Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) jana tarehe 19 Disemba, 2023 amefanya ziara ya kukagua huduma za afya zinazotolewa katika kituo cha afya cha Mbutu Kichangani, kilichopo katika kata ya Somangila, Wilaya ya Kigamboni.
Nakiri changamoto ya foleni barabara ya Tungi-Kisiwani-Kibada. Magari yamekuwa mengi sana.
Mpango wetu ni kuboresha njia za mchepuko kutoka Feri na Darajani kwenda maeneo mbali mbali ya Kigamboni ikiwa ni pamoja na barabara za Tungi-Maweni na Mkorea-Ungindoni.
Kukatika kwa umeme ni tatizo la kitaifa. Nimeendelea kuwasisitiza @tanescoyetutz kuzingatia ratiba za upatikanaji wa umeme wanazotoa.
Zaidi ya hapo, tunaendelea na zoezi la usambazaji wa umeme, tumefikia mitaa 66 kati ya 67. Tutahitimisha agenda hii kabla ya mwisho wa mwaka huu.
TAARIFA
Zoezi la kutia saini utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibada-Mwasonga-Tundwi Songani (41km) utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 4 Septemba, 2023 Mwasonga centre, Kata ya Kisarawe II kuanzia saa 2 asubuhi.
Tujitokeze kwa wingi kushuhudia zoezi hili muhimu.
Hata wale watakaouziana kupitia kwa wanasheria, utaratibu wa kupitisha mikataba WDC utatumika pia.
Aidha, niwaombe wananchi tushirikiane kupunguza utapeli na migogoro ya ardhi.
Hivyo, kabla ya kununua ardhi tuulize mamlaka na majirani wa eneo husika.
Sambaza ujumbe huu.
Ili kupunguza migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Kigamboni, Halmashauri imeweka utaratibu mpya. Kuanzia sasa ununuzi, upimaji na uandaaji wa michoro mipango miji NI LAZIMA upitie Kamati ya Maendeleo ya kata ya husika (WDC). Utaratibu wowote bila IDHINI ya WDC hautatambuliwa.
Manispaa ya Kigamboni imedhamiria kuboresha sekta ya elimu. Moja ya mkakati huo ni kutenga fedha za ndani kwa ajili ya kutengeneza madawati. Lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora iliyo kwenye mazingira bora.
Pichani: Mbunge Ndugulile na Mkurugenzi Ndugu Erasto Kiwale
Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile leo amekagua mradi wa kutandaza mabomba ya maji unaofanywa na DAWASA na kunufaisha kata za Mjimwema, Somangila na Kibada.
Ujenzi wa tanki la lita millioni 15 umeshakamilika. Ujenzi wa mtandao wa mabomba km 62.5 unaendelea.
"Leo Bungeni nimeuliza swali kuhusu mikakati ya Wizara ya Ujenzi ktk kutatua changamoto ya usumbufu kwa wakazi wa Kigamboni wanaotumia Daraja la Nyerere kutokana na ujenzi wa barabara ya mwendokasi na flyover malori yanayoingia nakutoka bandarini na uwepo wa mizani" @DocFaustine