@godbless_lema God! Acha chokochoko ndani ya Chama wakati sisi wananchi tunajivunia kwa kuupata upinzani wa kweli kupitia Mwenyekiti wetu mpendwa na Makamu wake. God "Tutakufatilia"๐ญ๐ญ
@Thommunkondya Ndani ya chama cha Mapinduzi kukiwa na sauti angalau kumi kama hizi hakika Taifa litatengamaa na kupaa kiuchumi pamoja na kuwa Siasa safi. Big up ndugu!!
@fbuyobe Mimi ninafollowz kiduchu lakini nimechagua kukupuza kwa kilichokuwa kinaendelea juu yako. Kuhusu huyu jamaa uliyemsaidia kwenye matatizo yake harafu anakuletea dharau kwakweli inabidi aende hospitalini akapimwe akili.
@MsigwaPeter Petro aliulizwa kuwa hata wewe u mmoja wao? Lakini Petro aligoma katakata ila kwa muonekano wa Petro ni Mgalilaya๐๐๐ Mch. Rudi tu nyumbani maana muonekano wako wewe ni mpinzani wa kweli
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuutarifu umma kuwa leo, tarehe 10 Aprili 2026, Makamu Mwenyekiti wa chama, Mheshimiwa John Heche, ameongoza jopo la viongozi wa chama katika kikao na ujumbe maalum wa Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Rais mstaafu wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera, ambao wapo nchini kwa ajili ya kufuatilia matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyoripotiwa kutokea tarehe 29 Oktoba, ambapo wananchi wengi walipoteza maisha.
Walioambatana na Mhe. @HecheJohn
ni Katibu Mkuu Mhe. @jjmnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara Mhe. @amanigolugwa, Mwanasheria Mkuu wa Chama Mhe. Rugemeleza Nshala, Mwenyekiti wa Bazecha Taifa Mhe. Susan Lyimo na rafiki wa Chadema Mhe. Jenerali Twaha Ulimwengu
Katika kikao hicho, Dkt. Chakwera amepokea taarifa ya msimamo wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, amepewa maelezo ya kina kuhusu matukio yaliyotokea kabla na baada ya tarehe 29 Oktoba, ikiwemo kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama, Mheshimiwa Tundu Lissu, pamoja na wimbi kubwa la utekaji, mauaji ya raia, na kuzuiwa kwa shughuli halali za kisiasa za chama.
Vilevile, Dkt. Chakwera amepokea ombi rasmi kutoka CHADEMA la kuruhusiwa kwenda kumuona Mheshimiwa Tundu Lissu akiwa gerezani, ili kujionea hali halisi na kupata taarifa za moja kwa moja.