Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 27 Agosti, 2025.
1. Haki na Wajibu wa Kisiasa kwa Mujibu wa Katiba
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa) inatambua na kulinda:
Haki ya kushiriki shughuli za kisiasa (Ibara ya 20 na 21), ikiwemo kujiunga na chama cha siasa na kushiriki mikutano ya kampeni.
Uhuru wa mawazo na kujieleza (Ibara ya 18), ambao hujidhihirisha kwenye mikusanyiko ya hadhara kama hii.
Kwa hiyo, wingi wa watu waliokusanyika Kawe ni kielelezo cha haki ya wananchi kushiriki kidemokrasia, mradi tu shughuli hizi zinafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu.
2. Sheria za Uchaguzi na Kanuni za Kampeni
Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani (Sura ya 343) na Kanuni zake, pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zinaweka misingi ya kampeni:
Kampeni lazima zifanyike katika mazingira ya amani na usalama.
Vyama vyote vinapaswa kupewa nafasi sawa ya kufanya kampeni.
Viongozi na wagombea wanakatazwa kutumia lugha za chuki au kuchochea uvunjifu wa amani.
Kwa kuwa umati mkubwa umejitokeza, jukumu la vyombo vya dola na NEC ni kuhakikisha kuwa mikutano inabaki kwenye mstari wa amani na heshima kwa sheria.
3. Uwepo wa Viongozi wa Kitaifa na Wastaafu
Uwepo wa viongozi wa kitaifa na wastaafu una uzito mkubwa:
Kiishara, unaonyesha mshikamano wa kitaifa na mwendelezo wa uongozi.
Kidemokrasia, unathibitisha kwamba hata viongozi wastaafu wanashiriki na kutunza hadhi ya mchakato wa kisiasa.
Pia unatoa taswira ya umoja na mshikamano ndani ya chama na taifa, kinyume na migawanyiko ya kisiasa.
4. Mustakabali wa Taifa
Hali ya amani na utulivu iliyotajwa hadi sasa ni msingi wa mustakabali wa taifa:
Ikiendelea kudumishwa, itahakikisha uchaguzi huru na wa haki.
Wingi wa wananchi wanaojitokeza ni ishara ya imani kwa mchakato wa kidemokrasia, lakini pia changamoto ya kuhakikisha kila upande unapata fursa sawa.
Kwa taifa changa na lenye historia ya mshikamano, mustakabali wake hutegemea kuheshimu demokrasia, kutii sheria, na kudumisha mshikikano wa kijamii.
Kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Uchaguzi, mkusanyiko wa maelfu ya wanachama wa CCM Kawe ni tukio la kawaida la kisiasa, linaloonyesha haki ya kikatiba ya kushiriki katika shughuli za kisiasa. Uwepo wa viongozi wote – wa sasa na wastaafu – unaleta uzito wa kitaifa na kuimarisha mshikamano. Mustakabali wa taifa utategemea zaidi namna vyama vyote, viongozi na wananchi wanavyoshiriki kwa heshima, amani na kufuata sheria kuelekea Uchaguzi wa 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima (kulia) ameongoza watumishi wa Tume kuondoa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ubao wa matangazo wa Tume ikiwa zimepita saa 24 za kubandikwa fomu hizo ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria. Fomu hizo za wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilibandikwa ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Fomu hizo zilibandikwa na Tume Saa 10:00 jioni ya Agosti 27, 2025 ambayo ilikuwa ni siku ya uteuzi na kuondolewa leo Agosti 28, 2025 Saa 10: 00 jioni.
The Vice President of the Republic of Zimbabwe, H.E. Retired Colonel Kembo Campbell Mohadi arrived in Tanzania on August 30, 2025, for a two-day working visit ending on August 31, 2025. The visit was made at the invitation of the Vice President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Philip Isdor Mpango.
Upon arrival at Julius Nyerere International Airport, Vice President Mohadi was warmly received by the Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Honorable Cosato Chumi, along with other senior government officials.
During his visit, Vice President Mohadi will hold official talks with his host, H.E. Dr. Philip Isdor Mpango, at the State House in Dar es Salaam, followed by a press briefing.
In addition, Vice President Mohadi will visit the Mwalimu Julius Nyerere Leadership School in Kibaha, the College of Agriculture and Livestock in Kaole, Bagamoyo, and the African Liberation Heritage Centre in Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar.
Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
#KurayakoHakiyakoJitokezeKupigaKura
#oktoba2025
#tumehuruyataifayauchaguzi
#uchaguzi2025
#UchaguziMkuu
#uchaguzi
📍Dodoma.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 31 Agosti, 2025 imekaa na kujadili rufaa kuhusu uteuzi wa wagombea Ubunge katika Jamhuri ya Muungano na Udiwani kwa Tanzania Bara zilizowasilishwa Tume kwa ajili ya uamuzi.
Wanasayansi wanawake wawili – Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria – wametangazwa washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025).
Tuzo hiyo, yenye thamani ya Dola za Marekani 100,000, ilikabidhiwa na Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika.
Hafla ya kukabidhi tuzo ilifanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.
Katika hotuba yake, Dkt. Kikwete aliwapongeza washindi kwa mchango wao wa kipekee katika tafiti zinazolenga kuongeza tija ya uzalishaji na kuboresha maisha ya wakulima wadogo barani Afrika.
“Tuzo hii inadhihirisha nafasi kubwa ya wanasayansi wa Afrika katika kutafuta suluhu za changamoto za kilimo. Ingawa mwaka huu imeenda kwa washindi wawili, tunatambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa na watu binafsi na taasisi nyingi ili kuhakikisha bara letu linakuwa na mifumo imara na endelevu ya chakula,” alisema Dkt. Kikwete.
Profesa Abukutsa-Onyango amejikita katika tafiti za mboga mboga za asili za Kiafrika kama mchicha, sukuma wiki, mgagani, mchunga, figiri na kisamvu, akihamasisha uzalishaji na ulaji wake kwa madhumuni ya kuimarisha lishe.
Kwa upande wake, Mercy Diebiru-Ojo anasifika kwa kubuni na kuendeleza teknolojia ya kisasa ya uzalishaji na upandikizaji wa mbegu za mihogo kwa kutumia mbinu ya semi-autotrophic hydroponic technology, ambayo imeongeza mavuno na tija katika kilimo hicho muhimu barani Afrika.
Tuzo ya Chakula Barani Afrika ilianzishwa mwaka 2005 chini ya mwamvuli wa mpango wa Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA). Inatolewa kila mwaka kwa watu binafsi au taasisi zinazotoa mchango wa kipekee katika kuimarisha mifumo ya chakula na maendeleo ya sekta ya kilimo.
Kwa mwaka huu 2025, jumla ya maombi 601 kutoka ndani na nje ya Afrika yaliwasilishwa kuwania heshima hii kubwa.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imezitaka taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi na weledi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 08 Septemba, 2025 wakati akifungua kikao kazi cha Tume na taasisi na asasi hizo kilichofanyika Mkoani Dodoma.
"Ni vyema mkafahamu kuwa kifungu cha 10(1)(g) na (h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024 na kanuni ya 22 na 23 ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, zimeipa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi mamlaka ya kutoa elimu ya mpiga kura nchini, kuratibu na kusimamia taasisi na asasi zinazotoa elimu hiyo..
Hivyo, kazi mnayoenda kuifanya ni moja ya majukumu ya kisheria ya Tume na mnapaswa kuifanya kwa weledi na ufanisi mkubwa,” amesema.
Ndugu Kailima ameongeza kuwa, Tume inatarajia kuona kuwa, taasisi na asasi za kiraia zinatoa elimu iliyolengwa haswa kwa kutoa kipaumbele kwenye mambo ambayo yatawapa wananchi, wagombea na vyama vya siasa kwa ujumla uelewa wa namna ya kushiriki kwenye kampeni kwa amani na utulivu ikiwa ni pamoja na kupata uelewa mzuri wa utaratibu wa kupiga kura.
"Hatutarajii kabisa mtoe elimu ambayo italeta mkanganyiko kwenye jamii na kuiingiza nchi kwenye machafuko kama ilivyotokea katika maeneo mengine hapa Afrika na duniani kwa ujumla," amesema.
Amesisitiza kuwa taasisi na asasi hizo haziruhusiwi kuwapa watu wengine au taaisi au asasi nyingine vibali walivyopewa na kwamba vibali hivyo ni lazima vitumiwe na walengwa tu.