Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuufahamisha umma kuwa Serikali ya Marekani imetangaza kuiweka Tanzania katika kundi la nchi zilizowekewa vikwazo visivyokamilika vya kuingia nchini Marekani (partial restrictions and entry limitation).
Tangazo la kuiweka Tanzania katika vikwazo hivyo limetangazwa na Rais wa Marekani, Mhe. Donald Trump kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii mnamo Desemba 16, 2025.
Nchi nyingine ambazo zimewekwa katika utaratibu huo ni: 1. Angola, 2. Benin, 3. Cote dβIvoire, 4. Gabon, 5. Gambia, 6. Malawi, 7. Mauritania, 8. Nigeria, 9. Senegal, 10. Zambia na 11. Zimbabwe.
Kwa mujibu wa Tangazo hilo, Uamuzi huo umetokana na baadhi ya Watanzania kutozingatia masharti ya viza za kuingia nchini Marekani na kupelekea zuwio hilo kufuatia taarifa ya Wakaazi waliopitiliza Muda (Overstay Report) iliyoonesha kuwa kuna kiwango kikubwa cha Raia wa Tanzania ambao wanakaa nchini Marekani kinyume cha Sheria kwa zaidi ya muda ulioruhusiwa na visa zao.
Taarifa hiyo ilionesha kuwa Tanzania imekuwa na kiwango kikubwa cha ukaaji wa zaidi ya muda kwa asilimia 8.3% kwa Visa zote za B-1/B-2 (Visa za biashara na utalii) na asilimia 13.97% kwa Visa za kundi la F, M na J (ambazo ni Visa za Wanafunzi, Mafunzo ya Ufundi, na programu za Kubadilishana yaani Exchange Programmes).
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, viwango hivyo vilitathminiwa kuwa vinazidi hali ya kawaida inayokubalika chini ya sera za uhamiaji za Marekani, na hivyo kupelekea Tanzania kujumuishwa katika kundi la Vizuizi hivyo vya Viza.
Kufuatia hali hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kujadiliana na Serikali ya Marekani kupitia njia za kidiplomasia kati ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania na Wizara ya Nje ya Marekani ili kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
Aidha, Serikali inawasihi Watanzania wote wanaosafiri kwenda nchini Marekani, kufuata kikamilifu masharti ya Viza hizo na kuepuka kuongeza muda wa kukaa kinyume cha sheria ya Viza hizo, jambo ambalo limepelekea Tanzania kuwekwa kwenye kizuizi hicho kusaidia jitihada za Wizara kuondoa Kizuwizi hicho.
#KitengeUpdates
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kuahirishwa kwa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA), ambazo zilipangwa kufanyika leo, Desemba 13, 2025, hadi tarehe nyingine itakapotangazwa.
Jamaa mnajimaliza sana na comments za foreign policy, hata waziri Kombo atakuwa anashangaa π€£π€£ππ.. cyber soldiers hamna limit kwenye JD zenu????
The know example:
Jews sent their reps in priests and elders to petition Pontius to sign Jesusβ crucifixion, they also demonstrated about it. Pontius didnβt see what was wrong with a man calling himself King, But it was rule of the people (democracy). He eventually gave in.
The sexiest part of democracy is that, you seat there knowing it is because majority approved it.
Now, the bitter part is, no matter how unreasonable, they sound to you, you will have to listen to the ruled class and somehow give in their way.
Tricky system to many.