VIJANA WA KITANZANIA TUSIKUBALI NCHI ICHAFULIWE NA KUUZWA KWA WATU TUSIOWAJUA.
Tukatae haya Maandamano kwa Nguvu zote, Nchi yetu inataka kuingiliwa na watu tusiowajua na kutuletea machafuko.
Hatuna Nchi Mbadala ya Tanzania!
(Day 60/60 ya kampeni za CCM)
DKT. SAMIA AKIHITIMISHA MBIO ZA KAMPENI TANZANIA BARA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa CCM Kirumba-Mwanza kuhitimisha mikutano ya hadhara ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025.
#KigogoMediaUpdates
(Day 46/60 ya kampeni za CCM)
KAYANGA-KARAGWE LEO
Mgombea urais wa CCM Dokta Samia Suluhu akiwasili kwenye mkutano Kayanga- Karagwe kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025
#KigogoMediaUpdates
Siku kubwa, ya kihistoria na ya baraka za Mwenyezi Mungu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na nchi yetu, ambapo nimeungana na Mgombea Mwenza, Ndugu Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuzindua rasmi kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Hatua hii ni mwanzo wa safari yetu ya kwenda kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuendelea kuwatumikia.
Tunatoka kwenda kwa wananchi kwa sababu kuu mbili; Moja, tumetekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya CCM 2020 hadi 2025 ikiwemo kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Pili, CCM kwa umadhubuti, kuaminika kwake, utendaji wake na historia yake ni nguzo muhimu kwa utumishi na mustakabali wa Taifa letu.
Tumejipanga kuongeza nguvu na kazi katika kuihudumia nchi yetu na watu wake ambapo, katika Siku 100 za Kwanza, kipaumbele kitakuwa kwenye sekta za afya, elimu, ajira, nishati, maji na biashara tukilenga matokeo yenye kuboresha ustawi wa wananchi, hasa wenye kipato cha chini.
Niwatake wagombea na viongozi wote wa CCM, twende kwa wananchi tuwaeleze tuliyofanya na tutakayofanya. Wananchi wengi wana imani na CCM katika ustawi na mustakabali wa nchi yetu. Nguvu na ustawi wa Taifa letu viko kwenye umoja wetu, amani yetu na mshikamano wetu chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ikiwa Tundu Lissu anaendelea na Ziara katika mikoa ya Kusini,Leo yuko Mkoa wa Ruvuma Mbambabay na video hapo chini ni Wananchi waliofika kusikiliza sera zake.
Idadi ya watu imeendelea kudhorota kila siku kwenye mikutano yake ijapokuwa alionekana kuwa na mvuto kwa watu huko nyuma.
Ikiwa ni muendelezo wa Ziara ya CDM Tunduma Muitikio wa Wananchi umekuwa mdogo kwenye Mikutano hali inayoleta simazi na hofu katika Mwaka huu wa Uchaguzi.
Pichani ni Mkutano uliofanyika leo shule ya Sekondari Nyerere iliyopo Tunduma Mjini!
Kuwataka wahariri na waandishi wa habari kusitisha ushirikiano na CHADEMA katika kuripoti habari za chama hicho hadi pale watakapotoa tamko rasmi la kuomba radhi.
Kuwakumbusha wanasiasa na viongozi wa umma kuheshimu vyombo vya habari kama sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa
Katika tamko lake, TEF imesema kauli ya Mhe. Lissu inaonyesha mtazamo wa dharau kwa vyombo vya habari na inaendeleza tabia ya kutoheshimu mchango wa tasnia hiyo katika kukuza demokrasia na maendeleo ya nchi.
Kutokana na hali hiyo, TEF imechukua msimamo ufuatao:..
Jukwaa la Wahariri Tanzania limepokea kwa masikitiko makubwa kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Lissu, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Sumbawanga, mkoani Rukwa. Katika mkutano huo, Mhe. Lissu aliwatuhumu wahariri na waandishi wa habari kuwa hawana akili..
Mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeanza katika uwanja wa Shule ya Msingi Ndui, Sumbawanga Mjini, lakini kwa muitikio mdogo wa wananchi. Hadi sasa, idadi ya waliohudhuria inaonekana kuwa ndogo, huku tukio likiendelea. Je shida ni nini?
Sumbawanga โ Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wasitisha masomo ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndui, Sumbawanga Mjini, baada ya kutumia uwanja wa shule hiyo kwa mkutano wa hadhara.
......hali iliyosababisha walinzi wa Heche kuchukua hatua za mabavu dhidi ya Siglad. Haijafahamika bado chanzo halisi cha mvutano huo, lakini tukio hilo limezua taharuki miongoni mwa wanachama wa CHADEMA waliokuwepo katika kikao hicho.
Mwenezi wa (BAWACHA) Taifa, Siglad, amepigwa na walinzi wa Mbunge wa zamani wa Tarime Vijijini, John Heche, katika kikao cha ndani kilichofanyika usiku wa jana mkoani Njombe.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema vurugu hizo zilianza baada ya mvutano uliozuka ndani ya kikao hicho,
Vita kati ya timu Lissu na timu Mbowe ndani ya Chadema bado inaendelea hata baada ya uchaguzi na taarifa za ndani zinasema wafuasi wa Mbowe wamesusia chama chao kutokana na kutokukubali uongozi mpya wa chama na hiyo ndiyo sababu hawaonyeshi ushirikiano kwenye shughuli za chama.