Nina swali, wale wapuuzi waliokuwa wanapush maridhiano kati ya Watanzania na wauwaji wa CCM wana la kusema kwa sasa????
Wanaharakati tulipokuwa tunayakataa maridhiano tulijua wauwaji hawako tayari kwa maridhiano ya kweli, wanachotaka kwenye maridhiano ni legitimacy na uwezo wa kuwazodoa international community kwa kuwaambia, msituingilie sisi tumeshafanya Maridhiano na tume heal.
Uzuri walijua wanapanga mambo gizani kumbeeee!
Na siku zimesha tutajua hadi majina yao yote na picha zao! Vijana msikubali kutumika!
7/7 kaa nyumbani kama vipi we mdhalimu!
#TutaelewanaTu
Miili ya wenzetu ilichomwa moto tarehr 29 October, hatuwezi kurudisha uhai wao lakini tunaweza kushinikiza haki zao zipatikane kwa gharama ya jasho na damu zetu.
7/7 twendeni tukachore mstari.
ENOUGH IS ENOUGH.
#FreeLissu#FreeTanganyika
‼️Mipango miovu ya CCM na polisi‼️
Nimepokea taarifa hapa na pale ila chanzo hiki ndo imeeleza kwa kiina kile kinachosemwa kipo ktk mipango ya mafedhuli dhidi ya CHADEMA
Vijana kupewa silaha na kujifanya wametumwa na Chadema! Ujinga na upumabvu ila ndo wamekomea hapo kiintelijensia!
Kwa mujibu wa mtoa taarifa Walikuwa Morena hotel wakipanga na jana wakati wa giza nene ndo walikuwa wanasambaza vitu
Picha za ushahidi nimehifadhi kwa sasa
Haya ndo mambo yao - ushenzi mtupu!
Plot to implicate opposition CHADEMA in a false flag event! The police and CCM are planning to give weapons to 20 young men in every region then claim that they were armed by Chadema - to prove their stupid lies that #TanzaniaMassacre in October 2025 was done by opposition
#SamiaMustGo #CCMmustgo
Siku nzima ya leo magari mawili ya polisi na polisi wakiwa wameziba nyuso zao na silaha kubwa kubwa, wamenifuatilia tangu nikiwa Urambo kwa kupokezana mpaka nafika Kigoma.. njiani nimesimama mara mbili kuwauliza shida yao ni nini kwangu hawakuwa na majibu ya maana.
Nimefika hapa Kigoma kila ninakopita na hapa Hotelin kwangu wamejaa maafisa wakiwa na nguo za Kiraia..
Mimi ni Mwanasiasa wa upinzani ninaetimiza wajibu wangu wa kikatiba… Chama chetu ni chama cha siasa ambacho kimesajiliwa na chenye haki zote katika Nchi hii.
Nimepokea taarifa nyingi kwa watu wema wakitaka niwe makini, wengine wanasema mimi na familia yangu tumetolewa maelekezo mabaya.
Nitatimiza wajibu wangu bila uoga wala hofu, hakuna mtu anaweza kuniondoa kwenye haki na wajibu wa kutetea Nchi yangu na watu wetu.
Ninawashauri watawala dhalimu kuacha kucheza na utulivu huu uliopo . Hofu haijawahi kuzaa amani, hofu huzaa hofu zaidi.
Hakuna siku nitakimbia Nchi yangu.
ANAANDIKA ASKOFU BAGONZA PhD
JAMANI MSIMUONEE KATAMBI; SIYO MJALUO❗️❗️❗️
Ni Wajaluo tu ambao huwa wanasimamisha saa ili kuokoa muda wasichelewe wanakoenda. Katambi si mmoja wao. Yeye ni Msukuma gete gete🤣🤣
Tatizo siyo Katambi. Tuna mgongano sugu kati ya Majasusi Wanasiasa NA Wanasiasa Majasusi. Hawa ni watu wawili tofauti. Nitaeleza siku nyingine. Mnaoogopa kuchanganya Dini na Siasa, ogopeni pia kuchangana Ujasusi na Siasa.
Kuna mambo 9 yanayozua maswali:
1. Paschal Chinyele (Jasusi Mwanasiasa), kamrushia mpira Spika (Mwongozo). Spika akatuliza kifuani. Akampasia mpira Katambi (Mwanasiasa Jasusi). Katambi akajifunga goli kwa kuinuka na tamko la serikali. Imekaa saa ngapi? Kama ilikaa kwa nini wampange Paschal na Spika? Wameuza mechi.
2. Zuio la mikutano likatolewa bungeni. Tuseme ni bunge limezuia mikutano?
3. Limetamkwa na Waziri; Tuseme ni Waziri kazuia? Aliishapiga chanjo ya kumkinga na kirusi cha kuvunja katiba?
4. Waziri katamka neno eti kwa niaba ya Amiri Jeshi, Je ni Rais kazuia kupitia Waziri, tena kupitia mhimili mwingine? Msimchonganishe rais wetu👊👊
5. IGP kaagizwa kukiuka katiba. Atatii? Akitii, nani mkosaji? Aliyeagiza au aliyetii?
6. Kwa nini Waziri hakusubiri Waziri Mkuu ndiye atoe zuio hilo kwa niaba ya serikali wakati anaahirisha bunge?
7. Kwa nini serikali isitumie TCD au Msajili wa Vyama, wakaitwa wadau na kushawishiwa wakubaliane kuvunja katiba?
8. Je ili zuio/katazo la mikutano au zuio/katazo la kutumia katiba; yaani kwamba imeenda likizo kwa muda?! Hatua hii hufanyika nchi ikiwa vitani au wale jamaa zangu majirani wa Wajaluo wanapoamua kuchanganya cha Arusha na siasa🤣🤣. Sasa tunaomba katiba mpya ya nini ikiwa iliyopo haina kazi mpaka inaenda likizo??!!
9. KWA UPOLE: Hivi mikutano ya kisiasa ni haki ya kikatiba au ni fadhila za serikali kwa wananchi. Pleaseee nimeuliza kwa upole tu.
USHAURI: Kwa kuwa umeanza kama mchezo wa kuigiza, tujifanye igizo limeisha, tuendelee na mishe mishe zetu za weekend.
HALAFU: Msiende kubugudhi wageni kwenye hoteli usiku wakati wa doria. Mtaona yasiyowahusu. Ishia mapokezi kwa kunyata. Kama kuna Mjaluo anataka kuandamana, sibiri kupambazuke, mdake Tanganyika jeki hata kama Tanganyika haipo, mpeleke kwa Polisi siyo Safe House.
MAKATAZO HAYA: Yaishie hapo kwenye siasa. Msiguse mikutano ya dini, harusi, jando wala Yanga atakapomfunga Simba.
Gudubai, Wajaluo kuweni macho, kuna jamaa ana kisu kikali na anatahiri bila ganzi🙈🏃🏃🏃
Marekani wamesema juzi ( 24 June 2026) kwamba mradi umezinduliwa, na wala hawakuwa na mambo mengi
wakashukuru rais wa Marekani kwa kuwezesha kifedha huu mradi
Samia na Malasusa wamekimbilia KCMC kujenge Jiwe la Msingi na kujipigisha picha na kuweka majina yao hapo kuonyesha kuna shughuli wamefanya.
Huyo mwenye kura 98% sasa amekuwa wa kuvizia miradi na kujenge majiwe ya msingi ya uzinduzi
Ukiangalia Malasusa amesimama kama mateka wa Bi Msumi, kwa sababu anajua ukweli hili tukio lina uongo, Bi Msumi hawa maaskofu wa KKKT umewapakazi ngumu sana na utawakosanisha tu na waumini wao sio muda mrefu, Uongo na utapeli umekuwa mwingi sana