"Neno la kutia moyo:
Nikiwa kama mgonjwa mkongwe napenda kuwapa moyo wagonjwa wenzangu kuwa kuishi ugonjwa adimu hakukuwekei mipaka ya kuwa mtu mkubwa na kuleta athari chanya katika jamii inayokuzunguka." Ms. Getrude Maruma mgonjwa wa #MyastheniaGravis#rarediseaseday2020
Watoto kama @AliKimara na #MalcolmTheBeliever wanahitaji elimu bora pasipo na shule. Muda umefika kuangalia upya sera zetu ili tusiwabague watoto wanaoishi na magonjwa adimu. #RareDiseaseDay
Moja ya changamoto kubwa inayowakabili watoto wenye magonjwa adimu ni shule. Magonjwa haya huwazuia watoto kuhudhuria shule kama kawaida hivyo hukosa fursa wanazofaidi watoto wenzao wasiosumbuliwa na magonjwa adimu.
"Wazazi wetu wetu wapendwa, najua mmebeba mizigo mizito sana ila nataka kuwahakikishia kwamba watoto wenu ni Baraka. Katika watoto hao wapo madaktari, wahandisi, wanauchumi, wataalamu wa ustawi wa jamii, viongozi na watu wa taaluma nyingine mbalimbali."
#rarediseaseday2020