Kaka, umenikumbusha mbali na kunitonesha kidonda kabisa! 😁
Mimi ni mmoja wa watu waliosoma PGM kwa makusudi kabisa kwa sababu ndoto yangu ilikuwa kuwa rubani. Nilipofika Form Six nilikuwa tayari nimejiandalia roadmap ya maisha. Nilijua wazazi wangu wasingeweza kumudu gharama za masomo ya urubani kwa sababu tulitoka kwenye familia ya kawaida, hivyo matumaini yangu yote niliyapeleka jeshini.
Nilikuwa naamini kwamba nikifaulu vizuri, JWTZ wangenichukua na kunipeleka Russia au China kusomea urubani wa ndege za kivita. 😁😁 Tena kichwani nilikuwa nimeshajiona narusha zile Sukhoi za Kirusi! 🤣
Lakini mambo hayakwenda kama nilivyotarajia. Kwanza sikuchaguliwa kujiunga na jeshi, jambo lililoniumiza sana. Kisha matokeo yakatoka nikapata D mbili. Kwa shule yetu, kati ya wanafunzi zaidi ya 100 wa sayansi, tuliokwenda degree kupitia PGM hatukuzidi watatu. Sasa wewe unaenda wapi na D mbili zako? 💔
Nakumbuka nililia sana. Nilijuta kusoma shule ya serikali, na hapo ndipo niliona ndoto yangu ya urubani inaanza kuzimika kabisa.
Baadaye nikaelezwa kuhusu kozi ya Aircraft Maintenance Engineering pale NIT. Nilipofuatilia nikakuta ada ni zaidi ya milioni 10. Nikamwambia baba. Alinicheka tu! 🤣🤣 Yaani hata kufikiria kuniambia “utaenda” ilikuwa ngumu.
Hapo ndipo nilijifunza kwamba kuna baadhi ya ndoto ambazo wazazi wako ndiyo wanatakiwa wakusaidie kuziota. Urubani ni mojawapo. Sisi watoto wa wavuja jasho kuna ndoto ambazo, licha ya kuambiwa “the sky is the limit,” mazingira yanafanya zionekane kama si za kuota kabisa.
Lakini Alhamdulillah, maisha yana njia zake. Chuo UDSM nilisoma kozi zinazohusiana na jiografia, nikafundishwa kutumia na kurusha drone kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa za kijiografia kupitia picha za anga (drone surveying).
Kwa hiyo, kwa namna fulani, ndoto haikufa kabisa… 😄
Sikuwa rubani wa Sukhoi, lakini leo ni rubani wa drone. 🤣🤣
Give a man free sex, entertainment, and comfort, and he’ll forget his goals.
Give him pain and heartbreak, and he’ll feel like conquering the world.
Dear bro, hard times are a blessing, not a curse.
Dear God,
Thank You for the precious gift of life. As we begin this day, we acknowledge that You are our strength, our wisdom, and our peace.
Father, go before us today. Order our steps, guide our decisions, and align our plans with Your will. Bless the work of our hands and let our efforts bear good fruit. Give us clarity where there is confusion, courage where there is fear, and discipline in all we do.
Protect us and our loved ones, keep us in good health, and surround us with Your favor. Let this day be filled with progress, breakthroughs, and opportunities that draw us closer to the purpose You have for us.
May everything we do today bring glory to Your name and reflect Your goodness. We declare that our work is blessed, our decisions are sound, and our steps are ordered by You. Through Your grace, we shall overcome every challenge and grow in strength, wisdom, and faith.
In Jesus’ name we pray
Niwape story nyingine ya Nabii AYUBU? 😂
Ukisoma Biblia AYUBU 1:1, Biblia inasema Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyoofu. 😎
Unajua kuwa mnyoofu wewe! Mungu alikuwa proud naye sana. Lakini kulikuwa wanoko 😂 wakasema, Mungu huyu unamuona yuko hivyo kwa sababu umempa kila kitu.
Chukua hivyo vitu vyake uone kama bado atakuwa mwaminifu kama unavyosema, Mungu akaona isiwe kesi ngoja tuone
Ghafla utajiri ukaondoka, mali zikapotea, watoto wakafa, na Ayubu akapata maradhi makali ya mwili.
Halafu wale wale Ma snitch wakaanza kusema, Hapana, lazima huyu kuna dhambi kubwa amefanya, Lakini pamoja na yote hayo, Ayubu aliendelea kushikilia imani yake.
Ndipo katika AYUBU 1:21 tunapata maneno haya
“Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana libarikiwe.” 🙏🏾
Guess what 😂 Baada ya kipindi chote cha mateso na maumivu, Mungu alimrudishia Ayubu kila kitu, tena zaidi ya alichokuwa nacho mwanzo. Hapo ni AYUBU 42:10.
Wakati mwingine hali ngumu tunazopitia kwenye maisha yetu si kwa sababu tunastahili, hapana. Wakati mwingine ni kwa ajili ya kutujenga, kutufundisha, na kutuandaa kwa kile kinachokuja mbele yetu.
Usikate tamaa katikati ya story yako. Mungu bado hajaandika mwisho wake. ☺️
Nisikie Amen kutoka huku nyuma.
Jambo gumu ambalo nimekubaliana nalo ni kua nchi zetu hizi kufikia Dunia ya kwanza labda Mungu aingilie kati.
Hamuwezi kua mnazalisha Nyambizi, ndege za kivita, mitambo mizito, satellites au robots mkawa mnasumbuana na jezi za vyama haiwezekani.
Inauma sana ila kweli
Nine months. Not because it took that long to build, but because we refused to launch until it was built for the long term.
Today we are proud to announce the V3 of the @SerengetiBytes website, the third version in seven years of existence. We built our first in 2018. Our second in 2022. This one is for the next chapter.
It is available in seven languages: English, Kiswahili, Chinese, Russian, French, Spanish, and Arabic, and across four country domains: https://t.co/KhdN3TVhZi, https://t.co/WRaigrvc4C, https://t.co/d7BqbwFIsR, and https://t.co/bljOorULGI, with the Burundi version coming in Q3 2026.
We are also expanding our portfolio of services and products, and this website is the beginning of that story becoming visible.
We build slowly. We build deliberately. And when we ship, it is because we are ready.
MITI INAUZWA 🌲
Kuna Ekari 100 za miti ya Mpaina (pine) zinauzwa. Mmiliki anataka msitu wote uchukuliwe kwa pamoja. Tangu kupandwa ina miaka 20.
Eneo- LUDEWA (Njombe)
#BEI - 100M
Ukaguzi wa msitu unahitaji zaidi ya saa 5. Kumbuka kuweka posho yangu
Call/WhatsApp 0719542184
Nathibitisha
Katika hii June, nitatembea katika neema ya Mungu na baraka zisizo za kawaida.
Kila fursa iliyokusudiwa kwangu inanipata.
Kipato changu kinaongezeka kwa kasi na nitapata faida kila kona.
Mimi na familia yangu tuna afya njema, amani, ulinzi na mwongozo wa Kimungu.
This is the real truth, but our leaders lack very important thing. They lack intelligence & integrity. We have to be strategic to win a against world elite. Tubadilishe sera na mentality ya wananchi, we can win them ila hizi porojo za wanatuonea wivu and so so....👐👐👐
This needs months-long conversations.
But nataka kusema utajiri au umasikini siyo hali ya bahati mbaya katika ngazi ya nchi na ya mtu binafsi. Mwananchi au nchi kama Tanzania kuwa masikini siyo kwasababu ni sisi wenyewe kama taifa tuna makosa, bali kuna makusudio ya nje pia.
Ukweli ni kuwa tukichagua viongozi wetu huwa HAWATUAMBII UKWELI wote kwamba ni kwanini nchi inaendelea kubaki masikini. Wamechagua kutunza dignity yao, kuwa hata wao wana ma-boss wao pia, na katika hiyo occult ya umasikini na utajiri, inaweza kuwaondoa madarakani kama wakiokoka. Na muhimu ni kuwa, wakiamua kupursue mambo yatakayoleta maendeleo, nao watageuka kuwa wanaharakati, ambao watapingwa na wananchi wao wenyewe (sisi) na global interests.
Umasikini ni man-made, na una internal na external factors zake. We should be honest about this first
Moja ya kitu kinaninyima usingizi recently ni hili swala la wanaharakati kuwa wanalipwa!! (Kama ni kweli)🤔
Hizo taasisi au watu binafsi wanaolipa wanaharakati, huwa wanatazama vigezo gani kukulipa?
Influence? au Numbers (Followers)
au uwezo wa kuongea na kuandika au engagement ya social media au nini?
Binafsi nimeanza hii course ya harakati tokea siku namaliza form six na kutoa wimbo wangu wa kwanza Tanzania (2007) nikiwa very young!
Hadi leo nina Teremsha bunduki 2026!
Miaka 19 kwenye hizi harakati
NA SIJAWAHI KUPEWA HATA SHING 10 TOKA KWENYE HIZO TAASISI!!
WALA KULIPWA NA MTU BINAFSI ILI NIFANYE HIKI NINACHOKIFANYA!!
Na kuna muda unakuwa na uhitaji haswa, tena sometimes ni uhitaji wa kufanya projects hizi hizi za kusaidia hizi harakati….. you just end up using your own pocket money!!
Kwenye hizi harakati nakutana na challenge nyingi, nakosa opportunities na michongo kwasababu naonekana niko against na gavoo na kuna muda napoteza hata kidogo nilichobakiza!!
Nabaki empty hadi familia inakwambia si utemane na hizo mbanga……nawajibu I WAS BORN TO DO THIS!!
Ni kama roho/nafsi inakataa ku-give up!!
Tunafanya haya kwa passion,
kuna a driving force tu inatusukuma kutetea, kukemea, kushauri na kupaza sauti tunapoona haki inakosekana, maendeleo hakuna, rushwa na ufisadi kwa viongozi vinakithiri, umasikini unazidi kwetu sisi raia, uongozi na utawala mbovu, shida za ajira na miundo mbinu, watu kutekwa, kufungwa na kuuliwa bila hatia na kucreate awareness kwa raia kuhusu issue za kisiasa na kijamii etc.
Nikisikia mtu anasema kuyafanya hayo ni unalipwa…..nawaza nakosa majibu!!
Wanatumia vigezo gani kukulipa?
Hebu mtu anieleweshe pengine napishanaga na gari la mshahara!!
Followers ninao (1.3M) influence pia si haba nikitoa miwa inapokelewa mtaani!! MBONA MIMI SILIPWI?
Nways tusiache hizi harakati hata kama hazitupi pesa kwa sasa, faida yake mbeleni ni kubwa zaidi kwa nchi nzima na vizazi vijavyo!!
Kama nimeandika kwa hisia sana ee?😁
Kwakuwa tuko duniani;
Na kwakuwa kuna haki ya asili, haki ya Mungu na haki ya duniani;
Na kwakuwa, kwa wengine, kisasi ni haki;
Na kwakuwa hakuna lililo au litakalofanyika hapa duniani likafichika kamwe;
Hivyo, basi, tunaitazamia haki na aibu ya watesi wetu kwa shauku kuu!
Bwana…
Nimechoka.
Nimechoka kutumaini.
Nimechoka kusubiri.
Nimechoka kutoelewa.
Kuna siku nakuamini.
Kuna siku sielewi ni vipi hasa.
Ila, bado niko hapa.
Baki nami katika hili...
hata kama sina nguvu ya kusema mengi zaidi.
Amina.
Falsafa moja ambayo nimejifunza na kuiamini ni hii: survival hutegemea uwazi wa msimamo.
Ni salama zaidi kusimama wazi kwenye jambo unaloamini kuliko kubaki katikati ya watu ambao hawakuamini wala hawashiriki misingi yako ya fikra. Ambiguity inaweza kuonekana kama fikra ya kimkakati ila mara nyingi huwa ni ukweli uliocheleweshwa tu.
Siku moja, msimamo uliokataa kuuchukua utachukuliwa na mtu mwingine kwa niaba yako. Na simulizi itakayobaki haitakuwa yako. Itandikwa na wengine.
Watu wengi niliowahi kuwaheshimu maishani hawakuwa sahihi kila wakati. Hapana. Lakini walikuwa watu wenye mahali pao. Watu ambao unajua wanasimama wapi na kwa nini. Hiyo ni sifa adimu sana katika dunia ya watu wanaotaka kupendwa na kila upande kwa wakati mmoja.
Chagua upande wako.
Simama kwenye upande wako kwa uwazi.
Neutrality si eneo salama la msimamo. Mara nyingi ni eneo ambalo kila upande huanza kukuona kama mtu asiyeaminika.
Mtu asiye na msimamo huandikiwa historia na wengine.
KANUNI mojawapo ya Ufalme wa Mungu inasema hivi:
Mtu yeyote aliyemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake, HALAANIKI. This is liberating.
Uwe na asubuhi njema.
Acha kujipa mawazo juu ya kile kinachofuata. Mungu tayari ameshughulikia. Kazi yako si kujua kila kitu; kuwa mwaminifu hapo ulipo. Jukumu unalofanya sasa linakutayarisha kwa linalofuata. Mungu anafanya kazi nyuma ya pazia, huku akipanga maelezo na namna ya kufungua milango.