hiyo video kutoka kwa mtaalamu?
Grorge: Mimi sikuisoma.
Mhe. Lissu : Je maelezo ya Kaaya ulisoma?
George: Nilisoma ndio.
Mhe. Lissu : Je Inspector Kaaya alisema kwamba walioingiza mtandaoni ni P?
George: Si kweli hakusema hivyo.
Mhe. Lissu anasema ngoja twende kwenye statement yako hapa.
Naomba nimsomee yafuatayo kutoka kwenye maelezo yako wewe mwenyewe. "Mnamo tarehe 06 nilimtafuta kiongozi wa Jambo nikimtaka anipatie picha halisi aliniambia muhusika na kifaa viko Dodoma" haya ni yako?
George: Yes niliandika mimi hapo.
Mhe. Lissu : Haya twendeleee kama unayatambua.
Mhe. Lissu : โbaada ya kuletwa memory card na maelezo ya shahidi kwamba nj yeye aliyerekodi na kuchapisha mtandaoni nilijiridhisha ni video halisi" haya maneno ni ya kwako au sio ya kwako?
George: Ni ya kwangu kabisa.
Mhe. Lissu : Haya ni maneno uliyoandika tar. 08/04/2025 ?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa tuzungumze kuhusiana na Uhaini.
Ulisema kwamba nilielekeza uchunguzi wa uhaini kwasababu Lissu alisema atahamasisha uasi?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Mheshimiwa nimekosea we sio mheshimiwa sasa kuna mahali kokote umetafsiri neno uasi?
George : Kuzuia uchaguzi, vitisho kwa serikali basi sikusema neno moja moja. kwahiyo sikutoa tafsiri ya neno uasi.
Mhe. Lissu : Je katika hati ya mashitaka ninayoshtakiwa nayo kuna ufafanuzi wa neno tutahamasisha uasi?
George: Huo ufafanuzi upo.
Mhe. Lissu : Sasa tuambie upo wapi? Hapo kwenye hati ya mashitaka? Nakusomea hati ya mashitaka ilivyosema? Neno uasi limetajwa mara mbili. Je kuna mahali kokote imeandikwa?
George: Uasi ilitafsiriwa.
Mhe. Lissu : Una akili timamu wewe afisa wa polisi?
George: Nina akili timamu ndio maana ni afisa wa Polisi.
Mhe. Lissu : unaweza kuwa afisa wa polisi nchi hii na ukawa huna akili timamu.
Part 67 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 8, 2025
Jana tuliishia Part 64 so leo tunaendelea na
Part 65
Mhe. Lissu ameshaletwa hapa.
Amepiga Kombati ya Kaki ya CHADEMA.
Shahidi nae amaingia amevaa shati la kanisani kabisa lina maua maua.
Utafikiri amekuja kuongea ukweli vile.๐
Sauti ya Courtttttt imesikika.
Majaji wanaingia na Mh. Lissu anatoa vitu vyake kwenye mifuko yake.
Makabrasha mengi sana na mavitabu.
Majaji wanaandika kidogo hapa.
Anaitwa Karani anasoma jinai na 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Jaji anawaita Mawakili wa Serikali wajitambulishe anaongoza Kazi hiyo Renatus Mkude, Wakili Mkuu wa Serikali akiwa pamoja na wenznake akina Ajuaye Zengeli, Nassoro Katuga, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa. Mshitakiwa yupo na anajitetea mwenyewe. Tuko tayari upande wa Jamhuri.
Jaji anamuuliza Mshitakiwa na Lissu anajibu na mimi niko tayari Waheshimiwa Majaji.
Jaji anamuonya Shahidi kuwa yuko chini ya kiapo. Akumbuke hilo.
Sasa kabla hatujaendelea kulikuwa na lile jambo kuhusu mmoja ya watu uliowaorodhesha alikuwa Na. 12 kwenye orodha.
Tulimwambia Msajili kuwa alifuatilie na uhalisia ni kwamba uhamiaji walisema wanahitaji nyaraka kwa mtu huyo na tumeambiwa Bwana mmoja anaitwa Heche alikuwa analifuatilia.
Kwahiyo nasisi mahakama tutaendelea kulifuatilia pia.
Tuendeleee.
Maswali yanaanza.
Mhe. Lissu : Habari ya asubuhi shahidi
George: Nzuri.
Mhe. Lissu: Mhe Jaji hiyo usiirekodi.
Mhe. Lissu: shahidi kuna mambo nataka tumalize haraka haraka katika maelezo yako ya juzi ulisema ulishika madaraka pia ndani ya hii miaka yako 22 ya upolisi ulikuwa Deputy RCO wa Rufiji 2008.
George: Ni kweli kabisa.
Mhe.Lissu: Ulikuwa Rufiji lini?
George : Nilikuwa kuanzia tar. 01/07/2018 hadi Tar. 17/07/2019.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama Rufiji ni mkoa wa kipolisi au wilaya ya kipolisi?
George: Rufiji ni Mkoa wa kipolisi wenye wilaya nne.
Mhe. Lissu: Ni nani alikuwa RPC wako?
George: SACP Onesmo Lyanga.
Mhe. Lissu : NANI ALIKUWA RCO?
George: Alikuwa anaitwa ACP Faustine Mafwele na mwingine SSP Richard Mchomvu.
Mhe. Lissu : Mafwele huyu huyu?
George: Kimya
Mhe. Lissu : Nilikwambia jana uwe unajibu maswali yangu usiwe na kiherehere.
Mhe. Lissu : Je kipindi kile ukiwa Deputy RCO mkuranga, kibiti, kulikuwa na mauaji mengi?
George : Ni kipindi hicho hicho kweli nilikuwa Deputy RCO.
Mhe. Lissu : JE unakumbuka idadi ya waliouawa?
George: Sikumbuki idadi yao.
Mhe. Lissu : Je unaweza kueleza sababu ya mauaji hayo mengi?
George : Kulikuwa na makosa mengi ya kigaidi ndo maana yalikuwepo.
Mhe. Lissu : Na wewe ulikuwa Deputy RCO na hujui idadi ya watu wengi waliokufa?
George : Ungenipa muda ningekuja na idadi hiyo halisi.
Mhe. Lissu : Wakati unaonyeshwa ile video ulikuwa na police notebook?
George: Yes nilikuwa nayo na hiyo notebook niliitumia kurekodi yale muhimu.
Mhe. Lissu: Naomba ueleze kama uliwasilisha hiyo Police notebook?
George: Sikuiwasilisha.
Mhe. Lissu : Ulizungumza kwa kiasi kidogo juu ya mashahidi waliopatiwa ulinzi wa mahakama?
George : Ndio ni sahihi.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ulihusika kuwahoji hao mashahidi wa siri?
George: Sikuhusika kabisa kuwahoji.
Mhe. Lissu : Ieleze Mahakama kama unawafahamu hao mashahidi wa siri?
George: Siwafahamu kwa majina.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji kama uliona maombi yaliyopelekwa mahakama kuu kuwaombea ulinzi?
George : Sikuyaona kabisa.
Mhe. Lissu : uliona hati ya viapo ya AMIN MAHAMBA NA MOSSIE KAHIMA?
George: Sikuona kabisa.
Mhe. Lissu : Je unajua chochote kuhusu kilichofanya katika jambo hilo la mashahidi wa siri?
George : Mimi ninachojua waliopatiwa ulinzi huo ni raia tu.
Part 66 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 64
Tunaendelea na Cross examination
Mhe. Lissu : Katiba inasema itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama cha siasa?
George Ni kweli.
Mhe. Lissu : Sasa kuhusu Kikwete alikuwaje Mwenyekiti wa CCM?
George: Hilo sijui.
Mhe. Lissu : Je Kinana nae?
George:Nae sijui
Mhe. Lissu : Yusuph Makamba nae katibu Mkuu wa Ccm alikuwa mwanajeshi na alikuwaje kiongozi wa Ccm?
George: Yeye alikuwa Mwanajeshi mstaafu.
Mhe. Lissu : Ni kweli National Prosecution Act kunapokuwa na kosa lolote ambalo adhabu ni kifo DPP anapaswa kujurishwa?
George: Ndio ni kweli inapaswa kuwa hivyo.
Mhe. Lissu : Kati ya tar. 04 na tar. 08 wakati nakamatwa Mbinga kama ulitoa taarifa kwa DPP?
Georgia : Mpaka tarehe 08 nilikuwa sijapeleka.
Mhe. Lissu : Na kwenye maelezo yako pia hujasema jambo hilo?
George : Ndio sijasema.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji Sheria ya NPS niliyoitaja DPP au mawakili wake ndio wenye mamlaka ya kuratibu makosa ya jinai?
George: Ni sahihi.
Mhe. Lissu : Je DPP aliratibu upelelezi ukiwa Chief investigator?
George : kwa siku ambazo mimi nilikuwa kiongozi wa upelelezi sikuwahi kumuona wakili kutoka kwa DPP, hawakusimamia au kuratibu huu upelelezi.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema Mheshimiwa Jaji muda umeenda na wenzetu wa Magereza wanasema barabara ni mbovu kwahiyo tunaomba kuahirisha hadi kesho.
Mhe. Lissu anaulizwa wewe unasemaje?
Mhe. Lissu Wah. Majaji basi tuwakubalie na mimi niende nikale, huyu niko nae sana.
Bado nahitaji kuendelea nae.
Jaji anasema lakini kwa maafisa wa Mahakama jana tuliahirisha kesi hapa mkashikana mashati.
Leo tulikuwa tunawaangalia mnafanya jambo gani hapa, hatutaki kukitumia kifungu cha 114 hapa.
Tusingependa yatokee hayo.
Hakuna Afisa wa Mahakama mwenye immunity. Anajaribu kuwasema mawakili wa serikali.
Kesi imeahirishwa, Tukutane kesho saa tatu asubuhi
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 62
Mhe. Lissu : Kifungu cha 39(2)d lengo la uhaini kionekane kwa maandishi in writing, publication or any overt act?
George: Ni sahihi iko hivyo.
Mhe. Lissu : Neno publish maana yake nini soma kifungu cha 3 cha cyber crime act ili tujue maana ya kupublish?
Georgia anasoma hapa kwanza, Publishing means distributing, transmitting, disseminating, printing or offering for sale. Umemaliza?
George: Naendelea kidogo.
Mhe. Lissu : Swali langu sasa shahidi kwa maelezo yako mwenyewe aliyepeleka kwenye mtandao wa Jambo TV ni nani?
George: mfanyakazi wa Jambo Tv.
Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa ushahidi wako wewe na P aliyerusha maneno hayo ni P?
George: Hapana, aliyerusha ni wewe Lissu na P.
Mhe. Lissu : kama nilichapisha mimi na P kwanini P hajashitakiwa?
Mhe. Lissu anamwambia George tutafika tu mmezoea kuwasingizia watu kwa makesi ya uongo ila Tutafika tu.
Anatafuta maelezo ya P hapa.
Ameyapata, sasa waonyeshe majaji kuwa P alisema Mh. Lissu alitutoa nje ili tusisikie maneno fulani fulani.
Anaangalia hapa Afande George.
Jibu lake tunasubiri muda huu.
George ametoa macho kama mtu aliyejinyonga kwa kamba.๐
Anangalia kwenye maelezo uniambie kama P alisema Lissu alitutoa nje ili kuna maneno tusisikilize.
Anasoma hapa kwamba "walibaki wenyewe Chadema wakatutoa kuzungumza mambo yao"
Mhe. Lissu: Kuna mahali kuna jina la Lissu.
George: Halipo hilo jina, halipo jina la Lissu.
Katuga amesimama ukisoma kifungu cha 170 cha Evidence kama kuna maswali ambayo yanamuonyesha shahidi hafai, anaitwa Nshomile tunaomba haya ya umeiba vyeti haya asiambiwe. Kama kuna tuhuma za kuiba vyeti akafungue kesi.
Mhe. Lissu : basi nitamuita msomi wa polisi.
Mhe. Lissu : Umesema mimi ndie niliyewaalika waandishi wa habari? Ile tar. 03/04.
George : ndio ni wewe ndie uliwaita.
Mhe. Lissu : Je niliwaita kwa njia ya simu?
George: Sijui uliwaita kwa njia ya simu.
Mhe. Lissu: Je barua?
George: Sijui kwa njia gani? Mimi sijui uliwaita kwa njia gani?
Mhe. Lissu : Je nilitangaza magazetini?
George: Sijui mimi ulifanyia wapi?
Mhe. Lissu : Je wewe ni polisi wa aina gani ambae hujui mkutano ulifanyika wapi?
George : HUKUTUALIKA.
Mhe. Lissu : Hujui niliwaalikaje?
George: Sijui njia uliyotumia kuwaalika.
Mhe. Lissu : Je ulimuhoji Katibu Mkuu wa Chadema kuhusu utaratibu wa kualika waandishi?
George: Sikumuhoji.
Mhe. Lissu : Je Amani Gorugwa ulimuhoji?
George: Sikumoji.
Mhe. Lissu ;Ulimhoji Brenda Rupia ulimuhoji kuhusu utaratibu wa kuita waandishi?
George: Nilimuita lakini hakuja.
Mhe. Lissu kwahiyo ulimuhoji?
George: Sikumuhoji.
Mhe. Lissu: Hujui walialikwaje? Hujui nani aliwaalika? Ila unang'ang'ania ni Tundu Lissu ndio alialika.
George: Mimi sijui kwakweli.
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama mimi ni mmojawapo wa wakurugenzi wa Jambo TV.
George: sina uhakika na hilo.
Mhe. Lissu : je mimi ni mmoja wa waandishi wa habari wa Jambo Tv
George : sina uhakika na hilo pia.
Mhe. Lissu : Ni kweli au si kweli hizo video zilipatikana kwenye mtandao wa Jambo Tv?
George: Ni kweli zilipatikana huko Jambo TV.
Mhe. Lissu : je unafahamu mimi nina password za mtandao wa Jambo TV uliwaambia hilo majaji?
George: Siwezi kufahamu kama unazo.
Mhe. Lissu : Kama inawezekana kitaalamu kwa mtu asiye na password kuingia na kuweka chochote?
George: Sijui uliingiaje na uliwekaje hizo video.
Kumbukeni jamani kosa lake wanasema alitoa na kusambaza. Hapa anashughulika na kipengele cha kusambaza. ๐๐๐๐
Part 63 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 61
Mahakama imerejea muda huu saa 9 dkika 25 alasiri.
Imepeigwa sauti ya High Courtttttt
Wameingia majaji.
Karani anasoma namba ya shauri.
Shahidi yupo na Mshitakiwa yupo.
Tunaendelea maswali ya Dodoso.
Jaji anauliza mko tayari.
Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema wako tayari na corum yao ni kama asubuhi ila wamepungua watatu.
Renatus Mkude, Nassoro Katuga, Mwinuka, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa.
Jaji anamuuliza Mh. Lissu kama yuko sawa.
Anamkumbusha shahidi kuwa uko chini ya kiapo.
Tunaendelea.
Mhe. Lissu : katika ushahidi wako ulisema kwanini kwa ufahamu wako maneno niliyosema ni uhaini?
George: Kweli nilisema.
Mhe. Lissu : Ulisema lengo waisikie watanzania na wasio watanzania?
George: Ndio nilisema hivyo.
Mhe. Lissu : Kuita waandishi wa habari ni kosa la uhaini?
George : itategemea?
Mhe. Lissu : soma sec. 39(2) d ya Penal code, kama kuna mahali kinasema kuita waandishi ni kosa la uhaini? Inasema hivyo?
George anaanza kusoma Mhe. lissu amemwambia soma wewe kimya kimya unijibu.
George: Hayo maneno hayapo kwenye hiki kifungu kuwa kuita waandishi wa habari ni uhaini, Hayajasemwa kwenye sheria.
Mhe. Lissu : Je tarehe 08 au 10 kwenye maelezo yako kuna mahali ulisema kuwa mimi kuita waandishi wa habari ni uhaini.
George : Ulisema una kiapo kwenye maelezo yangu niliandika.
Mhe. Lissu : hayo sijakuuliza we sema kwenye maelezo yako kama uhaini ni kuita waandishi wa habari?
George: Hilo hakuna sijaandika hivyo na sikusema hivyo.
Mhe. Lissu : katika kuonesha maneno yangu yalikuwa ya kihaini ni kutoa na kuchapisha taarifa hizo mtandaoni?
George: Ni kweli nilisema.
Mhe. Lissu: hizi video kwa vile ziko mtandaoni je litakuwa ni kosa la cyber?
George: Yes litakuwa hata kosa lingine.
Mhe. Lissu : kosa langu ni kutoa na kuchapisha hii kutoa ni uttering?
George: Yes ndio kingereza chake.
Mhe. Lissu : ninayo cyber crime act kifungu cha 3 cha sheria hiyo sasa soma maana ya neno uttering?
Georgeanapewa sheria aisome ili atuambie maana ya uttering kama ipo sema ipo.
George; Nimeona ipo inasema communication.
Mhe. Lissu : Sasa communication sijashitakiwa nayo.
George : Uttering haipo sawa.
Mhe. Lissu : kifungu cha 39(2)d cha Penal Code soma hayo maneno na uwambie kuna mahali neno uttering limeandikwa kama halijaandikwa usitupotezee muda sema halipo.
George anasoma, anasema neno uttering halipo kiukweli. Hakuna kabisa.
Part 62 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako
๐๐๐น๐ฎ ๐๐๐ฎ๐ธ๐๐น๐ฎ ๐ต๐ถ๐๐ถ ๐ธ๐ฎ๐ฏ๐น๐ฎ ๐๐ฎ ๐ธ๐๐ณ๐ฎ๐ป๐๐ฎ ๐๐ฒ๐ป๐ฑ๐ผ ๐น๐ฎ ๐ป๐ฑ๐ผ๐ฎ/๐บ๐ฎ๐ฝ๐ฒ๐ป๐๐ถ (๐๐๐ฎ๐ป๐ถ๐๐ต๐๐ธ๐๐ฟ๐)๐
๐๐๐๐ผ ๐ผ๐๐ผ
๐Uzi mfupi/๐ง๐ต๐ฟ๐ฒ๐ฎ๐ฑ'๐๐
Kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vimeonekana kuwa na uwezo wa kuongeza hamu
SHUKA NAO๐