Hawa wapuuzi walifurahi sana EU imesitisha misaada walikuwa wanajiona wameshinda vita
Leo hii misaada imerudi wamebaki wanatafuta maneno
Maria Sarungi na timu yako, haya ndiyo matokeo ya kuuza uongo
Propaganda ina muda wake. Leo muda wake umeisha.😂🫵
#LimewashukaWanaharakati
Tanzania’s €156 million EU development programme is back in focus. The European Commission confirmed that the full allocation was made available from 23 July 2026, following months of uncertainty. The next test is implementation and measurable public benefit. #Wanaharakatichali
Ni jambo la kushangaza kuona kiongozi anayejiita wa upinzani ambaye kila siku amekuwa mstari wa mbele kubeza na kupinga uwepo wa serikali iliyopo madarakani leo anaamka na kuanza kutoa maelekezo ya jinsi serikali hiyo hiyo inavyopaswa kuendesha wizara zake.
Bwana @godbless_lema unapaswa kujibu swali moja lakini lenye uzito mkubwa wa kikatiba na kimsimamo.
Hivi ni tangu lini umeanza kuitambua rasmi Serikali hii iliyopo madarakani pamoja na Viongozi wake wateule?
Siku zote umekuwa ukituambia wananchi kwamba hauitambui serikali hii huku ukinyoshea vidole kila hatua inayochukuliwa na kutangaza kuwa mko nje ya mfumo wa utawala uliopo.
Leo hii imekuwaje umeanza kuichimba Wizara ya Maji na kutoa ushauri kana kwamba umeamua kuwa mkuu wa idara ya ufuatiliaji ndani ya serikali hiyo hiyo?
Je hii ina maana kwamba sasa hivi umetambua rasmi kuwa Serikali ya Awamu ya Sasa ni halali na ina viongozi halali wateule na ina mamlaka kamili ya kusimamia rasilimali za nchi?
Ama huu ni muendelezo wa siasa za fursa ambapo serikali ikiwa kwenye utekelezaji wa miradi mnaipinga lakini mkitaka "kiki" za mitandaoni mnaanza kujifanya wataalamu wa bajeti na ufanisi wa miradi?
Ukweli ni kwamba Sekta ya Maji nchini inagusa maisha ya kila Mtanzania na ndio maana Serikali imekuwa ikiwekeza trilioni za fedha kusogeza huduma hii kwa wananchi.
Kukaa kwenye mitandao na kuanza kuuliza maswali ya kijumla jumla bila kuwa na takwimu au ushahidi rasmi bali kwa nia tu ya kutengeneza mashaka na taharuki kwa wananchi ni mbinu ya zamani sana ya kisiasa.
Huwezi ukawa hukubali uwepo wa nyumba halafu ukawa wa kwanza kupiga kelele kwamba paa la nyumba hiyo linavuja.