Mwaka 2025 nikipokea gawio na michango kutoka taasisi na mashirika ya umma nilitoa maelekezo ya uboreshaji zaidi. Nina furaha kuona maelekezo hayo yamefanyiwa kazi, na gawio la serikali mwaka 2026 limeongezeka kwa asilimia 30, kufikia shilingi trilioni 1.32. Siku ya Gawio si siku ya kusherehekea mafanikio ya kifedha pekee, bali ni fursa ya kutathmini maeneo yanayohitaji uboreshaji zaidi ili mafanikio tuliyoyapata yaendelee.
Mafanikio hayo ni uthibitisho kuwa, taasisi na mashirika ya umma yanaweza kutoa huduma na kuwa sehemu ya ujenzi wa uchumi wa taifa letu. Tunapoelekea kuanza utekelezaji Dira ya Taifa 2050, ni muhimu tufahamu kuwa hatutaweza kujenga uchumi shindani kwa taasisi zinazofanya kazi kwa mazoea, ni lazima tujipime kwa matokeo, na si takwimu. Haya ndiyo maono na mwelekeo wa taifa letu.
Pamoja na hayo, ninazipongeza taasisi na mashirika yote yaliyotoa gawio kwani hii ni sehemu ya lengo letu la kuongeza mapato ya ndani katika kugharamia shughuli za maendeleo. Hata hivyo, pongezi hizi zisiwe sababu ya kuridhika na kubweteka, kwani hatutasita kuchukua hatua tunapobaini uzembe na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
Gawio la Serikali laongezeka kwa asilimia 108 chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan:
🔵 Mwaka 2021: TZS bilioni 637
🔵 Mwaka 2026: TZS trilioni 1.32
Ufanisi huo ni matokeo ya hatua anazoendelea kuchukua kuimarisha taasisi na mashirika ya umma.
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel:
Ikulu Tanzania na Tovuti: https://t.co/wmldPXYfck
#TanzaniaYetuSote#NchiYetuKwanza
#MaendeleoEndelevu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Juni 29, 2026 ameongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Jijini Dar es salaam.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mfizikia Tiba Bi. Rehema Ramadhan kuhusu utendaji kazi wa mashine ya kutibu saratani (Linear Accelerator) baada ya kuzindua Jengo la Tiba Mionzi (Radiotherapy Unit) katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 24 Juni, 2026.
Ninalishukuru Baraza la Taaluma la Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) kwa kunitunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa). Nimepokea heshima hii kwa unyenyekevu mkubwa kwa niaba ya Watanzania wote ambao ndiyo msingi wa mafanikio tunayojivunia na yanayoitangaza nchi yetu.
Chuo hiki ni sehemu muhimu ya maendeleo tuliyonayo kwani maarifa, ujuzi, nidhamu na weledi ambao zaidi ya Watanzania 1,100 wamepata kwa kusoma hapa, vimechangia ustawi wa wananchi, kuijenga nchi yetu na kuimarisha uhusiano wetu. Mchango huu bado unahitajika, sawa na ilivyokuwa wakati kinaanzishwa.
Ahsanteni sana.
Nikihitimisha ziara yangu ya Kitaifa katika Shirikisho la Urusi, leo pamoja na mambo mengine nimepata fursa ya kuhutubia Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Urusi pamoja na Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF), ambayo yamekutanisha viongozi, wataalamu wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.
Nimewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu salama na bora kwa mitaji yao, tukijivunia mazingira wezeshi ya kisheria, amani na utulivu, miundombinu bora, ukuaji imara wa uchumi, uwepo wa nguvu kazi na fursa ya kufikia soko la zaidi ya watu milioni 500 ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Pia, nimebainisha sekta za kimkakati ambazo ni kipaumbele katika uwekezaji zikijumuisha madini, kilimo, nishati safi, mafuta na gesi, afya pamoja na usafiri na usafirishaji.
Habari njema zaidi ni kuwa, kuanzia Julai 2026, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) itaanza safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Moscow. Hatua hii muhimu itaimarisha zaidi utalii, biashara na uwekezaji, na kufungua ukurasa mpya katika historia ya uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
Mwaka huu Tanzania na Singapore tunaadhimisha miaka 45 ya uhusiano wetu ambapo kwa upekee leo tumempokea Rais wa Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam, Ikulu jijini Dar es Salaam. Hii ni historia na heshima kwa nchi yetu kwani ni mara ya kwanza Rais wa nchi hiyo kutembelea Tanzania, hatua inayodhihirisha dhamira yetu ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya nchi zetu na watu wake.
Baada ya mazungumzo yetu, tumeshuhudia utiaji saini mkataba na hati nne za makubaliano zinazolenga kufungua fursa mpya katika biashara, uwekezaji, kuwezesha vijana kupitia elimu ya ujasiriamali, ujuzi na ubunifu hasa katika uchumi wa kidijitali. Aidha, tumekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo sambamba na kuanzisha mfumo wa pamoja wa mashauriano utakaosaidia kuratibu utekelezaji wa makubaliano yetu na kushughulikia changamoto kwa ufanisi na kwa wakati.
Katika hatua nyingine, nimeikaribisha Singapore kufungua ubalozi wake nchini ili kurahisisha utekelezaji wa makubaliano haya na kuimarisha zaidi uhusiano wetu.