"Usipoteze muda kukosoa, kubeza kuiga na kuhujumu kazi ya mwenzako. Tafuta namna ya kufidia pengo lililo katika kazi yake na kujiunganishia fursa itokanayo na mnyororo wake wa kazi yake. Kazi ni kujengana si kubomoana. Usipanue ushindani, panua fursa." ~Togolani Mavura.
"Leo yako na unayoyapitia, yawe mazuri au mabaya, yaweza kuwa ndio jana ya wenzako au kesho ya wenzako. Usilazimishe leo yako iwe ndio leo ya kila mtu. Kila mtu na leo yake!" ~Togolani Mavura.
"Usiamini haraka na kwa urahisi kila unaloambiwa kuhusu tabia, maneno na matendo ya watu wengine. Usimhukumu mtu bila kuwa na uhakika wa “dhambi” zake. Bahati mbaya kwenye jamii yetu tuna watu wengi ambao hupenda kusingizia uongo na kupaka matope wenzao na watu hawa hawataisha."
"Ukifanikiwa kumfanya walau mtu mmoja kwa siku akamshuhudia, kumtaja au kumshukuru Mungu kwa sababu yako, basi umetoa sadaka kubwa sana." ~Togolani Mavura.
"Tunapishana na fursa kila siku tunapowachukulia poa watu tunaokutana nao kwa mara ya kwanza,kwa kuwadhania hawana manufaa kwetu.Katika maisha utakutana na sehemu ndogo tu ya watu waliopo duniani.Kila unayekutanishwa naye katika maisha iko sababu na liko kusudi."~Togolani Mavura.
"Ogopa sana nguvu ya wakati na nguvu ya swali. Mabadiliko na uelekeo wa maisha yetu hutokea tunapojiuliza swali sahihi katika wakati sahihi." ~Togolani Mavura.
"Mara nyingi chuki dhidi yetu hupaliliwa na tambo na majivuno yetu hadharani kisha tunalaumu watu na kuwaita wabaya. Tuwe wanyenyekevu." ~Togolani Mavura.
"Kwa udhaifu wetu, tunatenda dhambi kila siku iwe kwa kuwaza, kwa kunena, kwa kutenda au kwa kutotimiza wajibu. Ili kufidia, tujitahidi kutimiza japo ibada moja na kutenda wema japo mmoja kwa siku kila siku kusawazisha dhambi zetu." ~Togolani Mavura.