Katika kura ya kwanza, Rebeca Grynspan wa Costa Rica aliongoza kwa tofauti ndogo, akifuatiwa na Carolyn Rodrigues-Birkett wa Guyana na Rafael Grossi wa Argentina.
Chanzo: Reuters
#JibridNews#BreakingNews#UN#UnitedNations#SecurityCouncil
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa mazungumzo mapya kati ya Marekani na Iran yataanza Jumatatu, baada ya kuamua kusitisha mpango wa shambulio kubwa la kijeshi dhidi ya Iran lililokuwa limepangwa mwishoni mwa wiki.
Chanzo: Reuters
(Pre-Session Meeting) kwa ajili ya maandalizi ya shauri.
Kesi itasikilizwa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kwa njia ya mtandao kwa baadhi ya hatua za awali.
Source: High Court of Tanzania (Court Notice).
#BreakingNews#JibridNews#Tanzania#HighCourt#TunduLissu
Tanzania High Court, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga kuanza kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu kuanzia Aug.10- Sept 7, 2026.
Kwa mujibu wa waraka wa mahakama wa tarehe 31 Julai 2026, kabla ya kuanza kwa usikilizwaji huo kutafanyika kikao cha awali ..
Mahakama ya Rufani ya Tanzania leo imetoa uamuzi katika maombi ya marejeo (Criminal Revision) yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Tundu Antipas Lissu. Kwa mujibu wa uamuzi huo, Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya DPP.
Wataalamu wa afya wanaonya kuhusu ongezeko la maambukizi ya Mycoplasma genitalium (MG), ugonjwa wa zinaa unaozidi kuzua wasiwasi duniani kutokana na kutokuwa na dalili kwa wengi na kuongezeka kwa usugu dhidi ya baadhi ya dawa za antibiotiki.
Source: BBC
#Health#MG#STI
Mwezi kamili "Buck Moon" umeonekana katika maeneo mbalimbali duniani usiku wa Julai 29, ukiashiria kilele cha majira ya kiangazi katika Kaskazini mwa Dunia na kuandaa mazingira ya matukio muhimu ya anga yatakayofuatia mwezi Agosti, ikiwemo Total Solar Eclipse.
Source: Forbes
Saudi Arabia inatafuta kuunda muungano wa kimataifa wa kulinda usafirishaji wa meli katika Bahari Nyekundu, kufuatia mashambulizi yanayoendelea ya waasi wa Houthi dhidi ya meli za kibiashara, kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza na Reuters.
#BreakingNews#SaudiArabia#RedSea
US senet inatarajiwa kupiga kura kuhusu muswada wa vikwazo dhidi ya Urusi, hatua inayofanyika kama sehemu ya kumuenzi marehemu Seneta Lindsey Graham. Kwa mujibu wa Reuters, muswada huo unalenga kuongeza shinikizo la kiuchumi dhidi ya Urusi kutokana na vita vinavyoendelea.
Iran imependekeza mpango wa muda wa usimamizi wa Mlango wa Hormuz (Strait of Hormuz) ambao utaipa mamlaka makubwa zaidi katika kudhibiti njia za meli zinazopita katika eneo hilo.
Kampuni ya Ford imetangaza kurejesha sokoni SUV zaidi ya 80,000 kutokana na hitilafu za kiusalama zinazohusisha kiti cha dereva kujiegemeza chenyewe, jambo ambalo linaweza kuwabana abiria walioketi nyuma. Kwa mujibu wa Forbes, hatua hiyo inaongeza idadi ya magari yanayorejeshwa.
Jeneza la marehemu Seneta Lindsey Graham limewasili katika Capitol Rotunda, makao ya Bunge la Marekani, kwa ajili ya hafla maalumu ya kutoa heshima za mwisho.
#BreakingNews#JibridNews#USA#LindseyGraham#CNN
Waziri Mkuu wa Jimbo la Victoria, Jacinta Allan, ametangaza kujiuzulu kabla ya uchaguzi wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2026.
Kwa mujibu wa Reuters, chama tawala cha Labor kimemchagua Ben Carroll kuchukua nafasi yake, huku kikijaribu kuimarisha nafasi yake.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema haitamaliza kutumia fedha zilizotengwa kwa ajili ya msaada kwa Ukraine hadi mwaka ambao Rais Donald Trump atamaliza muhula wake wa urais, kwa mujibu wa chanzo kilichozungumza na Reuters.
Source: Reuters
#BreakingNews#JibridNews
Wanaharakati nchini India wamefungua kesi mahakamani kupinga matumizi ya teknolojia ya Akili Bandia (AI) kufuatilia waandamanaji wakati wa maandamano makubwa ya vijana yaliyotikisa nchi hiyo.
#BreakingNews#JibridNews#India#NarendraModi#AI
Shule zinazohudumia watoto wa wakimbizi wa Rohingya nchini Malaysia zinakabiliwa na kufungwa huku kukiwa na ongezeko la matamshi ya chuki na taarifa za upotoshaji zinazosambazwa mitandaoni dhidi ya jamii hiyo. Reuters
#BreakingNews#JibridNews#Malaysia#Rohingya#Education
๐ธ๐ป Vyama vikuu vya upinzani nchini El Salvador vimetangaza wagombea wao watakaowania urais dhidi ya Rais Nayib Bukele katika uchaguzi wa mwaka 2027.
#BreakingNews#JibridNews#ElSalvador#Bukele#Politics
PM wa India, Narendra Modi, ametangaza kuundwa kwa kamati maalumu itakayopitia na kufanya mageuzi katika mfumo wa mitihani nchini, kufuatia maandamano makubwa ya wanafunzi yaliyodumu kwa wiki kadhaa.
Source: Reuters
#BreakingNews#JibridNews#India#NarendraModi#Education
Shirika lisilo la kiserikali la Tech Transparency Project limesema kuwa majukwaa ya Facebook na Instagram yameruhusu maelfu ya matangazo ya program za AI za nudify licha ya sera za Meta zinazopiga marufuku maudhui ya aina hiyo
#BreakingNews#JibridNews#Facebook#Instagram
@IAMartin_ Serikali ya ugatuaji ni suluhisho la matatizo mengi maana, mfano suala la ajira ya mtumishi kama mwalimu, nurse, n.k hadi rais atoe kibali. Hatumtendei rais.