Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri, tarehe 5 Machi, 2026 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anazindua Makao Makuu ya ulinzi na usalama, Kikombo jijini Dar es Salaam.
"Ile asilimia kumi katika mikopo ya Halmashauri kwaajili ya vijana, wanawake na wenye ulemavu iongezwe na kufikia asilimia 15, ambapo asilimia 5 ni kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya kufanyia biashara vijana wetu" Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Tanzania na Uganda zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa biashara na miundombinu, ikiwemo matumizi ya bandari za Tanzania, upanuzi wa reli ya SGR hadi Lusahunga na mpango wa reli Tanga–Musoma ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kukuza uchumi wa Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofauti ya picha alipompokea Mgeni wake, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Viwanja vya Ikulu ya Dar es salaam kwa ziara ya siku Moja leo February 07,2026.
Rais Samia Suluhu amehudhuria uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) Dubai na kuwahakikishia wawekezaji uaminifu, uthabiti wa sera, na fursa endelevu.
Tanzania imewekeza kimkakati: nishati, reli, bandari, Maeneo Maalum ya Uwekezaji na Dirisha Moja la Uwekezaji.
Rais Samia amekutana na Katibu Mkuu wa UN Tourism, Shaikha Nasser Al Nowais, Dubai
Wajadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa utalii Tanzania kukuza miradi endelevu, kuongeza thamani ya rasilimali za utalii na kuendeleza ajira na utamaduni wa taifa#Tanzania #UNTourism#WGS2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt. Samia Suluhu Hassan aliposhiriki Sherehe za Mwaka Mpya na Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa (Diplomatic Sherry Party), hafla iliofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo January 15, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mh. George Simbachawene (Mb) kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na nafasi yake inachukuliwa na Mh. Patrobas Katambi (Mb).
“NI WAKATI WA KUTAMBUA MAKUNDI YA WANANCHI WA CHINI” – MATWEBE
Matwebe amesema uwezeshaji wa bodaboda, wamachinga na mama lishe utapunguza migogoro, kuongeza ajira na kuimarisha uchumi wa taifa kwa ujumla.
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amekagua hali ya uzalishaji na usambazaji wa maji Ruvu Chini, mkoani Pwani, Desemba 29, 2025. Amesema miradi ya kukabiliana na upungufu wa maji imeanza kutekelezwa kwa miaka 3 iliyopita. #Maji#Serikali
TUNASHUKURU VYOMBO VYA USALAMA KWA KILICHOTOKEA DISEMBA 09
“Mashukrani kwa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama. Matarajio ya watu kuhusu Disemba 9 yalikwenda tofauti, na hilo limewezekana kwa uthabiti wao. Tunawashukuru Serikali kwa ulinzi.”Amina Eli, Mkazi wa Dar es Salaam
Waimbaji wa nyimbo za Injili wathibitisha imani yao kwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia wimbo “Tuna Imani na Wewe”, wakionesha mshikamano, uzalendo na dhamira ya kuijenga Tanzania yenye umoja na maendeleo 🇹🇿
#UmojaNiNguvu#AmaniNaMaendeleo#TanzaniaYetU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Desemba, 2025.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na Balozi wa Kenya anayemaliza muda wake, Mhe. Isaac Njenga, Ikulu Dar es Salaam, kujadili kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya.
#Tanzania#Kenya#Uwekezaji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefungua rasmi Mkutano wa 9 wa CDF na Makamanda uliofanyika SKUA, Tanga, tarehe 15 Desemba 2025.
#CDF#JWTZ#SKUA#Tanga#UsalamaWaTaifa#SamiaSuluhu
GUTERRES: TANZANIA PASSES THE ELECTION TEST
The UN Secretary General has stated that despite incidents of violence during the 2025 General Election, Tanzania succeeded in maintaining national unity and peace.
#Election2025#Peace#SamiaSuluhu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Ivan Lancaric, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 11 Desemba 2025.
RAIS SAMIA AWASAMEHE WAFUNGWA 1,036.
Msamaha huu wa Disemba 9 unaendelea kuwa utamaduni wa kila mwaka. Wafungwa 22 waachiwa huru, 1,014 wapunguziwa adhabu. Serikali yatoa wito wajikite kwenye maisha mapya na kuchangia maendeleo.
MANGE NA CHADEMA WALIPANGA KUCHOMA MOTO NCHI SI MAANDAMANO.
Dkt. Nyamatari Mtengecha asema walipelekwa Nairobi kupata mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kuharibu amani. Alitoa kauli hii mbele ya Watanzania na Rais Samia.
@meta@swedenintz#AmericanEmbassyTanzania