Nashukuru mungu Leo mke wangu amejifungua salama,Tumepata mtoto wa KIUME .
Kwaheshima zote na nimeamua kumpa jina la mtu anaenikoshaga sana naye ni @godbless_lema ,Kwahiyo mtoto wangu anaitwa #GODBLESS_JONASA
CHADEMA imehitimisha salama vikao vyake vya Kamati Kuu vilivyofanyika mjini Kigoma.
Maazimio yaliyopitishwa katika vikao hivyo yatatangazwa rasmi na viongozi wakuu wa chama kwa wakati utakaotolewa.
Kwa sasa, msimamo na kipaumbele chetu ni mambo mawili tu: Uhuru wa Mwenyekiti Tundu Lissu na Katiba Mpya.
Hii ndiyo dira yetu, ndiyo ajenda yetu kuu, na ndiyo mwelekeo tunaopaswa kuusimamia kwa umoja na uthabiti. Tusiache ajenda hizi zipotezwe na mijadala pembeni; tubaki kwenye mstari huu hadi malengo yetu yatimie.
#KatibaMpyaFreeTunduLissu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 230
Anaendelea Mhe. Lissu.
Waheshimiwa Majaji naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo, maombi haya yameletwa kwa lengo moja tu kurefusha mashauri na kuchelewesha kesi ya msingi ili mjibu maombi aendelee kukaa Ukonga gerezani.
Leo ni siku ya 139 kesi haifanyiki na mimi nakaa Gerezani I'm completely innocent but I'm in prison kwa mwaka mmoja na miezi mitatu.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania article 59.b.4 inazungumzia mamlaka ya DPP kutokuchekewesha muenendo wa Mahakama.
Kuzuia Mahakama kuu kuendelea na kesi kwa siku 139 kwa kuleta maombi ambayo wanayajua hayana msingi wowote, kama hii ni kutenda haki then inabidi tutafute tafsiri nyingine ya neno kutenda haki.
Mamlaka ya DPP ni kuwezesha uamuzi wa haki, wa haraka na usiokuwa wa gharama kubwa.
Niko Mahabusu muda wote huo je hiyo ni haki? DPP na Mawakili wake wamepuuza mamlaka ya kikatiba ya DPP kwa maneno yao wenyewe walishabakiza shahidi mmoja lakini haijaendelea kwa siku 139 kwa sababu ya maombi haya.
Mhe. Lissu anasema ombi langu siyo tu Mahakama hii iyakatae maombi hayo siyo tu hilo, maombi yangu Mahakama ya rufani ina mamlaka ya kutoa amri ambazo zingetolewa na Mahakama kuu.
Kwa kutumia kifungu cha 367 cha kutaka mleta maombi anilipe fidia kwa kunifanye nikae gerezani kwa siku 139 bila kesi kuendelea kwa sababu ya maombi yake.
Yakataeni haya maombi na muamuru DPP anlilipe fidia kwa usumbufu wote alionifanyia.
Mhe. Lissu anasema ni hayo tu Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya rufani.
Anasimama Wakili wa Serikali Katuga.
Anasema tumeleta maombi yetu na tumeiomba Mahakama hii tukufu kwamba tumenyimwa haki ya kusikilizwa kwenye huo ushaidi tunaoomba uongezwe, ulikataliwa kabla ya kufika katika hiyo mahakama.
Mjibu maombi ameialika Mahakama hii kwenye proceedings kuanzia pg 391 akizungumzia submission ya uhalali wa notice yetu, tulipata nafasi ya kusikilizwa kuhusiana na notice yetu siyo nafasi ya kusikilizwa kuhusiana na huo ushahidi.
Hatueleweki harafu tunaambiwa tumefanya clever drafting, ushahidi umekataliwa kabla ya kuingizwa, tulisikilizwa kwenye notice tu.
Mjibu maombi anaposema tulipewa haki ya kusikilizwa hakutuelewa kwenye angle gani. Kuirejesha Mahakama hii katika kifungu cha 308 anasema ni kuomba rufaa kwa Mahakama hii sisi tulikuwa tunaonesha walichokifanya na kilichotakiwa kufanyika.
Katunga anaendelea kusema
Sisi hatujaleta maombi haya kuchelewesha kesi tumekuja hapa kuiomba Mahakama iwese kutafsiri Sheria. Kifungu cha 367 kinatumika pale Mahakama inapokuwa imesikiliza kesi na kuona kwamba kesi ni ya kutengenezwa.
Kwa mujibu wa Sheria tunasema maombi yetu ni ya muhimu tunaomba yakubaliwe na yatazamwe na kuita hizo proceedings kuangalia kile ambacho tunakilalamikia.
Jaji anasema basi baada ya kusikiliza pingamizi la awali pamoja na maombi haya tutakwenda kuamua kwanza kuhusu pingamizi la awali kama tutakuwa tumekubali basi itaishia hapo kama pingamizi litakataliwa basi tutaendelea.
Tutawajulisha tarehe ya uamuzi.
Inapigwa Court ya kinyonge ni kama jamaa mchana umepita kama upepo.
Nawatakia Ijumaa njema.
Julai 7, 2026 tukutune barabarani, usihau kubena bango lako lenye ujumbe wa madai yetu ya msingi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 229
Anasimama Mhe. Lissu.
Anasema baada ya kusikiliza hoja za Wakili wa mleta maombi naomba nianze kwa kunukuu maneno ambayo Mahakama hii iliyasema kwenye kesi ya Commissioner General of TRA Criminal case namba 62/2022 pale ambapo maombi ya mdaawa yamezuiliwa na sheria, hawezi kufanya drafting ya kuhadaa Mahakama.
Wanasema uamuzi ulifanyika bila wao kusikilizwa, mgogoro ulianza 19 February 2026 ukurasa 391 wa record, Ugomvi ambao umetuleta hapa ulianza siku Tano kabla ya maamuzi ya Mahakama.
Wakili wa Serikali mkuu Renatus Mkude alisema "waheshimiwa Majaji tuko tayari kuendelea na mashahidi 3 lakini kabla ya kuendelea tuna notice of additional substance of evidence, ambayo imejazwa electronically siku ya Jana"
Katika ukurasa wa 392 Mahakama ikaamua kuwa tuendelee na mashaidi kwanza baadae tutarudi kwenye hoja za notice.
February 20, 2026 ukiangalia ukurasa wa 405-419 utayaona maneno niliyoyasema.
Mahakama ikaamua tumesikiliza sehemu zote kesi hii anahairishwa hadi jumatatu ilikuwa 23 February 2026 kuanzia ukurasa 420 unaonesha hayo.
Mkude akasema wako tayari kuendelea na Katuga akafanya submission in chief pg 421, 423 Katuga akajibu PO, nikafanya rijoinder, pg 428 kuna ruling of the court.
Baada ya submission ya Renatus, submission in chief ya Katuga, rejoinder yangu na reexamination in chief ndipo Mahakama ilitoa uamuzi.
Kwa record hiyo yote nguvu ya kusema hawakusikilizwa wanaitoa wapi?
Kwasababu ya maombi haya leo ni siku ya 139 kesi haiendelei kwa sababu ya uongo wao kwamba hawakusikilizwa.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba ni kweli sasa kwa ushaidi huu wanawezaje wakasema hawakusikilizwa?
Mmemsikia Wakili Katuga akisema Mahakama ilikosea ilipaswa iangalie reasonablity ya hiyo notice, ipokee ushaidi, iangalie competence kisha iamue.
This is an appeal under 6.3 wanayoitaja, it's only clever drafting inayolenga kuiadaa Mahakama.
Iangalie TRA vs New Musoma textile industry kwenye orodha yangu ni kesi namba 7 hawaruhusiwi kuleta malalamiko kuhusiana na hiyo notice kwenye Mahakama hii. Kifungu 6.3 cha AJA mamlaka ya Mahakama hii siyo hiyo wanayoiomba wao.
Ukurasa wa 21 unaonesha mjadala mpana wa ninachokisema sasa na inamaliza huu mjadala, hamuwezi kuanza kuangalia hiki kilicholetwa ni kitu gani mnapaswa kutazama je huu uamuzi ni legal.
Wanasema hawakusikilizwa mnaangalia kwenye record, Je ni kweli hawa watu hawakusikilizwa, hamuendi kwenye huu usikilizwaji ulikuwaje, Mahakama hii haiangalii mambo superficial.
Waheshimiwa Majaji mleta maombi alisikilizwa hivyo ruling ya mahakama ni legal, imeandikwa na Majaji wenye mamlaka baada ya kusikiliza pande zote hata kama hauwafurahishi wanapaswa kukubaliana nao.
Waheshimiwa Majaji waleta maombi hawana hoja yeyote ya maana on the basis of this record. Section 308 ya CPA imetajwa kwa lengo la kuwaalika mtengue kilichoamuliwa na Mahakama kuu nawaombeni msiende huko.
Nitasema kwa kifupi sana juu ya section 308 ya CPA na nini Mahakama ilisema inakataa kuongezwa kwa ushahidi mpya inadeal na Shaidi mpya tu.
Inazungumzia ni katika mazingira gani shaidi ambaye hakutajwa kwenye commital proceedings anaweza kuongeza kwenye trial, mleta maombi hapa analeta ushahidi mpya wa shaidi ambaye ametajwa kwenye commital na siyo shaidi mpya kama Sheria inavyotaka.
Anaendelea Mhe. Lissu
Kwenye uamuzi huu hakuna sehemu ambayo Mahakama imesema ushaidi huo haufai bali imesema ni ushahidi mpya na haufai kisheria.
Hii clever drafting in order to avoid the legal power, kama wanataka kupinga uamuzi huo wasubiri kesi iishe kisha wakapinge uamuzi huo.
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 228
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nimalizie nisiwachoshe.
Hoja yangu inahusika na maamuzi ambayo hayamalizi kesi, kesi bado ipo na tutakapoenda kwenye substance nitawaoneshe Majaji kwenye hicho walichokileta wao wenyewe ambavyo kesi bado inatusubiri.
Kwa bahati mbaya wametupotezea muda sana hivyo nawaombeni Waheshimiwa Majaji mkatae maombi hayo.
Anasimama Katuga anasema Waheshimiwa Majaji maombi yetu yameletwa chini ya kifungu cha 6 kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya mamlaka ya rufaa ya mahakama hii na kanuni ya 65 kanuni ndogo ya 1. Waheshimiwa Majaji ukisoma notice yetu inataja kifungu cha 6 cha Sheria ya mamlaka ya rufaa ya mahakama hii, Waheshimiwa Majaji lalamiko la mjibu maombi lisingekuwepo kama angeipitia kanuni ya 48.
Jaji anamwambia Katuga ulishamaliza usilete jambo jipya nenda moja kwa moja kwenye maombi.
Katuga anaendelea
Waheshimiwa Majaji maombi yetu yamejikita kuiomba Mahakama hii tukufu iweze kuangalia uhalali na usawa wa muenendo wa shauri lililoko mbele ya Mahakama kuu.
Maombi haya yametokana na mzizi wa upande wa Jamhuri kuleta notice ya kuongeza ushaidi ambao haukusomwa wakati wa commital na upande wa Jamhuri ulifanya vile kuendana na kifungu cha 308 cha CPA, kifungu hiki Waheshimiwa Majaji kinaweka zuio kwamba hakutakuwa na ushahidi ambao utaongezwa Mahakamani kama ushahidi huo haukusomwa hautaruhusiwa kuongezwa unless upande wa Jamhuri utatoa notice ya kuongeza ushaidi huo.
Tunatakiwa kutoa notice ili mshitakiwa asikutane nayo by surprise, kifungu hicho kinaitaka Mahakama wakati inafanya reasonablity ya notice ifanye vitu gani.
Mahakama wakati inatakiwa kutambua reasonablity ya notice inapaswa kuzingatia kifungu cha 308 kifungu kidogo cha 3 inatakiwa kuuchambua ushaidi wenyewe.
Naona Job Mrema ni kama kambonyeza Katuga ameinama sijui wanaongea nini na wenzake,
Halafu sio mara moja kila baada ya sentence kadhaa vikao vinakuwa vingi.😤
Anaendelea Katunga
Mahakama ilienda kuangalia huo ushahidi katika ukurasa wa 431 wa muenendo wa Mahakama kuu na kuita ni ushaidi mpya umekusanywa baadae na hivyo wamekataa.
Ushaidi unakatakiwa pale ambapo unakuwa umefikishwa Mahakamani baada ya kuwa umepimwa ndipo Mahakama inaamua uingie au usiingie, upokelewe au usipokelewe lakini hauwezi kuamuliwa wakati unakuwa introduced.
Kifungu cha 308 kimetoa nini Mahakama inafanya, ndo maana kwenye maombi yetu tunasema tumenyimwa haki ya kusikilizwa in relation na huo ushahidi.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba, maana ya hii haki ya kusikilizwa ni kumpa mtu haki ya kumsikiliza full kwa utimamu ndo maana Mahakama ina vitu vitatu vya kupima.
Ushaidi unapimwa unapokuwa umefika Mahakamani, kusema ushaidi ni mpya usiletwe ni kuukataa ushaidi kabla hata haujafika Mahakamani.
Mahakama hata haikuusikia ushaidi lakini ikaenda kusema ushaidi huo ni irrelevant.
Utaratibu wa proceeding ulikuwa umekiukwa na ukiukaji ambao unaenda kwenye shauri yenyewe na ndiyo maana upande wa Jamhuri tukaona kwa busara zenu muangalie hizo proceedings hatuwezi kuendelea na hizo illegalities.
Anaendelea Katuga
Tunataka Mahakama iangalie ni kwa namna gani kwa muda gani ushaidi unaangaliwa na kuwekwa kama ushaidi.
Kwenye kifungu hakuna sehemu tuliposema Mahakama iende ikaupime huo ushahidi ilikuwa ni notice tu, ushaidi kuja Mahakamani na kufukuzwa kabla ya kusikilizwa huko ni kutunyima haki.
Ni vigumu kupima ushaidi ambao hauko hata mahakamani.
Ukurasa wa 431 wa proceedings naomba muuangalie waheshimiwa Majaji, jambo hili lilikiuka taratibu za mienendo ya proceedings.
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya rufani tunaomba maombi yetu yaangaliwe na yakubaliwe.
Waheshimiwa Majaji ya kwetu ni hayo tu.
Part 229 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 227
Anasimama Wakili wa Serikali Mrema
Anasema naomba kuongeza kidogo kwenye mawasilisho yaliyofanywa na Wakili mkuu wa Serikali Katuga, naomba kuongeza yafuatayo.
Waheshimiwa Majaji hii obligation inayowasilishwa mbele ya mahakama ya rufani lazima iwe na uwezo wa kuondoa shauri hilo lililoko mbele ya Mahakama hii, nikirejea shauri alilolilejea, shauri la DPP dhidi ya Mohammed Ussi naomba kuialika Mahakama hii kwenye kifungu cha 5 kifungu kidogo cha 2.
Mleta maombi amefanya reference kwa kifungu ambacho kimepitwa na wakati it's not applicable.
Kifungu hiki kukihusianisha na kesi ya Mohammed Ussi na kukileta kwenye Sheria ya sasa it's not applicable.
Kifungu cha 8 kinazungumzia mashauri ya madai, swali la kujiuliza ni je shauri hili ni la madai.
Jaji anawasha kipaza anauliza. Katuga ulisema Mrema anaongezea sasa mbona anarudia yaleyale.
Watu wanacheka😂😂😂😂😂
Jaji anamwambia Mrema aendelee ila asirudie mambo ambayo tayari Katuga ameongea.
Mrema anasimama anasema waheshimiwa Majaji ni hayo tu.
Watu wanacheka maana ni kama alichosema Jaji kimemto kabisa Mrema kwenye mood.😂😂😂😂
Anasimama Mhe. Lissu
Waheshimiwa Majaji naomba mniruhusu nijibu hoja za waleta moambi.
Wanacholalamikia siyo order wanalalakikia findings.
Waheshimiwa Majaji wanacholalamikia wamekileta wenyewe kwenye hati yao ya maombi hicho kiko kati ya ukurasa wa 428-431 wanalalamikia rulling, uamuzi.
Uamuzi wanaoulalamikia unajadili ushaidi wanaotaka kuuingiza, na Mahakama ikajadili ushaidi huo kwamba ni kinyume na Sheria hautaingizwa.
Kama wasingekuwa wanalalamikia hii ruling wasingeileta mbele ya Mahakama yako. Finding is not similar to a decision.
Waheshimiwa tuasume Mawakili hawa wako sahihi finding is similar to decision, tuangalie Mahakama inasema nini juu ya aina hii ya ushaidi, Mahakama ikasema ni kinyume na Sheria hauruhusiwi kuingia.
Mawakili waleta maombi wameleta kesi muhimu sana kesi ya Peter Michael Madeleka, kuna mahali katika kesi hiyo ambako Mawakili wa Serikali wamepakimbia kama ukoma, ukurasa wa 9 Mahakama ilisema hivi kuhusiana na hicho kifungu hayampi mamlaka ya kuimove Mahakama.
Mhe. Lissu anawambia Mawakili wa Serikali ahsanteni sana kwa kuleta kesi ya Madeleka.
Watu wanacheka 😂😂😂😂 maana akina Katuga wameleta kesi ambayo badala ya kuwasaidia kumkandamiza Mhe. Lissu yenyewe ndo imekuwa msaada kwa Mhe. Lissu.
Anaendelea Mhe. Lissu
Mamlaka ya Mahakama ya rufani kuitisha Suo moto ni mamlaka yake yenyewe haiwezi kuwa moved na waleta maombi.
Kama Mahakama haijaiona yenyewe haiwezi kuletewa maombi.
Wanasema nisiwafundishe lakini mkiangalia record waliandika barua, walileta maombi kisha wakaandika barua wanataka kuimove Mahakama.
Katuga amesema maombi yao wameyaleta under 6.3, Waheshimiwa Majaji nawaomba muangalie maombi hayo kama kuna sehemu wametaja kifungu hicho. In their notice of motion hakuna sehemu wametaja ni 6 ipi kati ya vifungu 6 vya Sheria hiyo hawawezi kuja hapa kuzungumza kitu tofauti na maombi yanavyozungumza.
Nirudi kwenye hoja ya Job Mrema, mmealikwa Majaji kukubaliana na hoja kwamba Sheria imeshabadilika ni vifungu tofauti, Waheshimiwa Majaji mimi nina revised Act of 2023 inasema section 5 haina marekebisho ya kabla ya 2023 kwa hiyo hii hoja ya kwamba kuna Sheria imebadilika ni vitu tofauti ni hoja ambayo nachelea kusema haina mashiko.
Waheshimiwa Majaji wakili ametaja rule 48.1,
Waheshimiwa Majaji inazungumzia PO must have a capacity to dispose of application na kwa maana hiyo anasema pingamizi langu halina uwezo wa kumaliza madai,
Je kwenye hoja ya kwangu hii kwamba maombi haya hauruhusiwi kwasababu hayana uwezo wa kuyafuta maombi kama inasema imeletwa chini ya kifungu cha 8.2.d? hakuna hoja hapo.
Part 228 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 226
Anaendelea Mhe. Lissu.
Waheshimiwa Majaji uamuzi uliotolewa na Mahakama ya rufani katika kesi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA na bodi ya wadhamini wa CHADEMA vs Saidi Issa Mohammed na wenzake inasema kwamba kama mdaawa (Mleta maombi) analeta maombi mwenyewe ni yale yaliyoko kifungu cha 6 kifungu kidogo cha e, maombi mengine ni Mahakama yenyewe ndiyo inaamua bila kusukumwa na yeyote au kuletewa maombi yenye hati ya kiapo.
Waheshimiwa Majaji kwa vyovyote vile maombi hayo hayako halali mbele ya mahakama hii kwani hayakuletwa katika utaratibu wa kisheria kwani Mahakama hii haijaamua maombi haya yaje yenyewe Suo moto kwa hiyo Mahakama isikubali kusikiliza maombi hayo kwasababu ambazo nimezisema.
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa waheshimiwa Majaji sijui kama mnaniruhusi niendelee au wajibu kwanza.
Jaji anasema Jamhuri wajibu kwanza PO kisha tutaendelea.
Anasimama Wakili Katuga anasema Waheshimiwa Majaji tukirejea mapingamizi yake ya awali yameletwa chini ya kifunga cha 8.2.d hiki ni kifungu mahususi kwa mashauri ya madai.
kifungu hiki kilikopwa kikatumika kwenye madai kwenye mashauri ya rufaa, hata kama Mahakama yenu tukufu kwa rejea hizo za Mahakama hii ikakikopa kitumike kwenye maombi yetu haya bado tunasema kwamba maombi yetu yako sahihi mbele ya mahakama hii tukufu tofauti na kile ambacho mjibu maombi amekileta kama pingamizi la awali.
Maombi yetu yameletwa chini ya kifungu cha 6 specifically kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya mamlaka ya Mahakama. Kanuni ya 65 na kanuni ya 45 ya kanuni za Mahakama ya Rufani inasuport maombi yetu.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa Majaji ukiyasoma maombi yetu kwenye notice of motion hakuna sehemu yeyote tunayoiomba Mahakama hii tukufu ipitie order ya Mahakama au uamuzi wa Mahakama, pale mwisho tunasema Mahakama idiscuss kukataa ushahidi hatujazungumzia kukataa notice, sisi tunazungumzia kuuchambua na kuukataa ushahidi.
Hakuna sehemu kwenye maombi haya tunalalamikia order, Mahakama yenu itaona kwamba pingamizi la mjibu maombi limekuwa mislead hakuconsue sawasawa maombi yetu.
Pale ambapo neno or litatumika kwenye Sheria yeyote maana yake maneno haya hayako similar yanatumika tofauti, Waheshimiwa Majaji nimewarejesha humu muweze kukitafsiri kifungu cha sita. Haya maneno yanatakiwa yatafisiriwe tofauti hayaendi pamoja ama hayategemeani, inaweza kuwa kimoja wapo kati ya haya.
Kama mahakama yenu imekikopa kifungu cha 8.2.d kinazungumzia katazo la decision or order ndo hauwezi kuziombea appeal or revision.
Sasa tunapata wapi nguvu za kuleta pingamizi kwa tafsiri hiyo tunaiomba Mahakama hii ikaangalie maana ya maneno haya.
Waheshimiwa nawarejesha kwenye kamusi kwa sababu nayo ni kati ya vitu vinavyopaswa kutumika kutafsiri Sheria. Katika ukurasa wa 129 kamusi inadefine order ni nini?
Kwenye application yetu hakuna sehemu tumeombea decision or order, kwenye kifungu cha 8 hata kama kimekopwa hakiwezi kucocer maombi yetu.
Mahakama yenu ilishawahi kuiamulia hili kwenye kifungu 394 cha CPA, katika kesi ya Peter Michael Madeleka dhidi ya jamhuri.
Kutaja kitu fulani means exclusion ya kitu kingine, kitendo cha kifungu cha 8 kutaja findings and order means haijatuzuia kwa maana hiyo findings hapa haijazuiwa kwa maana hiyo tunachotaka kuiambia Mahakama yako ni kwamba ule ushahidi ulikataliwa kabla ya wakati wake.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa naomba niishie hapo kwenye hilo ili tusiende mbali kwa kuyasema hayo mtaona kwamba kesi ambazo mshitakiwa amewapitisha ni distinguishable kwenye mazingira yetu.
Hii kauli ya kwamba hatuna mamlaka ya kuomba Mahakama iitishe ‘Suo moto’ sisi tunasema mamlaka tunayo.
Katiba anasema naomba Mrema anisaidie anayo nyongeza.
Anasimama Wakili wa Serikali huyu anaitwa Job Mrema anakipara kama Mrema wa ubwabwani, sijui na yeye huwa anakunywa visungura kama mwenzake, anyway
Part 227 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo July 3, 2026
Last time kwenye ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu tuliishia part 224 so leo tunaendelea na -;
Part 225
Mheshimiwa Tundu Lissu anaingia ndani ya chumba cha mahakama, ukumbi namba 01 wa Mahakama Kuu.
Anaonekana mwenye tabasamu na furaha usoni kwake kama ilivyo siku zote.
Upande wa Jamhuri wapo kama kawaida yao
Inapigwa Court…..
Jopo la Majaji watatu wanaingia,
Kesi inatajwa
Anasimama Wakili wa Serikali anajitambulisha jina lake Ajuaye kisha anatambulisha Mawakili wenzake.
Jaji anaamuliza Mhe. Lissu kama yupo tayari
Mhe. Lissu anasema yuko tayari kuendelea.
Kama kawaida yao anasimama Wakili wa Serikali Katuga kuweka pingamizi.
Mhe. Lissu anapendekeza maombi yake ya sikilizwe kwanza ndo pingamizi lao lijibiwe.
Majaji wanasema tuanze kwanza kusikiliza PO, kisha taratibu nyingine zitafuata.
Anaanza Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji kesi hii inatokana na maombi namba 19065 ya mwaka 2025, Juu ya maombi ya kuongeza ushahidi katika muendelezo wa kesi, uamuzi wa tarehe 24 February 2026 wa Mahakama Kuu wa kukataa kuingizwa kwa ushahidi mpya.
Waheshimiwa Majaji uamuzi wa February 24, 2026 ni uamuzi mdogo, uamuzi ambao haujamaliza shauri na kwa mantiki hiyo kisheria kabisa haupaswi kukatiwa rufaa au pingamizi.
Waheshimiwa Majaji wa rufaa, Mahakama hii katika kesi ya Mkurugenzi wa Mashitaka dhidi ya Mohammed Mussa Ussi criminal appeal namba 521 ya mwaka 2023 Mahakama ikiwa imeketi Zanzibar ilisema msingi wa kukataza rufaa ama mrejesho (revision) ya jinai msingi wa hiyo hoja ni kifungu cha 8.2.d kutokana na marejeo ya mwaka 2023 mahakama hii ilisema uamuzi huo hauwezi kukatiwa rufaa kwani ni uamuzi usiomaliza shauri.
Anaendelea Mhe.Lissu
Kesi ambazo nimeziwasilisha mbele yenu waheshimiwa Majaji zinazungumzia uamuzi mdogo ni wa aina gani na uamuzi unaoweza kutolewa kama uamuzi wa mwisho unaoweza kuombewa revision ni wa aina gani.
Uamuzi unaomaliza kesi na kunyima haki za wadaawa ndiyo unaopaswa kukatiwa rufaa, uamuzi unaokuwa treated as the final order ndiyo unaomaliza haki za msingi za wadaawa lakini kama uamuzi haufanyi hivyo hauwezi kukatiwa rufaa.
Sasa waheshimiwa Majaji baada ya kuwapitisha kwenye kesi hizo nirudi kwenye hoja yangu ya msingi je uamuzi wa February 24 mwaka huu ulimaliza kesi hii?
Kama ni hivo ulimaliza kesi hii na kwamba Sasa hivi sina kesi ya uhaini basi hoja yangu haina msingi na maombi haya hayawezi kusikilizwa.
Hoja yangu waheshimiwa Majaji ni kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu wa February 24, 2026 haukumaliza kesi namba 19065/2025 na kwasababu haukumaliza maombi haya ya revision yanakatazwa kuletwa Mahakama ya Rufaa.
Anaendelea Mhe.Lissu
Waheshimiwa Majaji uamuzi huo unasema nini, ili tujue kama ulimaliza kesi lazima tuusome huo uamuzi unasema nini.?
Rulling yenyewe iko ukurasa wa 405-432, kwenye ukurasa wa 431 paragraph ya mwisho waheshimiwa Majaji mtaona Mahakama ilichokiamua.
Kilichokataliwa kupokelewa na Mahakama ni notice of additional substance of evidence, Mahakama Kuu haikusema kesi haitaendelea. Mahakama kuu ilitoa Mwongozo haikutoa uamuzi wa mwisho wa kesi, uamuzi wao ulikataa subodinate issue.
Waheshimiwa Majaji ushaidi mwingine huko kwenye maombi yenyewe yaliyoletwa. Mahakama inasema ilijadili na kukataa notice yao ya kuongeza ushahidi haisemi kesi ilifia hapo kutokana na uamuzi huo.
Mahakama imekata notice of additional substance of evidence, kwahiyo wanalalamikia uamuzi wa notice kukataliwa.
Jambo la pili ni Je mleta maombi anayo mamlaka ya kuiambia Mahakama itumie mamlaka yake ya kupitia kumbukumbu ili kuridhisha matakwa yake mwenyewe?
Jibu ni hapana hiyo siyo haki yao kisheria kwani wajibu wa kuangalia record ni wa mamlaka yenyewe.
Part 226 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
‼️DEREVA WA HECHE AUWAWA KWA SUMU‼️
Kwa msiomfahamu Suez Dani Maradufu ambae ni Dereva wa Mhe. Heche kabla hajawa Dereva wa Heche alikuwa dereva wa Baba ake Mhe. Heche.
Amefanyakazi kwenye familia ya Mhe. Heche kwa miaka mingi baada ya Baba ake Heche kufariki, mwaka 2015 Mhe. Heche alipochaguliwa kuwa Mbunge ndipo alimchukua Suez Maradufu ili awe Dereva wake.
Sasa turudi kwenye issue ya mauaji/kifo
Siku ya tukio Mzee Suez Dani Maradufu aliamka asubuhi kama kawaida akatimiza wajibu wake, na alikuwa ni mzima wa afya.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa anasema kwamba siku ya tukio, kabla Mzee Suez hajarudi kulala mahali alipokuwa amefikia, kuna Vijana wa Abdul na Sumai wakiongozwa na mtu ambae anaitwa Mark
Walienda mahali alipokuwa amefikia Mzee Suezi, walijitambulisha kwa mmoja wa wahudumu kwamba wao ni maofisa wa Usalama, wanataka kuonyeshwa chumba ambacho analala Mzee Suez Dani Maradufu ili wafanye ukaguzi maana kuna taarifa wamepewa kwamba ndani ya iko chumba kuna vilipuzi ambavyo CHADEMA wamepanga kuvitumia kwenye Maandamano ya 7/7 na kwamba wanavigawa kila Mkoa.
Muhudumu alikubali, akaongozana nao mpaka kwenye hicho chumba kisha akawafungukia mlango, walipoingia ndani ya chumba hawakufanya upekuzi kama walivodai badala yake walipulizia vitu ndani ya chumba cha Mzee Suez kisha wakaondoka zao lakin kabla hawajaondoka walimwambia Muhudumu asiseme chochote maana akisema wao watajua tu.
So baada ya muda kidogo kupita, Mzee Suez alifika bila kujua chochote akaingia chumbani kwake kulala, ilivofika asubuhi baada ya wenzake kumkosa kwenye simu, walimfuata mahali alipofikia na kumgongea mlango muda mrefu bila mafanikio, ndipo ikabidi watoe taarifa Polisi ambapo walifika eneo la tukio, wakavunja mlango na kukuta mwili wa Mzee Suez upo chini damu zikiwa zimetapakaa sakafuni.
Alikuwa na damu mdomoni, puani na masikioni, Polisi walichukua mwili na kuupeleka Hospital ya Mkoa kwa ajili ya Uchunguzi.
Sasa kwa mujibu wa mmoja wa Vijana wa Abdul anasema kwamba hao wauaji waliompa sumu Mzee Suez ndo wale ambao gari yao ilipigwa picha Makambako wakati inafuatilia msafara wa Mhe. Heche so walifuatilia msafara tangu akiwa Lindi mpaka anafika Kigoma ila walikuwa wanabadili Plate number za gari ili wasishtukiwe.
Wauaji hao baada ya kufanikisha mauaji ya Dereva wa Heche, juzi mchana walirudi pale Lodge alipokuwa amefikia Mzee Suez wakachukua baadhi ya Wahudumu na kuondoka nao akiwemo yule ambae aliwafungulia chumba cha Mzee Suez ili kuzuia taarifa isivuje.
Mtoa taarifa anasema kwamba majibu ya Postmortem tayari wanayo tangu jana mchana wakati huo hata Uchunguzi bado haujafanyika, wamepanga kusema kwamba Mzee Suez alikuwa na mwanamke, alikunywa dawa za kuongeza nguvu za kiume, dawa zikamzidia na kusababisha umauti.
Ndo maana Polisi kwenye taarifa yao wanasema kwamba walimkuta na dawa, wakati dawa walizomkuta nazo ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa na tumbo, wanataja sana izo dawa kwasababu wanajua mwisho wa siku Report yao ya mchongo itasema ivo ivo.
So hata ile kauli ya IGP Mstaafu Simon Siro ambae ndo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwamba kifo cha Suez ni cha kawaida haikuwa bahati mbaya ndo maana hata hao MaPathologist walivofika tu Kigoma, wakaenda ofsini kwa Sirro kupewa maelekezo ya nini ambacho wanatakiwa kufanya.
#JusticeForSuezMaradufu
There are no more 8pm matches until July 7. Here’s what’s happening tonight at the #FIFAWorldCup:
Matches:
10pm: Bosnia 🇧🇦 v Qatar 🇶🇦
10pm: Switzerland 🇨🇭 v Canada 🇨🇦
1am: Morocco 🇲🇦 v Haiti 🇭🇹
1am: Scotland 🏴 v Brazil 🇧🇷
4am: Czechia 🇨🇿 v Mexico 🇲🇽
4am: South Africa 🇿🇦 v South Korea 🇰🇷
Press conferences:
10pm- Australia 🇦🇺
10:30pm- Japan 🇯🇵, Tunisia 🇹🇳
11:30pm- Sweden 🇸🇪, Netherlands 🇳🇱
00:30- Türkiye 🇹🇷, Paraguay 🇵🇾
00:45- Curaçao 🇨🇼
1:45am- Ecuador 🇪🇨, USA 🇺🇸, Côte d’Ivoire 🇨🇮
2:4am- Germany 🇩🇪
(All times EAT)
Leo, tarehe 23 Juni 2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. @HecheJohn, akiwa katika Operesheni Katiba Mpya, Free Tundu Lissu amezindua Ofisi ya Kata ya Nsalaga katika Jimbo la Mbeya Mjini. Katika uzinduzi huo, amekabidhi Shilingi 200,000 kwa ajili ya ununuzi wa mifuko 10 ya saruji, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono ujenzi na uimarishaji wa ofisi hiyo.
Macho yako yanaona kama MIMI?😳
Huyu mtu alieuwa watu kwa MAELFU kwenye maandamano ya MO29 jana kaonekana akimfuatilia Makamu mwenyekiti HECHE na msafara wake.
Mtandao hausahau—naiacha hapa kama sehemu ya kumbukumbu zetu.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Hii Gari inatufutilia msafara wa Makam Mwenyekiti Mhe. @HecheJohn kila wanakoenda kuna watu zaidi ya 6 wapo ndani na inapaki nyuma ya Mkutano hata sasa hivi ipo Kwenye Mkutano wa Makambako
Homa ya MAANDAMANO ya 7/7 inazidi kupanda.
Watanzania wanataka kumaliza MISIBA ya wapendwa wao—wanataka wapewe miili ya ndugu zao waliouliwa kikatili #MO29
Hii nchi haitakuja kutulia mpaka watanzania wazike wapendwa wao. #77Tunatoka
REPOST 200
Leo tupo hapa Ruaha – Mikumi, wilaya ya Kilosa, mkoa wa Morogoro. Wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema na Boniface Jacob watazungumza na wananchi wa RUAHA. Muda huu ni wakati tunaingia uwanjani, umeona huo mtitiiii? Watu ni wengi kama mchanga. #peoplespower
Baada ya kuvuja screenshot kutoka kwenye group la Maafisa Habari wa Serikali haram ambayo Msigwa alikuwa anawalaumu Maafisa hao kwamba kwanini Serikali haram inashambuliwa na wao wapo kimya hawaitetei.
Kwenye ile screenshot kulikuwa na namba ya Gerson Msigwa, watu walichukua ile namba wakamsalmia baada ya kumsalmia Gerson aliagiza Jeshi la Polisi liwashughulikie hao Vijana waliomsalmia.
Kuna Vijana zaidi 150 kutoka mikoa mbalimbali walitekwa na Jeshi la Polisi mpaka sasa haijulikani walipelekwa wapi.
Kama mnavomskia anavotamba hapa, ipo siku mtatuambia mlipeleka wapi ndugu zetu.
Ufaransa ni miongoni mwa timu hatari duniani, tena wanatajwa kwenye orodha ya timu zinazoweza kuwa mabingwa wa dunia mwaka huu. Kipindi cha kwanza hawajacheza vizuri, kipindi cha pili wamebadilika na wameshinda. Hii ndiyo maana ya kuwa na wachezaji bora wenye hadhi ya dunia.