Kwa vile ndoto moja imekwama haaanishi ndo mwisho wa kua na ndoto, inabidi uwe mwepesi kupata ndoto nyingine. Na ndoto si lazima iwe ile ya utotoni, bali ni malengo katika maisha.
Kama inakubidi uwapoteze baadhi ya watu kwenye maisha yako, ili malengo yako yatimie..
Jitahidi ufanye hivyo, kwasababu ata wao wenyewe wangefanya hivyo kwako..
Kuna umri ukifika stress zako zinatakiwa ziwe kuhusu kutimiza ndoto zako, majukumu ya familia yako, kazi na pesa na sio kwa ajili ya nani anakupenda na nani hakupendi au nani anaongea na nani haongei na wewe. Angalia na zingatia maendeleo na ukuaji wa maisha yako. GoodMorning ❤️