Furaha yako wakati mwingine inategemea na kutokujua taarifa au ukweli fulani. Kwepa kutafuta taarifa na kuujua ukweli ambao ama haukuhusu au moyo wako hauko tayari kuupokea na kuhimili. Huwezi kuumizwa na usilolijua
You are not meant to train a grown person to be empathetic. If you keep having to explain why your feelings matter, the issue is not your delivery, it is their capacity. Empathy is chosen, not forced.
Studying yourself is one of the most life-changing decisions you can make. When you learn why you react the way you do, what you're protecting, what you're repeating, you stop living on autopilot. Self-awareness becomes freedom.
Hakuna ujinga mtupu wala upumbavu mtupu. Hata wajinga na wapumbavu nao hufikiri isipokuwa mtiririko wa mawazo yao ndio wa tofauti na ule wa wenye akili. Ukifuatilia mtiririko wa mawazo yao kuna mawili matatu ya maana utayapata
Katika maisha yako tofautisha kati ya fadhila (priviledge) na haki (right). Haki ni stahili, fadhila ni tunu. Unaweza kuidai haki lakini huwezi kuidai fadhila. Epuka kuizoea fadhila, maana ikikuzoea itakugeuza Mfungwa wa Nadhiri
Usiyapime matatizo ya wenzako kwa mzani wako. Ulionalo dogo kwako ni kubwa kwa mwenzio na lile kubwa kwako dogo kwa mwingine. Yale yasiyo tatizo kwako ni kwa sababu yako ndani ya uwezo wako
Matarajio yako uliyoweka juu ya watu ndio mtego wa furaha yako na sababu ya kukosa kwako furaha. Usilolitarajia huwezi kulikosa wala haliwezi kukukosesha furaha. Usipokuwa na matarajio juu ya watu huangushwi wala huumizwi
Ahadi huamsha matarajio, humpa mtu subra, huchepusha dua na sala za watu, humbwetesha mtu asitafute mbadala. Ahadi unayotoa yaweza kukuinua ama kukubomoa mbele ya muahidiwa. Usiwe mwepesi wa kuahidi yasiyo ndani ya uwezo wako. Ahadi si tu ni deni, bali ni mtego wa heshima