VIDEO:
Mtaalamu wa masuala ya ulinzi na usalama aliyewahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na baadaye Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Prosper Makonya, ametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza kuwa amechukua hatua hiyo kwa sababu CCM ni chama cha Watanzania wote.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Taifa, Kenani Kihongosi, uliofanyika Stendi ya Mbondole wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Makonya amesema atawajibika kukilinda Chama Cha Mapinduzi, mali zake na viongozi wake.
"Na kama kuna mtu anasema hatuwezi, tukutane naye field ndio atajua tunaweza au hatuwezi. Field ndio inayokutambulisha kazi yako.", ameeleza Makonya ambaye pia aliwahi kuwa msaidizi wa aliyekuwa mjumbe wa sekretarieti kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Marehemu Ali Mohamed Kibao akifahamika zaidi kama K2.