@Mwabuk2Boniface Mhm Mwabukusi washauro Chadema waingie kwenye Maridhiano wasijifanye vichwa vigumu, mimi ni chadema Lakini na jua hizi cases zote tukienda mezani tunaweza kufikia muafaka mzuri, Wafungwa wachiliwe na Machakato wa katiba mpya iende haraka
@HildaNewton21 Mawakili wa Samia walikua hawana nia ya kuendelea na kesi wameamua kutumia mbinu ya kumnyima chakula ili kesi iahirishwe baada ya mahakama kuwakatalia mwanzo
Kesi ya Uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. @TunduALissu imepangwa kuendelea katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam tarehe 09 Februari 2026.
Kesho Jumatatu tujitokeze kwa wingi kupata darasa la sheria kutoka kwa Mhe. Lissu.
#FreeLissu
*TUNA WATU. TUNA MUSTAKABALI.*
Miaka thelathini na mitatu ya mapambano imetufundisha ukweli mmoja usiotetereka: nguvu ya mabadiliko haikai kwenye dola, wala haikai kwenye woga, inakaa kwa watu. Taifa linaweza kunyimwa haki, sauti zikazimwa, na matumaini yakajaribiwa kufifishwa, lakini watu wakibaki, mustakabali haupotei. Watu si watazamaji wa historia; wao ndio waandishi wake. Kila kizazi hubeba wajibu wa kuamua kama kitanyamaza au kitasimama, kama kitaacha hofu itawale au kitaipa tumaini nafasi ya kuongoza.
*“Tuna Watu”* si kauli ya hisia; ni tamko la nguvu ya kijamii, ya mshikamano, na ya uamuzi wa pamoja. Ni uthibitisho kwamba mabadiliko ya kweli huanza pale wananchi wanapotambua thamani yao na haki yao ya kuamua kesho yao. Na *“Tuna Mustakabali”* ni ahadi kwamba safari ya haki, usawa, na demokrasia haiishii leo, inaendelea kwa sababu watu wapo, wanaona, wanafikiria, na wako tayari kusonga mbele.
Hapo ndipo tumaini la taifa *linapokaa: mikononi mwa watu.*"
_John Heche, Makamu Mwenyekiti - Chadema(T)