Mtu akisema CCM haijafanya chochote kwa miaka zaidi ya 60 ya uongozi, aidha hafahamu historia ya nchi hii au amekuta mengi yakiwa tayari yamejengwa.Mtu akisema hivyo huwa namuona kama mtoto au mwendawazimu. Ni kweli zipo changamoto, lakini kusema hakuna kilichofanyika si sahihi. Je, wakati wa uhuru tulikuwa na shule karibu kila kata, hospitali za rufaa kila mkoa, au miundombinu mikubwa ya barabara na reli? Kukosoa ni haki, lakini pia ni muhimu kuthamini hatua zilizopigwa na maendeleo yaliyopatikana. Au nyie mmepata uhuru na SGR.?
Kama hutembei na kufuatilia mambo, unaweza kudhani sijui nipo wapi ๐. Kumbe niko SONGWE kitovu cha biashara za nchi za SADC na lango muhimu la biashara kati ya Tanzania na nchi jirani.
Hapa ndipo ilipo Songwe International Airport, moja ya miundombinu mikubwa ambayo inaweza kuibadilisha kwa kasi kubwa Nyanda za Juu Kusini kiuchumi. Hata hivyo, bado tunashuhudia wasafiri kutoka Zambia, DRC Congo, Zimbabwe na maeneo mengi ya kusini mwa Tanzania wakilazimika kusafiri hadi Dar es Salaam ili kupata ndege za kimataifa.
Je, si wakati sasa wa kuanza kuvutia mashirika ya ndege ya kimataifa kutua moja kwa moja Songwe?๐ค
Hatua hiyo itarahisisha usafiri, kupunguza gharama kwa wasafiri na wafanyabiashara, kuongeza biashara ya mipakani, kukuza utalii, kuvutia uwekezaji na kufungua fursa nyingi za ajira kwa vijana wetu. Songwe na Tunduma tayari ni kitovu kikubwa cha biashara katika ukanda wa SADC,kinachohitajika sasa ni kuunganisha nguvu hiyo ya biashara na usafiri wa anga wa kimataifa.
Maendeleo ya Tanzania hayapaswi kujikita Dar es Salaam pekee. Kila mkoa wenye uwezo wa kiuchumi unapaswa kupewa nafasi ya kuwa injini ya ukuaji wa Taifa. Safari za kimataifa kutoka Songwe International Airport zitakuwa hatua muhimu katika kuifanya Nyanda za Juu Kusini kuwa lango la biashara, uwekezaji na maendeleo kwa Tanzania na Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.
SONGWE IPO TAYARI. Kilichobaki ni maamuzi ya kimkakati ya kuifungua zaidi kwa dunia.
Leo alfajiri, nilipokuwa natafakari mafanikio ya tukio la SENET Mkoa wa Mbeya na kujaribu kuona maeneo ya kuboresha kwa ajili ya matukio yajayo, ghafla nikajikuta mawazo yangu yakielekea kwenye jambo lingine muhimu zaidi hasa vijana na siasa katika zama hizi.
Nikajiuliza maswali kadhaa:
Je, vijana wa kisasa bado wanajiunga na vyama vya siasa kwa sababu ya sera, itikadi na misingi ya chama kama ilivyokuwa zamani?
Ni nini hasa kinawasukuma vijana kujiunga na vyama vya siasa leo?
Ni njia ipi yenye ushawishi mkubwa kwa vijana kujiunga na chama cha siasa ni ahadi,maneno, vitendo, au ushawishi wa viongozi?
Je, wewe binafsi ni nini kilikufanya uwe mwanachama au mfuasi wa chama unachokiunga mkono?
Ni jambo gani linakuvutia zaidi katika chama hicho?
Nina hamu ya kujifunza na kuelewa kwa undani fikra za vijana wa kizazi hiki kuhusu siasa. Karibu tushirikiane mawazo.
Leo tulipata heshima ya kumpokea Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa, Cde Debora Tluway aliyemwakilisha Katibu mkuu wa UVCCM Taifa cde Halid Mwinyi , katika Kongamano la Vijana wa Mkoa wa Mbeya lililolenga kujadili maisha ya chuo na baada ya chuo.
Kupitia mada yake, vijana tulijifunza kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi, ujasiriamali, uongozi na ushiriki katika siasa kama nyenzo ya kuleta maendeleo binafsi na ya taifa. Ulikuwa wakati mzuri wa kupata maarifa, uzoefu na hamasa kutoka kwa kiongozi wetu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa UVCCM wa kuendelea kuwajengea uwezo vijana wa Kitanzania.
UVCCM ya KiGen Z, UVCCM ya vitendo. ๐ช๐ฟ๐ช๐ฟ
#TBT na Thom Leo ๐
Hii ndiyo ilikuwa gari yangu ya kwanza, Rav4 kipisi. Nikiwa UDSM nilijulikana kama DALALIMSOMI. Nilikuwa na certificate ya BRELA, sina ofisi bado, lakini nilikuwa napima ardhi, udalali wa viwanja na kutoa elimu kuhusu masuala ya ardhi. Safari ilianzia hostel.
Haka kadude m3 aseeh hii kazi ya production nayo inahitaji kujipanga sana
Wakuu nianze kuleta barua maofficine huko nipate pa kuanzia ๐๐au hamtaki wapiga picha