Katika hizi Ofisi ambazo mmepata kazi na zinasaidia kuendesha maisha basi ni muhimu kuchunga usiwe kikwazo kwa mwenzio ambaye naye anajitafuta.
Wangekuzibia milango waliokutangulia usingefika hapo. Kunjua nafsi riziki za watu Mungu hazishushi moja kwa moja zinapitia kwenye mikono ya watu. Kuwa kiunganishi kizuri usiwe kikwazo.