TEACHER|POLITICIAN|ADVISOR OF ECONOMIC DEVELOPMENT|MEMBER OF CCM PARTY|MEMBER OF RESTLESS DEVELOPMENT|FORMER SECRETARY OF UVCCM TABORA TEACHERS COLLEGE
William Ruto anapopata nafasi ya kuongea huwa hafanyi makosa ameongelea Afrika na changamoto zake huyu kweli ni kiongozi, ila wetu alikuwa anasoma tu yaliyobandikwa
Ruto kwenye speech ni mnyama sana huyu ndio maana wakenya huwa wanasema usimpe muda wa kujieleza Ruto 🙌🙌🙌👇👇
"Mafanikio katika maisha ni NIDHAMU,IMANI na MATUMAINI.Ukiwa na haya 3 hakuna mlima utakaoshindwa kuupanda,hakuna ukuta utaoshindwa kuruka." ~Togolani Mavura.
"Zipo kanuni za maisha za kudumu tunazipuuzia kwa kuhisi tunajua sana au zaidi ya waliotutangulia na hatimaye tunarudia makosa yaleyale." ~Togolani Mavura.
"Kwenye mitandao ya kijamii kuna karama,vipawa na taarifa nyingi sana. Ni kisima cha maarifa na taarifa kwa mtu mwenye moyo wa unyenyekevu na akili ya udadisi." ~Togolani Mavura.
Mjaluo wa Nairobi, aliyepiga soka kipaji kikaonekana. Akiwa na miaka 17 watu wakachanga pesa wakamsafirisha kwenda Spain. Akiwa huko wakala wake akamtelekeza, akakosa hadi nyumba ya kuishi ila akasaidiwa na timu yake ndogo. Leo hii Job Ochieng anachezea Real Sociedad ya La Liga
Mwanaume mwenye mipango anahitaji Mwanamke anayetambua kuwa mafanikio ni mchakato. Kujenga maisha ya maana tena yenye mafanikio sio jambo jepesi. Mwanamke sahihi ataelewa ugumu wa mchakato na uvumilivu unaohitajika. Mwisho atakuwa mnufaika wa matunda ya Mafanikio.
"Katika kwaya kuna sauti ya kwanza, ya pili ya tatu mpaka ya nne na hupokezana kwa kuimba na kupishana. Kila sauti ina umuhimu tu kwa wakati wake. Usidandie kuimba katika zamu isiyo yako. Na maisha ndivyo yalivyo." ~Togolani Mavura.
Seneta Risch, Mwenyekiti Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Seneti la USA amekataa msamaha ulioombwa na mtoto wa Museveni aliyeituhumu Marekani kwa kumtorosha Bobi Wine. Seneta huyo amesema Muhoozi amevuka mstari mwekundu na Marekani lazima itazame upya ushirikiano wake na Uganda
Nafikiri baadhi yetu tumemuona Pacome baada ya mchezo aliamua kuingia kati na kuongea na wachezaji wake. Sijui alitumia lugha gani kuongea, ili wenzake wamuelewe lakini hata angetumia lugha ya kwao kila mtu angeelewa tu. Ni Nadra sana kumuona Pacome akinena. Ukiona amenena basi anaamini tunapaswa kufanya jambo kubwa zaidi. Tuna kazi ya ziada Morocco. Kila mmoja wetu anatambua fainali yetu ipo Morocco
UKO WAPI MZEE ABDULRAHAMAN KINANA?. MWISHOWE UMEMPONZA SIMBACHAWENE
Mwl John Pambalu
Iko hivi,
Ukiwa na mke, ukakengeuka. Ukaacha kutoa matumizi, hakulalamikii. Ukawa na wanawake wa nje, hakulalamikii. Ukawa unalala nyumba ndogo, bado hakulalamikii.
Siku akinyamaza kabisa, jua wazi: ulishakoma kuwa mume kwake.
Hiyo ndiyo hatua tuliyofikia kama taifa. CCM, chama kinachotawala japo kwa mabavu, umma umeshakoma kukieleza shida zake kwa matumaini ya kutatuliwa. Ndiyo maana leo watu wanajichukulia sheria mikononi mwao. Kahama watu wameandamana mgodini. Bariadi gari limechomwa moto. Karibu kila kona ya nchi, hali ni ileile, hasira iliyofikia kikomo.
Imefika hatua serikali hii, iwe inafanya jambo jema au baya, umma hauulizi, hauitikii, wala haujali. Sio kwa sababu wamekubali, bali kwa sababu wamesha move on. Taifa limeachana na CCM na utawala wake.
Mimi kama mwanasiasa kijana, sitamani CCM ife na kupotea kabisa. Kwa sababu ukweli mchungu ni huu, chama hiki bado kinashikilia dola japo kwa mabavu. Kadiri kinavyozidi kupoteza ushawishi wa kisiasa kwa umma, ndivyo kinavyozidi kuimarisha ukandamizaji, ukatili na hofu kwa raia.
Kadiri nguvu ya ushawishi wa kisiasa inavyopungua, ndivyo tutakavyowaona watu wa aina ya Murilo wakitumika kujibu hoja kwa vitisho vipigo, utekaji na mateso ya maporini kama ilivyotokea Aprili 24, 2025. Haya yote ni kwa sababu mfumo wa kupambana kisiasa kwa hoja wakina Kenani Kihongosi na Asharose Migiro kazi imewashinda, wamekata upepo. Watoto wa mjini wanasema: “wamekata kabisa.”
Sasa, kwa nini leo nimemkumbuka Mzee Abdulhamid Kinana?
CCM ya awamu ya Samia imefikia hatua ya kupoteza ushawishi na uwezo wa kuongoza mjadala wa kitaifa (public agenda) kwa sababu ya uovu, dhuluma na udharimu wa kutisha unaotekelezwa na serikali, mawakala wake au na machawa wake.
Hali kama hii, ingawa ilikuwa na nafuu kidogo ilitokea kati ya mwaka 2010 hadi 2015 chini ya utawala wa ndugu Kikwete. Serikali ilinuka rushwa kuanzia Ikulu hadi kwa mjumbe wa nyumba kumi. Kila kukicha, kashfa mpya: Richmond, EPA, Kagoda, IPTL. Ufisadi bandika bandua.
CCM ikatafuta Katibu Mkuu wa kurejesha angalau matumaini. Kila aliyejaribiwa, kazi ikawa nzito kama kwa mama Asharose Migiro. Hata Mukama alipoinuliwa, hali ikakwama. Ndipo akaibuka Abdulrahman Kinana.
Mzee akachukua vipaza sauti, akatembea mkoa kwa mkoa, akawaita mawaziri wa Kikwete mizigo, mafisadi na wezi. Kikwete akanyamaza kimya. Kinana akazunguka na script iliyochorwa, akivuta waliokata tamaa. Chama kikaanza kuonekana kama kimeamka. Watu wakaanza kusema, “huenda bado kuna matumaini.”
Matokeo yake, tukaingia uchaguzi wenye mvutano mkubwa kati ya Lowassa na Magufuli mwaka 2015, Magufuli akakwepa kutumia nembo na jina la CCM akawa anasema Tanzania ya Magufuli, akakwepa kutumia alama ya jembe na nyundo. Akaanza kutumia alama ya mwenge ambayo ni ya UVCCM (Kinana style). Yaliyotokea yamebaki historia, wapumzike kwa amani.
Sasa nirudi kwenye hoja yangu kuu: CCM ya sasa haina uwezo tena wa ku-set public agenda.
Ndiyo maana wanazungumza amani wakati umma unazungumza haki. Kila mbinu wanayojaribu, ina-backfire. Mama akaanza kwa kuzungumza na wazee wa Dar, aka-set agenda kuwa waliouawa walichokoza dola kwa kuchoma miundombinu. Narrative hiyo haikudumu hata saa 72, umma ukaikataa.
Akaja Mwigulu, akadai watu walilipwa kuchoma nchi, kuna mtu alipewa bilioni tano yuko Afrika Kusini. Nayo ikafa kifo cha kawaida.
Wakamtoa Kihongosi, hajulikani alianza wapi wala aliishia wapi, nayo ikafa, alidhibitiwa na kauli moja tu ya mzee Warioba, kijana acha mzaha kwenye maisha ya watu. Akapotea mazima
Wakawainua Wakatoliki wa Vikojora na Wakorinthio, nao wakaishia pale pale. Umma ukawakataa. Hii mbinu ikaleta mvutano mkubwa kati ya waumini wa kanisa Kikatoliki na dola. Nayo hiyo mbinu ikafa vile vile.
1/2
"Ndugu wa tumbo moja wanapatana zaidi ukubwani wakikaa mbali mbali kuliko wakiishi pamoja. Wakiishi pamoja ni rahisi kufitinishwa aidha na nongwa za toka utotoni au masimango ya wakubwa kwa fadhila walizowapa wadogo zao zamani." ~Togolani Mavura