Sayansi ya Mungu utaikufuru kisa njaa maana huwezi chagua aina ya mzazi atakae kuzaa, Jirani kazaliwa na waziri wewe mama ako kichaa baba mlevi alaf konda wa dala dala ya kibaha, Usikate tamaa wewe ndo wa kuibadili sura ya familia kuanzia sasa na unaweza.
Binafsi Tuzo za muziki za mwaka huu nilitarajia hizi lawama zinazoendelea na zaidi kwa aina ya hits zilizotengenezwa ni kama vijana walikuwa wanawaandalia lawama BASATA
Mfano: Enjoy, Shu na Single again ipi unaipa wimbo bora?
Huyu dada alikua mpishi wa washiriki wa BSS kwa miaka kadhaa mwaka huu akaomba na yeye ashiriki, Sahizi yuko fainali na anachokifanya kwenye perfomance zake ni mauaji matupu🔥
Nimeisikiliza hii ngoma mara nyingi niwezavyo ila akili yangu imegoma kukubali kuwa Marioo kaandika hii verse ya kwanza, Kila nikisikiliza namuona Harmonize akiandika🥲
Narudui Tena kuuliza hivi mnauhakika huyu Mmakonde hatumii Uchawi kuandika Mistari yake?🤔..... Basi kama ni Mjani serikali iruhusu tu nchi nzima tunyonge😀...Sema jamaa anamwonea sana Marioo, japo wote Mafundi lakini kwa Mara ya Pili Mmakonde anamkalisha TotoBad What a Verse🔥..