@godbless_lema Nadhani huna akili yote yanayofanywa na serikali huoni la maana haha au unaogopa ukiongea ukweli utaambiwa umeunga mkono juhudi za samia !?
Leo nilipata fursa ya kumwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. @KassimMajaliwa_ , katika hafla ya kupokea na kukabidhi vifaa kwa ajili ya makundi mbalimbali, vilivyotolewa na wadau kupitia uongozi wa Wilaya ya Kigamboni kwa ajili ya makundi ya wanawake, wazee, vijana pamoja na watu wenye mahitaji maalum.
Wakati hafla hiyo ikiendelea nilipokea simu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia , akawasalimia na kuzungumza na Wakazi wa Kigamboni, ambapo Mhe. Rais ameipongeza Serikali ya Wilaya ya Kigamboni chini ya Mkuu wa Wilaya, Bi. @halimabulembo , kwa kutoa majiko ya gesi kwa Mama na Baba Lishe zaidi ya 500 ili wayatumie kupikia kwa kutumia nishati safi, kugawa kadi za Bima kwa baadhi ya Wazee wa Kigamboni, Makoti ya Kujilinda kwa Madereva Bodaboda (Reflectors), kujenga vibanda vya kujikinga mvua na jua kwa waendesha bodaboda pamoja na Vifaa Tiba vya Kujifungulia kwa akina Mama Wajawazito.
Kipekee nampongeza sana Mhe DC Bulembo kwa ubunifu, uchapakazi na moyo wa kusaidia wenye uhitaji hakika huu ndio uongozi sahihi, hongereni watumishi wote wa Manispaa ya Kigamboni kwa kazi hii nzuri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Changamoto za Millenia (MCC) Bi. Alice Albright kwa njia ya video, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Desemba, 2023.
MCC imeichagua tena Tanzania kuingia katika mpango wa kupata msaada wa Fedha zitakazolenga kusaidia mabadiliko ya Sera na Kitaasisi nchini ili iweze kufanikiwa kupata mpango wa Compact.
Mara ya mwisho MCC iliwahi kutoa msaada wa Fedha wa Dola za Kimarekani milioni 698 mwaka 2008 ambazo zilitumika hadi 2013.
@ikulumawasliano@MCC_CEO@mwigulunchemba1
Nilipata fursa ya kufungua Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha.
Nimewaasa watangulize mbele uzalendo kwa kuwapa tenda wakandarasi wazawa kisha wazawa ndio waajiri wageni.
Hii ndio fursa pekee ya kukuza uchumi wa Kampuni zetu za ndani na kutengeneza matajiri wengi ambao watalipa kodi kwajili ya Maendeleo ya nchi yetu na hii ndio kiu ya Mheshimiwa Rais kuona Watanzania wanamiliki uchumi.
πππππ πππππ ππππππ , ππππ πππππππππππ ππππππππ
1. Katika Bajeti 44 trilion zinapigwaje 30 trillion? Afu na mishahara ya Trilioni 20 ikaendelea kulipwa? Huku mtaani miradi ya matrilioni ikaendelea kutekelezwa? Hata hili umeshindwa kuling'amua?
2. FIU kwa sehemu kubwa inachambua miamala ya sekta binafsi, hicho unachoona kwenye hiyo ripoti yao ni namna wafanyabiashara wamepata ahueni wanafanya manunuzi makubwa nje ya nchi kwa pesa nyingi wanakuja kuuza kwa faida kubwa, hiyo ndio faida ya Uchumi wa watu na sio vitu, awamu yenu mlifunga nchi biashara zikafa ndio maana hili linakuwa surprise kwako. Uchumi halisi unapokuwa lazima miamala mingi ifanyike nje na ndani ya nchi kwasababu biashara haina vikwazo wala kufungiwa. Mama karejesha imani ya wafanyabiashara nchini, wawekezaji wengi wamepata uhakika wa mitaji yao wameamua kuleta mapesa mengi kwa njia ya miamala maana dunia sasa ni cashless economy.
3. Hakuna mkopo uliovunja sheria, hakuna mkopo ambao haukupitishwa kwenye bajeti. Bajeti ambayo wewe uliiunga mkono kwa kinywa chako binafsi ukatamka 'Ndiooo". Kwa taarifa yako tu awamu hii kila kitu kimewekwa wazi wananchi wanaona kila jambo na wanapata muda wa kukosoa, wanajibiwa kwa hoja bila kutekana na kuuana. Awamu yenu Mmeliingiza Taifa hili kwenye mikopo umiza (Nyonyadamu) miliyokuwa mnachukua kimya kimya huku mkidanganya watu kuwa mnajenga kwa pesa za makusanyo ya ndani kumbe ni uongo mkubwa, tena mlikopa kwa masharti mabovu ya kihuni mkitoa tenda kwa single source kwa makampuni yaliyowapa rushwa na ushahidi upo hadharani CAG kausema, mlikopa kwenye mabenki ya kibiashara yenye riba za kutisha, leo hii unapata wapi uhalali wa kushuku mambo ambayo yako wazi kila mahali. Mama anatafuta hela kwenye taasisi zenye riba ya chini ya 1%, kila mkopo unawekwa hadharani, unakoelekea panajulika na kazi inaonekana. Hakuna tena blah blah.
4. SGR inaendelea hakuna kilichosimama. Natambua wewe na wenzio hao mnaokesha kupika majungu mlitarajia mradi huu ukwame ili sukuma gang mjigambe kwamba ninyi ndio mabingwa na miamba ya nchi hii, hilo mmekwama endeleeni kumeza panadol maana Mama hana shuguli ndogo kila kona anapeleka maendeleo. Mama alikuta lot 2 tena zikiwa asilimi za chini sana, kwa muda mfupi kapiga Asilimia zaidi ya 90 na kaanzisha nyingine 5. Hapa ndio panawafanya mchanganyikiwe kabisa.
5. Kuhusu uhujumu uchumi, as we speak ulitakiwa uwe gereza la butimba ukitumikia kifungo cha maisha kwa uharamia na ukatili mkubwa uliowafanyia wavuvi wa nchi hii, umewatia umaskini wa kutisha, ulichoma nyavu zao, ukawafunga, wengine wakatoroka nchi, uliwafanyia hivi kwasababu hawakukupa rushwa, hili liko wazi na ushahidi upo.
6. Nawapa taarifa tu na hao wenzio, nchi imerejea kwenye mstari sahihi, wananchi wanafuraha, hawatekwi, hawatishwi, hawabambikiwi kesi, wapinzani wamepewa kila wanachotaka lakini hawana ajenda, Uchumi wa watu umeimarika, Fedha zinaonekana mtaani, hakuna kilichosimama na miradi mipya ya kutosha.
Mwisho, number hazidanganyi, ni muda mwafaka urejee darasani, weke tunguri zako likizo weka ulozi wako pembeni ingia kimbwetani, ukitoka huko ndio uje tuzungumzie haya mambo lakini kwasasa huna unachofahamu, yamekuzidi kimo.