Yule Dogo uliyemnyima mchongo leo huko kwao waliuza kila kitu ili asome, amehitimu Wazazi wamejichokea wanamtazama yeye alee wadogo zake pia awasaidie wao.
Yule Dogo ambaye CV yake hukujisumbua kuifungua umeitupa chini, fahamu pesa ya kutoa photocopy hizo karatasi alikopa na mlo amekosa ili iwe nauli kufika hapo ofisini kwako.
Huyo Winga Kariakoo na Mfanyabiashara ndogo ndogo unayemtandika Kodi hatafuti ili akanunue gari bali yeye asife njaa na Wazazi wapate mlo hata mmoja kwa siku.