#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 21
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana jela)
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuwa maafisa Magereza. Wanapaswa kukagua barua inayotoka ndani au kuingia ndio inapaswa kusomwa.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Soma kifungu cha 46 Cha Sheria na kanuni ya 10 na 11 ya kanuni za Magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Anahangaika haoni.
Mhe. Lissu: Sasa wambie majaji kama kanuni ya 10 na 11 inahusu barua wanazoandika na wanazoandikiwa wafungwa.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na wanaosoma ni wewe au maafisa wako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe, Lissu: Ukiikataa barua unamrudishia na kumwambia sababu. Na kama ikikataliwa kwa aliyemletea pia unamrudishia na kumpa sababu. Na kama barua ni ndefu sana na huyapendi ni sahihi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama nje ya barua kwa wafungwa au kutoka kwa wafungwa una mamlaka ya kukagua na kusoma nyaraka nyingine yoyote.
Ntamamiro (Bwana jela) : Naomba soma Section 12 ya Prison Act.
Mhe. Lissu: Kwa kanuni hizi unaruhusa ya kusoma nyaraka nyingine.
Ntamamiro (Bwana jela) : Soma kifungu cha 12 cha Sheria ya Magereza
Mhe. Lissu: Unauwezo wa kusoma nyaraka za mawakili wanaokuja nazo magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sipaswi kusoma.
Mhe. Lissu: Hicho kifungu cha 12 unachosema kinahusiana na upekuzi wa magari na kumkagua mtu sio nyaraka ndio maana sitaki hata kukisoma. Hakikusaidii chochote.
Mhe. Lissu: Kisabo alisema wakiwaambia muondoke ili azungumze na mimi mteja wake mnakataa. Kweli au sio kweli.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Na mimi nimesema kwenye viapo vyangu kuwa alikuja Wakili Alute Lissu. Na kusema nina ujumbe muhimu kutoka serikali nataka niongee nae Faragha. Mkamkatalia. Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana jela): Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Umekuwa unaendeshwa na rimoti na Kamishna Mkuu na wanasiasa walioko serikalini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kuna siku umeniita ofisini kwako kuwa kuna ujumbe wa jumuiya ya madola napaswa kupelekwa mjini? Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sina Jibu.
Mhe.Lissu: Siku hiyo aliyekuja kunichukua ni Mangara?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: sio kweli nini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hujawahi kupelekwa.
Mhe. Lissu: Siku nyingine ulinifuata na kusema Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge Duniani amekuja kuniona anaitwa Martin Chungong na nikapelekwe mjini na Senior Mangara.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Kuna siku Heche, Amani na Mnyika uliwaruhusu kutokana na kulikuwa na maelekezo kutoka juu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kabla hujaja walikuwa wanaruhusiwa na ulipokuja ukawazuia hayo mamlaka ulitoa wapi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nimeshajibu.
Jaji: Ulijibuje
Ntamamiro (Bwana jela): Sikuwakataza.
Mhe. Lissu: Alipokuja Lema Godbless, wewe ulipokuja na kutukuta ulimfukuza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kama sio kweli kwanini haya yote hukuyajibu kwa nyaraka wakati mimi nimeyasema kwenye nyaraka zangu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Sasa kama umewazuia walalamikaji watatu, mashahidi wangu, umewazuia mawakili wangu. Unanitakia nini kwenye kesi ya uhaini inayonikabili ambayo adhabu yake ni mimi kunyongwa?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nilishajibu.
Jaji Mruma: Umejibu nini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sijamzuia mtu yeyote kuja kuonana na Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Sina swali lingine.
Majaji wanamuuliza Wakili wa Serikali.
Anasema naomba tuahirishe tuendelee kesho.
Wakili John Seka: Naomba tuendelee bado muda tunao.
Jaji Mruma: Sasa hoja ya kuahirisha na logistics zilivyo, TLS nao kupewa nafasi wamuhoji shahidi. Sisi tunaomba kusema yafuatayo.
Leo tutaahirisha kutokana na sababu kama za jana, tunaamini leo tumefanya kazi kubwa, kesho tutasema mengine.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 20.
Mhe. Lissu anaendelea kumshona Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza, Ntamamiro (Bwana Jela)
Mhe. Lissu: Wakati wote mawakili wakija gerezani, simamia, wapekuliwe na wamepekuliwa. Swali ni kwamba ni je wewe Bwana jela wa Ukonga unawashuku na una wasiwasi na mawakili 37 waliokuja kuona wateja Ukonga? Kumbuka kanuni inasena ili uwasearch ni lazima uwe na wasiwasi nao.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sitegemei kanuni.
Mhe. Lissu: Sasa twende kwenye sheria yenyewe kwenye Prisons Act kuwa unaweza kusearch mgeni kama hautakuwa na wasiwasi nae? Kifungu gani hicho?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa Majaji mtu yeyote anayeingia Gerezani awe mfungwa au mahabusu lazima apekuliwe.
Mhe. Lissu: Lazima apekuliwe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Yuko kimya.
Mhe. Lissu: Kama kweli ni lazima. Twende kwa Mawakili wa Serikali waliokuja Ukonga kama uliamuru wapekuliwe. Twende kwa hao sasa. Wah. Majaji SUPP 4 tarehe 19/11/2025 nenda haraka tumalize hii ngoma. Na Tarahe 21/01 mwaka huu.
Ntamamiro (Bwana Jela): Kila anayeingia lazima akaguliwe.
Mhe. Lissu: SUPP 4 inasemaje kuhusu Tarehe 19/11 walikuja mawakili wafuatao Debora Mushi kutoka NPS, Caroline Nana kutoka NPS pia, Cleoface Leonce ambae ni investigator na alikuja Justo Dimba au Simba kutoka kwa ZCO. na mwingine kutoka DCEA. Wote hawa shida walioijia gerezani walikuja kuongea na mahabusu. Maoni yako ukasema nini? Wasomeee majaji.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Wasikilizwe kwa utaratibu.
Mhe. Lissu: Wakija mawakili wengine simamia mazungumzo yao, wapekuliwe, wapekue, Simamia kwa ukaribu. Lakini wa serikali wakija wasikilizwe kwa utaratibu.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Mawakili 37 wote nipe mfano mmoja tu w wakili uliyesema asikilizwe kwa utaratibu.
Ntamamiro (Bwana Jela): Naomba Tar. 20/01 wakili hapo nimesema SIMAMIA.
Mhe.!Lissu: Ahsante sana. Sasa kwa mawakili wa serikali wapi hata mara moja umeandika SIMAMIA?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio lazima niandike.
Mhe. Lissu: Wabelgiji nilipokaa wanasema Papiere yaani Paper. Tunaenda na maandishi. Onesha maandishi acha rongorongo maneno mengi unatumalizia.
Sasa angalia majina yanayofuata. Hapo kuhusu mawakili wa serikali.
Ntamamiro (Bwana Jela): Niliandika Waletwe.
Mhe. Lissu: Maafisa wa Madawa ya kulevya na Mawakili wao waliokuja 28/11 kazi yao ni kutukamata na kutupeleka Mahakamani ndio unaosema wasikilizwe?
Ntamamiro (Bwana Jela): Hatoi jibu.
Mhe. Lissu: Hawa watu ni watumishi wa serikali kama wewe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli
Mhe. Lissu: Wanalipwa mshahara wa serikali kama wewe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio lakini.
Mhe. Lissu: Lakini utawapa mawakili wa serikali.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawa mawakili wa serikali huwa wanakuja kuongea na wote?
Mhe. Lissu: tuambie ni wapi umeandika kuwa walikuja kuongea na wote.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijaandika.
Mhe. Lissu: Ni sahihi kuwa kuna wakati nyaraka zinakataliwa na zinazokubaliwa lazima mseme zote. Kweli sio kweli mnafanya hivyo kwa mawakili wangu.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sio kweli zinasomwa. Ila zinakaguliwa.
Mhe. Lissu: la kwamba zinakataliwa pia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Katika nyaraka ambazo zinaletwa kwangu ni pamoja na hotuba ya Chande ya matukio ya tar. 29/10?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Lissu: Shahidi Paul Kisabo amesema wiki iliyopita Tar. 14/07 alikuletea waraka unaotoka common wealth kuwa niachiliwe ndani ya siku 30 na mliposoma mkakataaa.
Bwana Jela: Sio kweli.
Part 21 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 19
Mahakama Imerejea.
Majaji wameingia.
Wakili wa Serikali amesimama kujitambulisha anaitwa Narindwa Sekimanga.
Shaidi Mkuu wa Gereza nae yuko pale kizimbani yeye muda wote amekaa tu pale kizimbani.
Hajajihangaisha kusimama labda kwa vile ni mrefu na hicho kitambi anachoka kusimama pengine.😂
Jaji Mruma: Shaidi nakukumbusha bado uko chini ya kiapo.
Mhe Lissu: Sasa turudi kwa viongozi wangu wa Chama uliowakatalia wasije kuniona kule Gerezani. Angalia majibu yangu na uangalie kiapo kinzani kuhusiana na kiapo kinzani nilichomjibu Kisabo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ametoa macho. Hafanyi lolote.
Mhe. Lissu: Mawakili wa Serikali mnafanya nini si mumsaidie shahidi wenu azione hizo nyaraka naona ananiangalia tu.
Wakili wa Serikali anaenda.
Mhe. Lissu: Hizo aya kwenye kwenye kiapo changu kinzani zinaonesha namna ulivyowazuia viongozi na wanachama ikiwemo mashahidi na mawakili watatu ambao ni Dickson Matata, Deogratias Mahinyila na Gaston Garubindi. Swali langu waeleze majaji kama umewahi kupinga haya maelezo yangu yaliyopo kwenye kiapo changu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa Majaji nimeshalijibu hilo.
Jaji: Umeelewa swali lake kweli.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Nalo ni jibu pia. Haya kwenye aya ya nne wewe umefanya kampeni ya muda mrefu ya wewe na mlalamikiwa wa pili kamishna mkuu mmehakikisha nashindwa kujitetea wala kuandaa utetezi wangu na matukio nimeyasema kwenye para H na Y. kwamba umewazuia mawakili wangu watatu ambao Ni Mahinyila, Matata na Garubindi kama umewahi kujibu hili.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli nimewazuia.
Mhe. Lissu: Je umeleta supplimentary affidavit? Au majibu yoyote kwenye jambo hilo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : anatoa macho. Anashika makaratasi na kuyaacha.
Jaji: Umeelewa swali?
Mhe. Lissu: Ulileta counter affidavit mara ya kwanza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Baadae ukaleta suplimentary affidavit?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Sasa kwenye hizo nyaraka zako mbili kuna mahali kokote ulijibu tuhuma za kuwa umewazuia mawakili wangu na viongozi wa Chama?
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijajibu.
Mhe. Lissu: Tuhuma dhidi yako na maafisa wako kusearch mawakili na nyaraka zao kisheria. Jibu swali kwamba waleta maombi wote watatu wamesema wanasearchiwa, wanakaguliwa na kusomwa hizo nyaraka.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Reg. 17(2) ya kanuni za Magereza inasemaje?
Anatafuta hiyo kanuni.
Mhe. Lissu: Ni kweli mgeni anayekuja Gerezani kutembelea mfungwa atasachiwa endapo atakuwa na wasiwasi na huyo mgeni?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Haya isome sasa
Ntamamiro (Bwana Jela) : A prison officer when has any ground suspiciously may direct to search that visitor. Anasoma kingereza kibaya sana.
Mhe. Lissu: Any ground for suspicion may search or cause to search. Kumbe ataamuru asachiwe kama atakuwa na sababu za kumshuku?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Mgeni ataambiwa aondoke akikataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa mujibu wa kanuni hii ni kweli.
Mhe. Lissu: Anayemfukuza atatakiwa kuandika sababu za kumfukuza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : yuko kimya tena. Hebu rudia swali.
Mhe. Lissu anarudia swali. Si ni lazima uandike sababu za kumfukuza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Siku mjibu maombi wa Kwanza alipokataliwa kuingia gerezani tar. 28/11 alipokataliwa kuingia gerezani iliandikwa sababu kuwa amekataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kwa kanuni hii.
Mhe. Lissu: Tutajie kanuni hizo zingine tuzione? Kwenye kanuni kuna sababu yoyote nyingine kwa mujibu wa kanuni?
Bwana Jela: Sijaipitia kanuni yote.
Mhe. Lissu: Sasa mimi niliyepitia kanuni zote na hakuna sababu nyingine unasemaje?
Bwana Jela: Sina jibu.
Part 20 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam leo Jumatano Julai 22, 2026 Mch. Peter Saimon Msigwa amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Tundu Lissu.
Mch. Msigwa kabla ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 alitimkia Chama Cha Mapinduzi CCM kabla ya baadae kurejea Chadema, Chama ambacho amewahi kukitumikia kama Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, akiwa Mbunge pia kwa miaka 10 Iringa Mjini kupitia Chama hicho.
KITUKO KILICHOTOKEA MAHAKAMANI.
Wakati Mkuu wa Gereza yaani BWANA JELA ambae ni Andrew Shabani Ntamamilo alipohojiwa na Mhe. Tundu Lissu kuhusu Kuwazuia kabisa Mawakili kama Vile Deogratias Mahinyila, Dickson Matata lakini pia viongozi wakuu wa Chama akiwemo John Heche, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika na Amani Golugwa ambao ni mashahidi katika kesi ya Uhaini wamekataliwa kuingia Gerezani Ukonga.
Majibu ya Mkuu wa Gereza amesema yeye hajawazuia. Mhe. Lissu akasema basi watakuja kuanzia kesho. Akasema SITAWARUHUSU waingie kwasababu kesi bado iko mahakamani.
Jaji Amir Mruma ndio akaanza kumuhoji kuna amri yoyote ya Mahakama kuwa watu hawa hawapaswi kuja kumtembelea Tundu Lissu? Akasema kwa kiburi tena kuwa SITAWARUHUSU.
Jaji akavua miwani na kumuuliza unataka tufike huko. Uko serious kweli? Akiwa amekasirika sana. Maaskari Magereza walioko nyuma niliokaa nao karibu wamekimbilia nje kucheka.
Baada ya Jaji kukasirika Bwana Jela akaanza kuomba radhi kwa Jaji. Majaji wote watatu wametikisa vichwa vyao na kuonesha wanashangaa mambo haya yanawezekanaje kwenye Taifa lenye sheria na taratibu.
Kesi hii imeendelea tena kutuonesha watawala wa nchi hii wakoje. Ukisikia majibu ya Mkuu wa Gereza unajiuliza kiburi anakitoa wapi?
Ngoja tusubiri maamuzi ya Majaji mwisho wa kesi hii utakuwaje lakini naamini kila mtu anashuhudia uhalisia wa mambo ulivyo katika Taifa letu.
Tuendelee kusubiri lisaa likamilike turudi kuendelea.
Wanachama leo ni wengi mno. Mahakama imetapika. Yupo Makamu Mwenyekiti John Heche, Yupo Katibu Mkuu, Mnyika. Mama Suzan Lyimo, Mwenyekiti BAZECHA, Yupo Boniface Jacob Mwenyekiti Kanda ya Pwani, Dua Lyamzito, Katibu Mkuu BAVICHA, Pamela Massey, Katibu Mkuu Bawacha. Mzee Azaveli Lwaitama, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na wanachama wengine mbalimbali.
Tutaendelea kuwaleteeni live moja kwa moja mwenendo wa kesi hii kutokea Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 18
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu: Karibu ipi ambayo hawasikii?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Unaweza kuwa karibu na usisikie.
Mhe. Lissu: Kuna mawakili jumla 37 ambao umeleta nyaraka zao hapa pamoja na mawakili wangu. Sasa kwenye comment zako umekuwa ukisema simamia kwa karibi, simamia mazungumzo yao. Ni kweli kwa mawakili wote?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli lakini ni kweli naomba niseme ni kweli nimesema comment hizo kwa wote.
Mhe: Lissu: Katika Mawakili wote hao kuna mahali hata pamoja ulipoandika simamieni lakini msisikilize mazungumzo yao?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna
Mhe. Lissu: Je katika mawakili wote 37 umeandika wakiingia ofisini tokeni nje wazungumze ipo sehemu umeandika?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna nilipoandika.
Mhe. Lissu: Kuna mahali kokote umeelekeza kuwa angalieni lakini msisikilize?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna mahali hapo.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli au sio kweli kati ya Tar. 18/04/2025 nilikuwa nazungumza kwenye kioo na mawakili wangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kilikuwepo hicho kipindi.
Mhe. Lissu: Tulikuwa tunawasiliana kupitia simu zilizopo pale?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kweli
Mhe. Lissu: Je upande anaokuwepo mgeni ndio uko karibu na reception na kuna kachumba ambacho ni control room ya hizo simu zote? na kwenye hiyo control room anakuwepo afisa magereza anayeuwasha na kuuzima. Ili watu wazungumze yeye ndio anaamua hapo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni kweli.
Mhe. Lissu: Huyo Wakili anapozungumza kuna askari wanakuwepo kumsikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli a
Mhe.Lissu: Je huu upande wangu nakuwa pia na askari wananisikiliza niliotoka nao lockup na wengine wananisikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli.
Lissu: Kwenye hicho chumba kuna CCTV Camera inayorekodi kinachoendelea humo?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli
Mhe. Lissu: CCTV camera hiyo iko controlled ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana Jela): sio kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli kwamba baada ya matukio ya Oktoba 29 uliniita ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu : Ulivyoniita ukaniambia kuanzia sasa ni marufuku viongozi wa Chadema na wanachama wa Chadema kuja kukutembelea.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Na pia ulisema ni ndugu zako wa karibu tu ndio watakutembelea?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli
Mhe.Lissu: Na ukasema mazungumzo yako na mawakili yatakuwa kwa mambo ya kisheria tu?
Ntamamiro (Bwana Jela): sio kweli.
Mhe. Lissu: Wakili Gaston Garubindi alikuwa anakuja kunitembelea Gerezani kabla ya Tar. 14/11/2025
Ntamamiro (Bwana Jela) : kweli
Mhe. Lissu: kuanzia hiyo tarehe hajawahi kuruhusiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela): Simpangii.
Mhe. Lissu: Kuanzia niingie Gerezani Wakili Dickson Matata na Deogratias Mahinyila hujawahi kuwaruhusu waingie gerezani. Huyu Matata ni Mwenyekiti Kanda ya Magharibi na Mahinyila ni Mwneyekiti wa Vijana Taifa hawajawahi kuruhusiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela): Siwalazimishi waje au wasije.
Mhe. Lissu: Kumbe ndio hivyo. Haya Mahinyila na Matata kesho njooni Ukonga.
Ntamamiro (Bwana Jela): Kesi iko Mahakamani sitawaruhusu
Mhe. Lissu: John Heche, Amani Gorugwa, Katibu Mkuu Mnyika wakiwa kama mashahidi wangu kwenye kesi ya uhaini wamezuiwa kuingia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawawezi kuingia.
Jaji: Hilo la kwamba huwezi kuruhusu umelitoa wapi? Kuna amri yoyote ya Mahakama?
Ntamamiro (Bwana Jela): Siwezi kuwaruhusu.
Jaji Mruma: Tumefikia huko. Unaiambia Mahakama kuwa huwezi kuruhusu na hauna amri yoyote ya Mahakama? Uko serious kweli au hujaelewa ili tufanye maamuzi na sisi sasa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa majaji naomba radhi.
Jaji anamkata jicho
Mhe. Lissu: Soma hati yangu kinzani kuhusu Nashon Nkungu.
Anasimama Wakili wa serikali tunaomba Break.
Majaji wanashauriana.
Wakili John Seka anasema ni sawa tu.
Mhe. Lissu: Ni sawa.
Jaji basi tukutane mara baada ya lisaa limoja.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 17
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Na mazungumzo ya Kisabo pia ulisema yasimamiwe kwenye ofisi ya kaimu mkuu wa gereza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
Mhe. Lissu: Na tunakubaliana wale watu wote akina Mumbii, legal officer Stima, Kopro Dani, na akina mama watatu. Je hawa watu wanakuwemo humo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Si kweli. Huwa wanatoka. Wanaacha mazungumzo yafanyike.
Jaji: Lissu umeridhika na majibu ya shahidi.
Mhe. Lissu: Ngoja nataka kukamata watu waongo.
Mhe. Lissu: Kumbe maafisa wote mle chumbani wanatoka nje, sasa soma kiapo chenu ndugu yangu. Nakusomea kwenye kiapo chako
Kiapo kinasomeka kuwa walikuwepo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kuna ambao walikuwepo na kuna ambao walitoka.
Mhe. Lissu: Waliokuwepo ni akina nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waliosindikiza
Mhe. Lissu: Akina nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sikumbuki
Mhe. Lissu: Waleta maombi wote wamewataja majina akina Mumbii, Koplo. Dani, Akina mama watatu mle ndani, legal officer na mtu wa usalama. Wamewataja majina. Wewe unasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sikubaliani nao mimi.
Mhe. Lissu: Twende kwenye ofisi ya Recha ACP. Soma SUPP 4 Tar. 24/12 ulisema alipokuja Kisabo. Asimamiwe kwa kaimu mkuu wa gereza na kusema wayafanyie ofisini ukawataja majina ambao wanapaswa wasimamie. Waeleze majaji kuwa wakati wote Recha anakuwepo, asipokuwepo atakuwepo Mumbii, Mohamed lazima awepo au Hamisi na anakuwepo Stima na maaskari wanaonifuata muda wote.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sio kweli
Mhe.Lissu: Umewahi kuhudhuria mazungumzo hayo kwa Recha?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijawahi.
Watu wanacheka. 😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Tumewahi kufanya mazungumzo ofisi kwako mimi na mawakili wangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Tar. 12/12 imeandikwa SUPP 6 Umeiona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sioni
Mhe. Lissu: Mawakili msaidieni mmeleta wenyewe.
Ukiiona siku hiyo niliyosema tar. 12/12 ulielekeza hivi kaimu mkuu wa gereza, Mtu wa usalama na mwanasheria wa gereza ulisema mazungumzo yawe ya kisheria zaidi. Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli
Mhe. Lissu: Je hawa uliowaelekeza wote zaidi ya watu watatu walikuwepo au hawakuwepo kwenye haya mazungumzo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawakuwepo.
Mhe. Lissu: Walisikiliza au hawakusikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawakusikiliza.
Mhe. Lissu: Waliwezaje kusimamia mazungumzo wakati hawakuwepo na hawakusikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kuna facial impression.
Majaji wanacheka.😂😂😂😂
Ntamamiro (Bwana Jela): Naomba nifafanue.
Mhe. Lissu: Sitaki unifafanulie. Sasa kama hawakuwepo facial expression walizionaje wakati hawapo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hili suala ni la kisheria tunamkagua wakili kitambulisho.
Mhe. Lissu: Nani kakuuliza hayo.
Jaji: Usitupotezee muda. Hebu soma maelekezo yako kuwa wasimamie mazungumzo na watu hawakuwepo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ukiona wanakumbatiana hayaruhusiwi.
Jaji: Uliwaelekeza wafanye nini kwenye mazungumzo hayo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Walisimama mbali wakawa wanaangalia.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kitendo cha kukumbatiana ni maneno au kitendo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni kitendo.
Mhe. Lissu: Ulisema wakasimamie vitendo au maneno?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mazungumzo yaani maneno.
Watu wasonya tu. Majaji pia wamekasirika sana kwa majibu haya. Watu wengine wanacheka kimya kimya.
Mhe. Lissu: Sasa twende SUPP 6 ukurasa unaofuata. Wapo mawakili watatu ambao ni Catherine Chanjarita, Shamumoyo na Constatine kwenye comment zako umesema Adm. Officer simamia mazungumzo yao kwa karibu. Sasa swali langu simamia kwa karibu yanawezekana kutekelezwa bila maaskari hao kuwepo kwenye mazungumzo hayo?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijasema wasikilize nimesema wasimamie kwa karibu.
Part 18 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
VIDEO:
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka Mkoani Iringa Mchungaji Peter Msigwa leo, Jumatano Julai 22.2026 ni miongoni mwa wadau waliofika kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia mwenendo wa shauri la Kikatiba lililofunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mkuu wa Gereza Ukonga, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tundu Lissu
Shauri hilo la Kikatiba lililofunguliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma inayoketi Dar es Salaam, linasikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu (3) linaloongozwa na Jaji Amir Mruma
Waleta maombi katika shauri hilo waliojitambulisha kuwa ni Mawakili wa Tundu Lissu wanalalamikia kuzuiliwa na/ au kunyimwa faragha ya kuzungumza na mteja wao wanapomtembelea Gerezani
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 16
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Mkuu wa Gereza
Mhe. Lissu: Twende Taratibu. Hiki ulicholeta mahakamani ni photocopy?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
Mhe. Lissu: Original unayo ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Angalia Tar. 29 na Tar. 30 Sept. 2025. Kuna majina ya wageni kabla ya Tarehe hizo wapo wageni hawaonekani walikuja tarehe gani?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli
Mhe. Lissu: Hawa watu wanne walikuja tarehe ngapi? Wambie majaji sasa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Haioneshi.
Mhe. Lissu: Wewe unajua sasa? Walikuja tarehe ngapi? Maana original unayo wewe.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Tarehe haioneshi.
Mhe. Lissu: Je katika hao watu wa nne. Mtu wa 10 ni nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Paul Kisabo.
Mhe. Lissu: Alikuja kumuona nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : wewe hapo imeandikwa. Alikuja kukuona wewe.
Mhe. Lissu: Soma Tar. 30 Sept. Kwenye karatasi hiyo hiyo. Mtu wa kwanza ni Paul Kisabo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Tusiende mbali sasa: Tufafanulie jambo hapa kuna sehemu imenadikwa jina la ndugu, ID no. Simu namba, atokapo mgeni na maoni ya OIC. Sasa hiyo OIC ni Officer in Charge yani wewe hapo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Tar. 30/09 kwenye jina la Kisabo uliandika A/Zamu maana yake Afisa wa Zamu. Na kuna mahali umeandika ADM maana yake ni admission office in charge. Na kuna mahali umeandika IO maana yake intelligence officer?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: na kuna sehemu umeandika legal unamaanisha Legal Officer Stima.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
Mhe. Lissu: Hiyo sehemu ya maoni yako ni maelekezo yako kwa hawa niliowataja? Wewe ndio Boss.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kila ofisa ana kazi yake. Kwahiyo ni maelekezo yangu kwao.
Mhe. Lissu: Kwahiyo unakuwa umewapa amri?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Nenda Kwenye kilelezo SUPP 3 pia ni orodha ya mawakili waliokuja Ukonga. Nashon Nkungu lipo hapo ambae ni mlalamikaji wa pili. Andrew Mathew Chima pia alikuja kuniona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Je Andrew Chima yupo kwenye orodha ile ya mawakili wangu niliowaletea ile SUPP 1?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hayupo. Naomba nifafanue.
Mhe. Lissu: Sitaki. Utawafafanulia wa Serikali.
Haya huko mwisho kabisa KULWA MADUHU yupo au hayupo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Yupo namuona hapa.
Mhe.Lissu: Na kule mwisho kwenye maoni yako umesema aruhusiwe mwenye kibali. Maduhu hana kibali huko mbele sioni.
Ntamamiro (Bwana Jela): hayuko kwenye orodha ya mawakili wa mahabusu huyu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kuna sharti lolote la kisheria kwamba mfungwa yeyote mwenye wakili au wakili anapaswa kuwasilisha orodha ya mawakili wake kwa Bwana Jela?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Halipo kisheria. Lakini mfungwa ana haki ya kuchagua nani amtembelee.
Mhe Lissu: Nilichagua kuwa Kulwa William Maduhu na umemkatalia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuwepo kwenye orodha.
Mhe. Lissu: Andrea Chima alikuja kuniona yupo kwenye orodha gani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hayupo.
Mhe. Lissu: SUPP 5 twende sasa tar. 24/12/2025 angalia kwenye entry kuna Nashon Nkungu na Paul Kisabo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio wanaonekana wote.
Mhe. Lissu: Je Victoria Mgonja alikuja kumuona Jonson Muhanjo. Uliandkka kwenye maoni yako kuwa Adm. Simamia mazungumzo yao. Na mazungumzo hayo yalifanyikia kwenye ofisi ya Admn
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina kumbukumbu yalifanyikia wapi?
Mhe. Lissu: Kwamba tangu juzi tunazungumza kuhusu mazungumzo ya mawakili yalifanyikia wapi hujaenda kutafuta.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijui inaweza kuwa kwa Mkuu wa Gereza au Adm.
Mhe. Lissu: Mazungumzo na Nashon ulisema asimamiwe kwa Makamu mkuu wa gereza na kuwataka wasaidizi wako wanne wasimamie?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Part 17 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 15
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Mkuu wa Gereza, Ntamamiro (Bwana Jela)
Mhe. Lissu: Je askari magereza ambae hasikii au hauoni atashuhudiaje mazungumzo ya mfungwa na ndugu zake watakapokuja kumtembelea
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hayo ni masuala ya kidaktari.
Mhe. Lissu: Sasa Bwana Jela hujui kama wasaidizi wako wote hao kuwa hujui kama wanasikia au hawaoni wewe ni mkuu wa gereza wa aina gani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sik daktari.
Mhe. Lissu: Wewe ni Mkuu wa Gereza wa aina gani? Usiyejua afya za wasaidizi wako?
Ntamamiro (Bwana Jela): Nastahili kuwa kwenye nafasi hii.
Mhe. Lissu: Ndio maana nchi imekwama. Kama watu wenyewe ndio nyie na akili hizi
Mhe. Lissu: Umekuwa Officer incharge tangu lini pale Ukonga?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sept. 2025.
Mhe.Lissu: Ulihamishiwa Ukonga ukitokea gereza kuu la maweni Tanga?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio.
Mhe.Lissu: Ulikuja ukonga kuchukua nafasi ya Juma Mwaibaku?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli.
Mhe. Lissu: Ulipohamishiwa Ukonga mimi tayari nilishakuwa mahabusu ukonga toka April 2025?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Wakati unahamia Ukonga ulikuta nakaa kwenye special wing pale ukonga?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli
Mhe. Lissu: Wakati unahamia pia ulinikuta naishi huko pamoja na wafungwa wa adhabu ya kifo 100?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sikuwakuta.
Mhe. Lissu: Je ulinikuta nakaa peke yangu au sio peke yangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio peke yako.
Mhe. Lissu: Wafungwa gani hao?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mmoja.
Mhe. Lissu: Je kwa miezi 5 ambayo hukuwepo nilikuwa naishi na wafungwa wa kifo takribani 100?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sifahamu.
Mhe. Lissu: Umeona record ya maandishi ya waliokuwepo special wing umeiona au hujaiona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijapitia hiyo records.
Mhe: Lissu: Hili suala nilishalilalamikia na lipo kwenye nyaraka za mahakama.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sifahamu. Tuendelee na maswali mengine.
Mhe/ Lissu: Utaratibu wa wageni kuja kuniona ni weekend?
Ntamamiro (Bwana Jela) : kweli
Mhe. Lissu: Utaratibu wa wageni wangu kuja kuniona weekend ni kwamba siku moja wanakuja ndugu zangu na siku nyingine wanakuja viongozi wa Chama.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sifahamu.
Mhe.Lissu: Wakati unahamia Ukonga ulikuta utaratibu wa kutembelewa na mawakili wangu ilikuwa nimepeleka orodha kwa mkuu wa Gereza kwa mkuu wa gereza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Orodha ya kwanza uliiambatanisha kwenye hati yako ya kiapo kinzani ile ambayo nilikuwa na mawakili 10.
Ntamamiro (Bwana Jela): Orodha hiyo hiyo moja.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hakukuwa na orodha yenye jina la Deogratias Mahinyila, Paul Kisabo na Dickson Matata na Mary Stephano.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna hiyo.
Mhe. Lissu: Angalia kielelezo SUPP 1. Ukishakiona niambie.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Anapekenyua hapa..
Mhe. Lissu: Jina la Nashon Nkungu limo kwenye hiyo orodha lipo au halipo? Ambae ni mleta maombi wa pili.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio lipo.
Mhe. Lissu: Je jina la Kisabo na Maduhu mawakili wangu yapo au hayapo kwenye hiyo SUPP 1
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawa hawapo kwenye hii orodha.
Mhe. Lissu: Sasa hao wawili wamesema kwa kiapo na kusema hapa Mahakamani kuwa kabla hujahamia ukonga walishaingia gerezani kuonana na mimi walishaingia karibia mara tatu. Wewe unasemaje? Yaani wakati ACP Juma Mwaibako akiwa Mkuu wa Gereza walihudhuria
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama ulikuwepo wakati huo?
Bwana Jela: Sikuwepo wakati huo. Ila nyaraka zinasema.
Mhe. Lissu: Nenda kielelezo ambacho ni SUPP 2 hapo.
Jaji: SUPP 2 ni nini?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hiki ni kiambatanisho na. 2 kinahusu orodha ya wageni na mawakili waliotembelea gereza la Ukonga.
Part 16 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Mh. @TunduALissu Swali ni je, kubadilisha kanuni za wizara ana uwezo huo?
Ntamamiro (Bwana jela ) Nashindwa kuelewa. Huwaga tunawambia kila siku mwachieni Lissu matokeo yake nashindwa kuelewa 😂😂 #FreeTunduLissu
#TANZANIA: MSIGWA ATINGA MAHAKAMANI KESI YA LISSU KWA MARA YA KWANZA
Peter Msigwa leo Julai 22, 2026 amefika Mahakamani kwa mara ya kwanza kufuatilia mwenendo wa kesi ya Mwenyekiti wake wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam.
Zaidi: https://t.co/JNg8zw3qMq
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 14
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Mkuu wa Gereza, Ntamamiro (Bwana Jela)
Mhe. Lissu: Mmeleta PSO hapa?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio mawakili wangu waliileta.
Jaji: Wakili wa serikali nenda kaongee na shahidi wako anajua.
Mhe. Lissu: Sasa Shahidi nataka tuzungumze juu ya utaratibu wa mazungumzo kwa wafungwa au mahabusu? Tuanzie hapo. Soma kanuni ya 9(h) ya kanuni za usimamizi wa magereza. Je ni kweli wafungwa wana haki ya kutembelewa gerezani?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli.
Mhe. Lissu: Wafungwa watatimiza haki hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya kanuni hizo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni kweli
Mhe. Lissu: Soma kanuni ya 12(5) inasemaje? Je kwa kanuni hiyo wafungwa wanapotembelewa na wageni wao mazungumzo yao yatafanyika kwa kuona na kusikilizwa na afisa gereza mmoja?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sawa kwa kanuni hii.
Mhe. Lissu: Inahusu wageni wote wa wafungwa?
Ntamamiro (Bwana Jela): inategemea.
Mhe. Lissu: Utaratibu wa kutembelea wafungwa wa kifo na wa kawaida ni tofauti?
Ntamamiro (Bwana Jela): Inategemea.
Mhe. Lissu: Je askari mmoja kwa wafungwa wa kawaida na askari wawili wa wafungwa wa kifo. Utaratibu wa kutembelewa kwa wafungwa na watu wa kawaida na mawakili wao ni sawa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa mawakili askari ataona lakini hatasikiliza.
Jaji Rumisha: Si unaona tunaenda vizuri sasa Lissu.
Mhe. Lissu: Vizuri kabisa sasa shaidi tuambie mkuu wa gereza la ukonga una matatizo ya kusikia au hauna?
Ntamamiro (Bwana Jela): niko vizuri mimi. Nasikia.
Mhe.Lissu: Assistant Commisiomer on Prison Recha. Ana matatizo ya kuona na kusikia au hana?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui.
Watu wanacheka kimya kimya. Boss hajui kama msaidizi wake anasikia vizuri au laa😂
Mhe. Lissu: Je ACP Mumbii nae ana matatizo ya kusikia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sio Daktari sijui.
Mhe. Lissu: Je ACP Mohamed nae?
Ntamamiro (Bwana Jela): nae pia sijui kama ana matatizo ya kusikia.
Mhe. Lissu: SGT. Hamisi vipi nae anasikia au hasikii?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijui.
Mhe. Lissu : Insp. Stima legal officer nae vipi anasikia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nae pia sijui.
Mhe. Lissu: Wale akina mama watatu wanaofanya kazi admission office wana matatizo ya kusikia na kuona au hawana?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui.
Kwa Kifupi kesi imeanza sasa.😂😂😂
Mhe. Lissu: Koplo Dani mtunza fedha nae vipi ana matatizo ya kusikia au vipi? Maana na yeye mara zote huwa yuko ofisi ya admission?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijui.
Mhe. Lissu: Wale maaskari ambao huwa wanatoka na mimi ninakolala na kunileta kwako Insp. Kaisi na Mwingia wakiongoza nao pia huwa wanatatizo la kusikia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijui.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji umefanya kazi Magereza kwa miaka mingapi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni mingi tu.
Mhe. Lissu: Mingapi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Zaidi ya 25
Mhe. Lissu: Uliingia mwaka gani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : 1995.
Mhe. Lissu: Kwahiyo ni miaka 31?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
Mhe. Lissu: Umepitia mafunzo mbalimbali jadi kufikia cheo ulichonacho sasa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni sahihi.
Mhe.Lissu: kwahiyo wewe ni msomi wa masuala ya magereza hadi umefikia hapo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Mhe. Lissu: Je kwa uzoefu wako jeshi la magereza linaweza kuajiri askari haoni au hasikii?
Ntamamiro (Bwana Jela) : haliwezi kuajiri. Lakini unaweza kuumwa ukiwa kazini.
Mhe. Lissu: akiajiriwa haoni akapofuka ataendelea kuwa askari magereza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sio daktari
Watu wanacheka.😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Kama atakuwa hasikii je ataendelea kuwa askari magereza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Hata kutokuwa na jibu ni jibu pia.
Mhe. Lissu: Je askari magereza ambae hasikii au hauoni atashuhudiaje mazungumzo ya mfungwa na ndugu zake watakapokuja kumtembelea.
Part 15 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 13
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Ntamamiro (Bwana Jela)
Jaji: Sasa Bwana jela umeulizwa kuhusu kanuni tu. Jibu kwenye kanuni
Mhe. Lissu: Huko tutafika anakotaja anijibu tu ni kanuni gani inasema mfungwa wa kawaida atalindwa na askari wawili?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kwa kanuni hii hakuna kokote.
Mhe. Lissu: Kwa kanuni hizo wafungwa wamegawanywa kwa makundi matatu? Au unataka nikutajie?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nitajie?
Mhe. Lissu: Fungu la tatu soma wapo watoto, wapo wafungwa wanaoitwa star prisoners, na kundi la tatu ni wafungwa wa kawaida?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Hao wanaoitwa young prisoners ni wenye chini ya miaka 21.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli
Mhe. Lissu: Wanaoitwa wafungwa nyota ni wale first offenders? Wamefanya kosa kwa mara ya kwanza?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli
Mhe. Lissu: Oridnary ni wale wafungwa wengine wanaobaki wote wasio kundi la kwanza na la pili?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Jana ulimsikia Kalokola wakili wa serikali akisema kuna wafungwa wa umuhimu wa kisiasa au alisema Prisoners of Security Importance Je kwa kanuni hizo wapo?
Ntamamiro (Bwana Jela): Majaji mimi naongoza kwa mujibu wa sheria zingine pia ila Kwa mujibu wa kanuni hizo hawapo.
Mhe. Lissu: Sasa twende kwenye Sheria yenyewe. Soma kifungu cha 29 kinahusu classification of Prisoners.
Bwana Jela anakitafuta kwa muda mrefu sana.
Mhe. Lissu: Hawajakuandaa hawa watu. Unatumia muda mrefu sana kutafuta kifungu. Na niliwaambia.
Sasa nikwambie inasema hivi utatenga wafungwa kama walivyoelekezwa na sheria kwa makundi. Kweli au sio kweli?
Au nikusomeee?
Ntamamiro (Bwana Jela): sikioni.
Jaji: Msajili nenda kamsaidie akione.
Mhe.?Lissu: Ni kweli kifungu hicho kinasema unapaswa kutenga kwa zile classification tatu nilizosema?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli
Mhe. Lissu: Eheeee unawatenga vipi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Nimesema tunaongozwa na kanuni, sheria na miongozo mbalimbali.
Mhe. Lissu: Tulitoka kwenye kanuni sasa tupo kwenye sheria muda huu.
Ntamamiro (Bwana Jela): Naomba nipewe muda.
Jaji: Sasa Wakili wa Serikali ongea na shahidi tunataka kusogea mbele. Msaidie anachotafuta.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni sahihi kuwa sheria inasema kama ulivyosema.
Mhe. Lissu: Je wewe mkuu wa gereza la ukonga au mkuu wa gereza lingine mnaweza kubadili makundi hayo matatu tuliyosoma kwenye sheria. Na kuweka category nyingine nje ya za kwenye kanuni?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina uwezo huo.
Mhe. Lissu: Haya Makanuni hatujayatunga wewe, wewe jibu tu swali chakufia nini? Sasa tuambie Kamishna wa Magereza kama nae ana mamlaka ya ku change category za wafungwa zilizopo kwenye kanuni. Je Boss wako anayo hayo mamlaka? Yaani Principal Commissioner
Ntamamiro (Bwana Jela): Hana uwezo.
Jaji: Hebu tueleze vizuri.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa sasa Commisioner General wa magereza anao uwezo wa kutunga kanuni zingine.
Mhe. Lissu: Swali ni je kubadilisha kanuni za Waziri ana uwezo huo?
Ntamamiro (Bwana Jela): nashindwa kuelewa.
Jaji: Sasa Shahidi hizi kanuni narudia tena hukutunga wewe. Jibu tu swali.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hana uwezo wa kurekebisha wala ku ammend. Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Kifungu cha 105(1) kinasema kwa kifungu hicho ni waziri peke yake ndio mwenye mamlaka ya kutunga kanuni za utekelezaji bora wa kanuni hizi?
Jaji: Lissu endelea kuuliza swali.
Mhe. Lissu: Sasa jibu swali langu la mamlaka ya kutunga kanuni bora za utekelezaji wa kanuni hizo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Haisemi Waziri peke yake.
Mhe. Lissu: Waziri anaweza au hawezi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Anaweza.
Mhe. Lissu: Ni wapi pameandikwa kuwa Kamishna General anaweza kutunga kanuni?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sipaoni hapo.
Part 14 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.