#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 329
Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania?
Mnyika: Ni sahihi.
Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo?
Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu.
Job Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya Tarehe 18 na 19 August 2026?
Mnyika: Hizo Habari nazisikia kutoka kwako.
Job Mrema: Ikitokea wanachama wa Chadema wamepata ushahidi wakasema kuna pesa zimetoka huoni kiti chako kitakuwa rehani?
Mnyika: Tutasubiri kuona kama kuna aliyeidhinisha pesa kutoka ni nani na kwa sababu gani?
Job Mrema: Kutoa pesa za Tonetone kwa mujibu wa ibara ya 4.1.2 ni kuwaonea?
Mnyika: Anaisoma hiyo ibara. Inasema kukandamiza watu kwa rangi, dini
Job Mrema: Ndio maana wengine hamkuwalipa?
Mnyika: Mimi Katibu Mkuu ndio ninayejua kwamba kwa hali tuliyonayo. Alipwe Mlinzi pekee. Kwasababu yeye yuko ofisini kila siku na sio mfanyakazi mwingine. Wewe unajua nini kuhusu haya mambo kuliko mimi?
Job Mrema: Ibara ya 3.2.4 inasema kama inavyosema hapo?
Mnyika: anaisoma na kusema inasema hivyo.
Job Mrema: Sasa kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi unasemaje kuhusu hilo?
Mnyika: Sisi hatuna Ubaguzi wenye ubaguzi ni nyie Serikali ambao mmezuia fedha za Chadema. Ndio maana Chadema tunapambana fedha za umma zibaki salama.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa ukiaminika kwa dogo utaaminika kwa kubwa?
Mnyika: Chadema inaaminika kwa dogo na kwa kubwa pia. Ndio maana watanzania wameendelea kuiunga mkono.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 325
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea na maswali yake ya Kiwaki ila Mnyika anaendelea kumshona bila ganzi.
Katuga: Soma maana ya Kamusi hapa?
Mnyika: Ulipofungua hakuna maana ya Demokrasia labda fungua sehemu husika.
Katuga: Huwezi kufungua?
Mnyika: Demokrasia ni mfumo wa utawala ambao unapatikana kwa matakwa ya umma.
Katuga: Hiyo maana na ile yakwako vinafanana?
Mnyika: Vinakaribiana.
Katuga: Ni kweli kwamba Demokrasia inahusiana na utawala?
Mnyika: Inahusiana na mamlaka ya wananchi pia.
Katuga: Kama Katibu Mkuu Kuzuia uchaguzi kwa njia ya Demokrasia ukimzuia ni demokrasia kwa tafsiri hiyo? Hayo mamlaka uliyapata lini?
Mnyika: Sina hayo mamlaka Katibu Mkuu
Katuga: Mwenyekiti wako amepata mamlaka wapi ya kuzuia uchaguzi kidemokrasia?
Mnyika: Alipata kutoka kwa azimio la Chama la Mkutano Mkutano la Tar. 21/01/2025.
Katuga: Mkutano Mkuu wa Chadema una watu wangapi?
Mnyika: 1000 na zaidi.
Katuga: Hao watu elfu moja ni asilimia ngapi ya watanzania?
Mnyika: Huo ni mkutano wa uwakilishi kutoka maeneo mengin, ukisema asilimia labda uwe hujielewi.
Katuga: Nimemaliza naomba waendelee wengine.
Ajuaye: Amesimama Cathbert Mbiringe.
Cathbert: Chama chenu ni cha ukweli na uwazi?
Mnyika: Ndio
Cathbert: Wewe ni accounting officer?
Mnyika: Ndio
Cathbert: Ni kweli mnakusanya tonetone?
Mnyika: Ni kweli
Cathbert: Na mmeshatoa takwimu za tonetone la Baraza Kuu la Umma.
Mnyika: Milioni 302 hadi mara ya mwisho.
Cathbert: Unafahamu au hufahamu kuna milioni 100 nyingine ilichangwa?
Mnyika: Sifahamu.
Cathbert: Mara ya mwisho mmelipa watumishi wa Chama lini?
Mnyika: Mwezi uliopita.
Cathbert: Ikitokea kuna ushahidi kuwa hujalipa mishahara toka mwaka uliopita nani atakuwa muongo?
Mnyika: Wote watakuwa wakweli huwezi kukifungia chama siku 309 halafu ukazuia ruzuku ukategemea wafanyakazi walipwe. Nilichosema ni mara ya mwisho tumewalipa mwezi uliopita hizo posho zao lakini kuna madeni mengine. Mbona linaeleweka.
Cathbert: Viongozi wakuu wa Chama ni akina nani?
Mnyika: Lissu, Heche, Said Mzee, Mnyika, Amani Golugwa, Ali Ibrahim Juma. Hapo ni kuanzia Mwenyekiti hadi Naibu Katibu Mkuu wote wawili.
Cathbert: Ukiachana na Mwenyekiti na wewe kuna mwingine yoyote ambae hadai Posho?
Mnyika: Hata mimi nadai posho.
Cathbert: Kwanini hujatumia tonetone kulipa mishahara?
Mnyika: Tonetone inahusika na shughuli maalumu huwezi kutoa kwa mfano pesa za Baraza Kuu kwenda kulipa mishahara.
Cathbert: Huoni fedha hizo zitatumika kwenye utakatishaji wa fedha?
Mnyika: Mamlaka zipo na hela zetu zinapitia kwenye account zinazojulikana kwahiyo kama kuna shida maana yake hatua zichukuliwe. Huwa tunaweka account hadharani na hatuulizi watu kwamba hizo pesa mmezipata wapi?
Cathbert: Hizo pesa mnalipa kwenye account zao au vipi?
Mnyika: Kwa kutumia account zao huwa tunalipa.
Cathbert: Nimemaliza.
Anasimama Ajuaye sasa.
Ajuaye: Ulisema uasi ni nini?
Mnyika: Ni kupinga na kukataa jambo kwa nguvu kubwa kupitia njia za kidemokrasia.
Ajuaye: soma maana ya uasi kwenye Kamusi.
Mnyika: anaisoma. Anasema Mwalimu Nyerere alitumia neno uasi kwasababu lina maana pia kwenye siasa ndio maana halijawahi kuwa kosa.
Ajuaye: Kamusi ya siasa iko wapi?
Mnyika: Hatuna kamusi ni matumizi ya maneno ambayo ipo kwenye siasa.
Ajuaye: Wakati mnapanga kuhamasisha uasi mlipanga kukiuka sheria na kuvunja sheria kwa mujibu wa kamusi hii?
Mnyika: Wakati tunapanga No Reforms: No Election hatukutumia Kamusi. Na hatukupanga uhalifu wowote.
Ajuaye: Kwahiyo unapingana Kamusi hii?
Mnyika: Hiyo kamusi sio nyaraka yenye maneno yote ya Kiswahili na maana zote. Ndio maana zinarekebishwa na maneno yanaongezwa na kupunguzwa pengine.
Hii inaitwa Ajuaye Hajui. 😂😂
Part 326 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 324
Baada ya Break, Mahakama imerejea.
Tunaendelea sasa.
Anasimama Ajuaye anasema tunataka kuendelea.
Jaji Ndunguru anamwambia John Mnyika nakukumbusha uko chini ya kiapo tuendelee sasa.
Katuga: Iambie Mahakama hii uwepo wa Kesi ya Khatib Gandi?
Mnyika: niliwahi kusikia.
Katuga: Kwenye uamuzi wake kesi sio mpira wa miguu inayohitaji Ushabiki?
Mnyika: Sijawahi kusikia.
Katuga: Kesi ya jinai sio hisia na ushabiki?
Mnyika: Najua
Katuga: Kuwa Katibu Mkuu ni muhusika wa kujua idadi au majina ya Chadema?
Mnyika: Sihusiki moja kwa moja. Wapo wasaidizi.
Katuga: Kazi ya kujua idadi ya wanachama ipo kwa nani?
Mnyika: Katibu Mkuu na Kamati Kuu.
Katuga: Kuna malalamiko mitandaoni kuhusu posho za Chama unafahamu?
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Unafahamu kuna mwanachama aliyeitisha waandishi wa habari kutangaza kilichopangwa kufanywa Oktoba 2025?
Mnyika: Sifahamu. Mwanachama yupi huyo unayemzungumzia.
Katuga: Unafahamu mwanachadema huyu kwenye taarifa yake kwa umma kuwa kulikuwa na mifumo maalumu ya kuwasiliana ili kutekeleza nia ya kuvuruga Uchaguzi?
Mnyika: Sifahamu
Katuga: Kulikuwa na mipango ya kusimamia vurugu siku tofauti tofauti.
Mnyika: Sifahamu.
Katuga: Je uliwahi kupanga ama kujitokeza kumpinga Mwanachadema anaitwa Ishengoma wa Chadema kwamba matukio ya Tar. 29 chama kilihusika?
Mnyika: Taarifa unaijua wewe mimi sifahamu.
Katuga: Kwa mujibu wa hotuba ya Chande zilikuwa ni vurugu zilizoratibiwa na kupangwa?
Mnyika: Nilisikia Chande alisema hivyo. Kukubaliana nae ni jambo tofauti.
Katuga: Kuna watu walikamatwa kutokana na hizo vurugu za mwaka jana?
Mnyika: Walikamatwa na kuachiwa.
Katuga: Hao waliokamatwa walihojiwa kituo cha Polisi?
Mnyika: Sikuwepo.
Katuga: Waliofanya fujo zilitokana na kauli za kipenzi chao mwenyekiti wa Chama?
Mnyika: Sijaongea nao
Katuga: Uliwahi kuongea na mtu aliyekamatwa kwa kesi za uhaini mwaka jana?
Mnyika: Sijawahi kuongea na mtu wa aina hiyo.
Katuga: Tafsiri isiyo halali ni ipi?
Mnyika: Chochote kinachoweza kutafsirika na mahakama kuwa ni kuvunja sheria.
Katuga: Demokrasia ni nini?
Mnyika: Limeundwa na maneno mawili demo and cracy yaani utawala wa watu kwa ajili ya watu. Lazima uundwe na watu na ufanye kazi kwa ajili ya watu.
Part 325 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 312
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mnyika : Matendo aliyotuhumiwa nayo hayajawahi kutokea na DPP alipeleka hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo na kesi ilifutwa na Mwenyekiti Mbowe alikutana na Rais Ikulu. Toka kuwa mtuhumiwa wa UGAIDI hadi MAPOKEZI IKULU.
Watu wanacheka.😂😂😂😂😂
Na Lissu anasema kwa kejeli kwamba na Mimi itakuwa hivyo hivyo?😂😂😂
Mhe. Lissu: Hayo makesi yote na hii yangu vina uhusiano gani?
Mnyika: Hizi kesi zote ni mwendelezo wa kupambana na Chadema kwa kutumia Mahakama kukwamisha mapambano ya kudai demokrasia ya kweli na mabadiliko katika mifumo ya Uchaguzi. Haya ni matumizi yasiyo ya haki dhidi ya wapinzani ambao ni CHADEMA kutoka kwa Chama dola ambao ni CCM. Lengo lao ni kukwamisha mabadiliko tunayohitaji. Hivyo huu ni mwendelezo wa mambo mabaya ambayo yamekuwa yakifanywa na hawa serikali dhalimu.
Anataka kusimama Ajuaye.
Mhe. Lissu: Subiri namaliza muda sio mrefu. Umenifahamu lini?
Mnyika: Toka 2003 tukiwa wote kwenye sekretarieti, baadae Kamati Kuu na Baadae Bungeni miaka 23 nakufahamu.
Mhe. Lissu: Huyu mtu ni mtu wa aina gani ambae umemfahamu kwa miaka 23?
Mnyika: Toka mwaka 2003 tulipoenda kule Kwembe, nimekufahamu kama mtaka mabadiliko, ni mtu mkweli ambae siku zote umekuwa ni mtu unayetaka mabadiliko. Mimi naamini MASHITAKA HAYA NI GHARAMA UNAYOLIPA KWA KUWA MKWELI NA KUTAKA MABADILIKO NDANI YA TAIFA HILI.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Jaji nimemaliza kwa shahidi huyu.
Maneno aliyomalizia JOHN JOHN MNYIKA yamewafanya akina Mama waliopo humu MAHAKAMANI WATOE MACHOZI.
Yamekuwa ni maneno mazito sana na yenye ujumbe mzito, watu wamesikitika sana.🥹
Majaji wanaandika na kwa muda tulionao. Tutakwenda break na kurudi kwenye Cross Examination ya upande wa Jamhuri.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 314
Katuga anaendelea kumfanyia John Mnyika cross examination
Katuga: Ni kweli vyama hivyo vinaweza kuwa na Wanachama wake?
Mnyika: Siwezi kuwa na uhakika na wanachama wa vyama hivyo sina uhakika kama kweli vina wanachama.
Katuga: Hivyo vyama vingine pia vina itikadi yake?
Mnyika: Siwezi kuvisemea angalau ungeniuliza kuhusu Chadema, labda CCM na ACT ningweza kusema lolote.
Katuga: Mwanachama wa Chadema anapaswa kuheshimu Katiba?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Asiyefuata ni yule anayevunja Katiba ya Chadema?
Mnyika: Ni sahihi.
NB. KATUGA anamuuliza Mnyika kuwa ni form six. 😂 kila saa anaiulizia. Haoni hata aibu amekutana na shahidi form six lakini ana akili nyingi kuliko yeye na anamtesa vya kutosha.
Katuga: Si sawa kwa Mwanachadema yeyote kutokuamini anachokiamini mwanachama mwingine kwa itikadi yake?
Mnyika: Sasa sisi hatujasema tu habari ya vyama vingi kwa maana ya idadi.
Katuga: Kwahiyo mtu kupinga maoni ya vyama vingine ni kuvunja Katiba ya Chadema inayoamini vyama vingi?
Mnyika: Sio kweli maana upo uhuru wa maoni hata kupinga ni haki.
Katuga: Tarehe 03/04/2025 ulikuwepo kwenye Mkutano na nani alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo?
Mnyika: Hakukuwa na Mwenyekiti wa Mkutano.
Katuga: Kwahiyo mkutano wa Chadema hakukuwa na mwenyekiti wa Mkutano.
Mnyika: Sahihi Kabisa, hatunaga mwenyekiti wa Mkutano.
Katuga: Uliwaambia mikutano ipo ya aina gani?
Mnyika: Aina kuu ni mbili yaani Mkutano wa Hadhara na Mikutano ya ndani.
Katuga: Mikutano ya ndani na hadhara kwa mujibu wa Katiba ikoje?
Mnyika: Hakuna aina za mikutano kwenye Katiba ni taratibu za kiutendaji tu.
Katuga: Kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama alikuwa na cheo gani?
Mnyika: Alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama.
Katuga: Huo Mkutano ulikuwa na maudhui gani? Na ulisema ulikuwa wa nani?
Mnyika: Ni Mkutano wa Chama na Mwenyekiti alikuwa Mzungumzaji Mkuu.
Katuga: Hiki Chama chetu kinapoitwa watia nia na Chama wanaenda kuongea na nani?
Mnyika: Watia nia wanaenda kuongea na Chama.
Katuga:Kwahiyo hawaendi kuongea na Mwenyekiti, Katibu, Naibu
Mnyika: Unaongea na Chama kupitia viongozi wakuu wa Chama.
Katuga: Uliwahi kuita waandishi wa habari na kusema mashahidi wa Jamhuri kuwa ni waongo?
Mnyika: Lissu sio muhaini nimewahi kusema mambo ya kuzungumzia kesi sijawahi.
Katuga: Unaposema Mwenyekiti wetu hana hatia na sio muhaini. Haya maoni yako unayatoa kwa mujibu wa ushahidi wa jamhuri au maoni yako?
Mnyika: Kwa mujibu ninavyomjua Mwenyekiti.
Katuga: Wewe ni mratibu wa vikao vyote vya Chama?
Mnyika: Sio kweli.
Katuga: Vikao vya Kamati Kuu unaratibu wewe?
Mnyika: Ndio ni mimi.
Katuga: Hiki cha juzi cha Tarehe. 29/08 ulikiita wewe?
Mnyika: Ndio ni mimi
Katuga: Mwenyekiti wa Kikao anakuwa ni nani?
Mnyika: Mwenyekiti wa Chama kama hayupo anakuwa makamu Mwenyekiti.
Katuga: Kile mlichojadili mlikitolea taarifa kwa umma.
Mnyika: Nafahamu ilitolewa kwa umma taarifa.
Katuga: Mlijadili hii kesi kwenye kikao?
Mnyika: Tulipokea taarifa ya kuwa Mwenyekiti amekutwa na hatia.
Katuga: Bado unasema kuwa Katibu Mkuu ndio mtendaji mkuu?
Mnyika: Ni sahihi.
Katuga: Ni sahihi wanaweza wakatenda au wakafanya utendaji bila Katibu Mkuu kujua?
Mnyika: Wanaweza katika maswala yakawaida ya kiutendaji.
Katuga: Umesema Mwenyekiti alipendekeza na kuthibitishwa na Kamati kuu?
Mnyika: Sio Kamati Kuu bali ni Baraza Kuu.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema wewe ni shahidi mwenye interest?
Mnyika: Nina Party interest na Public interest.
Katuga: Kwa hicho ulichokisema na umesema amekuteua. Nitakuwa sahihi nikisema wewe una maslahi?
Mnyika: Maslahi unayosema wewe sio maslahi niliyonayo mimi. Ukitaka kujua maslahi yangu mitakwambia.
Katuga: Ulisomewa yale mashitaka. Unajua aina ya uhaini alioshitakiwa nao mwenyekiti?
Mnyika: Uhaini wa kuitisha serikali kwa kuchapisha maneno.
Part 315 Itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 187
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi ASP Geofrey Lutufye.
Mhe. Lissu: Mnajifanya mapolisi mnawasingizia watu vitu vya bure haya itakushangaza hao mliowakamata baada ya kesi yao kuisha ni mashahidi wa kesi hii?
ASP Geofrey Lutufye : Hainishangazi.
Mhe. Lissu: haikushangazi kwasababu huo ndio utaratibu wenu mapolisi wa Tanzania.
Mhe. Lissu: Au unabisha nikufungulie ripoti ya Jaji Mkuu Othman Chande amesema mnawafungulia watu makosa ya uongo.
Sasa nikuulize swali lingine, umewahi kuona video mimi nikiwa nazungumza habari za huo uchaguzi mkuu?
ASP Geofrey Lutufye : amekaa kimya
Mhe. Lissu: Unajua kwanini nimeshitakiwa kwa Uhaini ASP geofrey lutufye? Unajua sababu.
ASP Geofrey Lutufye : Sababu ya ile kauli uliyotoa.
Mhe. Lissu: Ipi hiyo?
ASP Geofrey Lutufye : Ulisema utazuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Mhe. Lissu: Ndio nakuuliza uliiona hiyo video?
ASP Geofrey Lutufye : Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Hawa ndio kesho watakuwa ma RPC siku inayofuata utashangaa anakuwa IGP,
Sina maswali mengine Waheshimiwa majaji.
Watu wanasonya tu hapa.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude kwa ajili ya Re-examination
Maelezo yako uliandika kama nani?
ASP Geofrey Lutufye : Kama shahidi.
Wakili: Unalizungumziaje kuhusu kujiandika mwenyewe?
ASP Geofrey Lutufye : naweza kujiandika mwenyewe au kuandikwa.
Renatus Mkude: Sina swali lingine. Re Examination imeishia hapo.
Jaji anamruhusu Shahidi.
Shahidi anatoka akiwa ameshika kipaza sauti.
Jaji Ndunguru: Unasahau maji yako hapo.
Shahidi: Hapana siyataki tena.
Jaji: Basi turudishie hiyo MIC tafadhali.
Anairudisha na kutoka nje akiwa anatikisa kichwa.
Watu wanacheka.😂😂😂
Kesi inaahirishwa watu wakale.
Tutaendelea baada ya lisaa limoja.
Naomba repost yako.
Jamaa mmoja alikuwa akifika bar anaagiza bia tatu tofauti safari, castle na kilimanjaro kisha anatafata meza yenye viti vitatu anakaa nakunywa zile bia moja bada ya nyingine zote tatu nakuondoka.
Alirudia hii tabia mara kadhaa ndipo mhudumu wa ile bar akashindwa vumilia ikabidi amuulize kwanini anafanya vile kuagiza bia tatu tofauti na kunywa zote?
Yule jamaa alimjibu kua waliwekeana makubaliano na rafik zake wawili ambao aliishi na kufanya kazi pamoja kwamba endapo wangetengana au kuhamishiwa maeneo tofauti basi kila mmoja popote atakapokua akienda bar kunywa basi awanunulie wenzake bia walizokua wanatumia na azinywe ikiwa sehemu yakuwakumbuka nakuenzi undugu au urafiki wao kwahiyo hata jamaa nao walikokua walifanya vile vile....
Siku nyingine tena mambo yalikua tofauti, jamaa aliingia bar nakuagiza bia mbili tu castle na kili, mhudumu alishangaa tena ikabidi amuulize kulikoni au kuna mmoja amefariki kati ya wale marafiki zake? Jamaa akamjibu hakuna aliyefariki wote wapo isipokua yeye ndo kaamua kuacha pombe...😁
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 17, 2026
Jana tuliishia Part 182 so leo tunaendelea na-;
Part 183
Mhe. Tundu Lissu ameingia muda huu leo makamanda wanaimba Shujaaa Shujaaa Shujaa.
Amepiga Tshirt yake nyeusi hapa.
Majaji nao wanaingia kama kawaida yupo
1. Jaji Dunstan Ndunguru Kiongozi wa Jopo.
2. Jaji James Karayemaha
3. Jaji Ferdinand Kiwonde
Wote watatu wapo wakiwa kwenye majoho yao mekundu na Beib nyeupe.
Renatus Mkude anasimama, yupo na ajuaye, Thawabu Issa, Ignas, Winiwa Kasawa pia.
Anasema leo wako na mashahidi watatu na tuko tayari kuendelea.
Jaji anamuuliza Mshitakiwa nae anamjibu niko tayari.
Majaji wanaandika kidogo.
Ukimfuatilia Mwenyekiti wa Jopo la Majaji, Jaji Ndunguru amekuwa anaonekana ni mtu mstaarabu.
PF 1864 ASP Geofrey Lutufye
Anaingia hapa kizimbani huyu ni askari huyu ni PW 9 ni shahidi ambae muonekano wake yupo kama amekesha hajanyoa nywele, ameshika kipaza sauti anatetemeka.
Naitwa PF18544 ASP Geofrey Aggrey Lutufye
Umri wa miaka 47.
Naishi Arusha.
Mkristu.
Huyu shahidi leo atadondoka kizimbani maana kwa anavotetemeka wote tunamuona hapa, Ukikutana nae barabarani huwezi sema ni Polisi maana amidevu na minywele yupo rafu sana.
Anaongozwa na Renatus Mkude.
Anaanza Renatus Mkude kumuuliza Maswali.
Wakili: Ikumbushe mahakama majina yako.
ASP Geofrey Lutufye: Anataja majina yake hapa
Wakili: Kazi yako?
ASP Geofrey Lutufye: upelelezi, niko ofisi ya mkuu wa upelelezi Arusha na mimi ni kiongozi wa kikosi cha Anti Robbery
Wakili: Anti Robbery ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Kikosi cha kuzuia uhalifu kama vile uporaji.
Kumbe ndio maana ana hali hii huyu askari. maana kiukweli amekaa hovyo sana kumbe anadeal na mambo ya kupora.
Wakili : Umepata mafunzo gani?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata tarehe 28/04/2003 Chuo cha Polisi Moshi.
Nilijifunza upelelezi na mafunzo mengine mbalimbali, nilimaliza mwezi wa 11, 2003.
Mafunzo mengine nilipata ya nyota ya kwanza, nilisomea Chuo cha Polisi Moshi ilikuwa ni Mwaka 2013 na baadae mafunzo ya cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi. Nililipata chuo Dar es salaam Polisi Academy hapa Dar es salaam nilimaliza mwezi wa 11 mwaka 2023.
Wakili: kingine ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Mengine ni on job trainning yaani mafunzo kazini.
Wakili: Una uzoefu kazini wa mwaka gani?
ASP Geofrey Lutufye: Miaka 15 ya upelelezi ninayo.
Wakili: Arusha uko tangu lini ofisi ya upelelezi.
ASP Geofrey Lutufye: Tangu mwaka 2023.
Wakili: kabla ya hapo ulikuwa wapi?
ASP Geofrey Lutufye: Nilianzia Polisi Oysterbay Dar es salaam, nilianza kama General Duty na baadae nikapelekwa Geita Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Geita ndo nikahamia mkoa wa Arusha baada ya huko.
Wakili: Majukumu yako hapo ofisi ya Upelelezi Arusha ni yapi?
ASP Geofrey Lutufye: Kufanya doria mbalimbali, kukamata watuhumiwa, kufanya upelelezi na kuwafikishia watuhumiwa Mahakamani.
Wakili: Tarehe 03/04/2025 kilitokea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuwa na wenzangu tukiwa na section 1 ambayo ni askari 9 hadi na dereva tukiwa kwenye doria.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Tulikuwa tunafanya doria tukiwa tunatumia gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser na nikapata maelekezo kutoka kwa kaimu mkuu wa upelelekezi ASP Bonny Mgogo.
Wakili: kwa njia ulipata maelekezo?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata kwa njia ya radio call ambayo ni kifaa cha mawasiliano. Maelekezo kuwa amepata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kwa Mromboo kijiwe cha Bajaji kuna vijana wanahamasishana kuzuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Wakili: Baada ya kufika huko kwa Mromboo nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuta vijana wakila njama za kuzuia uchaguzi Mkuu 2025.
Jaji anasema umesema Walikuwa wanakula nini?
ASP Geofrey Lutufye: Walikuwa wanazungumzia uchaguzi mkuu wa 2025.
Jaji: Kumbe walikuwa wanazungumzia sio kula tena?
Watu wanacheka.😂😂😂
Part 184 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 159
Anaendelea kusoma uamuzi Jaji Ndunguru
Pingamizi la nne lilihusiana na suala la fair trial na haki ya kusikilizwa.
Kwamba atashindwa kumdodosa pia shahidi vizuri kwasababu atakuwa haonekani na hawezi kumuhoji shahidi vizuri.
Mshitakiwa aliturejesha kwenye Katiba na Mikataba ya kimataifa juu ya haki sawa mbele ya Sheria.
Mahakama imetafakari hoja hiyo kwa makini haikuona ni kwa namna gani mshitakiwa atashindwa kumuhoji shahidi kwasababu hamuoni sura yake.
Pingamizi la tano kuhusu kifungu cha 194 cha CPA marekebisho yake hayakutangazwa kwenye gazeti la serikali hivyo ni Sheria ambayo haijaanza kutumika na sehemu ya pili mshitakiwa anasema kanuni za ulinzi wa mashahidi zimetengenezwa baada ya yeye kuwa ameshakamatwa na kufikishwa Mahakamani hivyo haziwezi kufanya kazi baada ya yeye kufikishwa mahakamani.
Upande wa Jamhuri walisema sheria za mwenendo zinatumika hata baada ya kuwa tayari mshitakiwa alishafikishwa mahakamani.
Je Sheria hiyo ilikuwepo wakati mshitakiwa alishafunguliwa mashitaka? Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi zimetengenezwa na Jaji Mkuu kwa mujibu wa kifungu cha 194 (3) cha CPA kilikuwepo toka mwaka 2018.
Hivyo basi vinaeleza kuwa ulinzi wa mashahidi unavyotakiwa kufanyika.
Jaji Mkuu amepewa mamlaka ya kutengeneza hizo kanuni za mashahidi hivyo basi kutengeneza kanuni mwaka 2025 wakati kanuni hizo zimetengenezwa chini ya kifungu cha 194 ambacho kilikuwepo toka mwaka 2018 basi hatuwezi kusema kanuni hizo ni sheria mpya.
Hata kanuni hizi zisingekuwepo basi hatuwezi kusema mashahidi wasingeweza kulindwa kwasababu kanuni hazikuwepo au hazijatungwa.
Mahakama imeridhika kuwa kifungu cha 194 kilikuwepo kabla ya kanuni hizi za 2025 na hatuwezi kusema sheria ya ulinzi wa mashahidi haikuwepo lengo la kanuni hizo ni kurahisisha utekelezaji wa kifungu cha 194 cha Sheria ya mwenendo wa Makosa ya jinai.
Wakati upande wa Mashitaka walitoa gazeti kuonesha sheria hiyo ilitangazwa na Mshitakiwa alisema hakufanikiwa kupata gazeti hilo na kusema sheria hiyo haikutangazwa.
Kifungu cha 63 na 64 cha ushahidi wa judicial notes kuwa sheria hiyo ipo na kuamini.
Mahakama imejiridhisha kuwa sheria hiyo ilitangazwa na imekubali pingamizi moja na mapingamizi mengine manne yaliyobaki Mahakama imeyakataaa.
Hivyo kizimba kirekebishwe na tuendeleee na usikilizwaji wa kesi kama ilivyoamriwa hapo juu.
Anasimama Renatus Mkude anasema baada ya kupata amri na uamuzi wa Mahakama tunaomba ahirisho ili kizimba kirekebishwe.
Anaitwa Mh. Lissu aseme.
Anasema yeye anapinga kesi kuahirishwa.
Jamhuri wa Mashahidi 30 na waliolindwa wapo 11 na 19 hawajalindwa sasa walipaswa kujua kuwa mahakama ikikataa mashahidi kulindwa lazima wawe na shahidi mwingine wa kuleta.
Hii ya kuahirisha kesi kwasababu ya kurekebishwa kizimba ni kunionea na kunikosesha haki zangu.
Waheshimiwa Majaji mimi sina hatia yoyote hii ya kuahirisha kesi kwa sababu hii siiungi mkono kwasababu mkiahirisha mimi naenda kukaa jela.
Anasimama Mkude tena anasema Mheshimiwa tuliwaandaa hao mashahidi wa siri kwa sasa hatuna shahidi mwingine yeyote na huo ndio utamaduni wetu wa kuendesha hizi kesi Mawakili wa Serikali kwahiyo hoja ya kuahirisha iko pale pale. Tunaomba tuahirishe kizimba kirekebishwe.
Naona Majaji Wanateta hapa.
Anawasha kipaza sauti Jaji Ndunguru.
Anasema tumesikia hoja zote, shauri hili litaendelea kesho February 12, 2026 saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
Vitu vya muhimu sana kwa kila MUANDAMANAJI 29.10.
Mapambano yakuwa ni MAKALI SANA—sio rahisi Wakoloni weusi kukubali kutusikiliza tunachotaka maana wanajua mwisho wao ni JELA. Lazima wapambane kubaki walipo, na sisi tunatakiwa kuwaonyesha nguvu ya UMMA.
REPOST 200
#MO29
#MaandamanoOktoba2
#SiriNiNamba
#TUPOWENGI
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Muda huu Sirari tarime baada ya tukio la kutekwa kwa mmoja wa wafanyabiashara, mapambano ya polisi na raia yanaendelea.
Ukinyamaza wakati haya yanatokea kesho mwanao yatamkuta haya paza Sauti kemea #Mo29
Hatimaye Enock Heche mdogo wa Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche ameachiwa kwa dhamana usiku huu.
Mungu awabariki sana wote mliopaza sauti zenu kwa ajili yake.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 136
Anatoa kesi nyingine ya Maghimbi Mzini Criminal appeal No. 304/2023 Mahakama ya Rufani
Ukurasa wa 21 unasema admissibility of documentary evidence huo ni mtego na Mahakama isiingie hapo.
Kwa kumalizia Mahakama hii naomba isiyazingatie mapingamizi ya Mshitakiwa.
Jaji anasema Mshitakiwa karibu kwa ajili ya Rejoinder.
Mhe. Lissu anaanza.
Waheshimiwa Majaji msishawishiwe na uamuzi wa awali kuhusu admissibility ya flash disk na memory card kwasababu hivi vitu viwili ni tofauti kabisa.
Hivyo msishawishike kusimama na msimamo wenu wa flash disk na memory card.
Wakili wa serikali Mkuu hajaelezea kwanini hizo nyaraka ni tofauti.
Sasa Majaji ni kweli hivi vitu ni tofauti kimoja ni karatasi na kingine ni memory card huo utofauti ni wa kweli hata kama hajaelezea.
Lakini swali la msingi hapa ni hii ripoti ambayo iko tofauti na flash na memory card inahusu nini? Content yake ni nini? Inahusu flash disk na memory card pamoja na kwamba they are different but they are related.
Bila flashdick na memory hakuna report na hayo ndio mahusiano yake kimoja kikianguka kingine hakiwezi kusimama.
Hii report Waheshimiwa Majaji kwasababu ni report ya Vitu vilivyokataliwa na Mahakama haiwezi kusimama yenyewe, kusimama kwake kunategemeana na kile ilichokichunguza.
Waheshimiwa Majaji kama taarifa ikipokelewa haitakuja kuprove chochote Mahakamani.
Wakili wa Serikali Mkuu Mrema amewaalika msiangalie content za hiyo report na anasema mimi nimeenda kwenye content za report.
Wakili wa Serikali Job Mrema anasema the fact kwamba hiki kielelezo hakijaitwa CERTIFICATE kuitwa kwake taarifa hakubadilishi Content.
Hii sio kesi ya kukosewa jina. This is not the case of misnaming this is a case of something being tendered which have never been tendered.
Hii taarifa sio tu taarifa jina ni taarifa kwa content kungekuwa na umaana wa hii taarifa yao wangeambatabisha na kurasa moja ya Certificate kwa mujibu wa sheria.
Sasa wametuletea kurasa 11 za maandishi hiyo tunaita nini kama sio taarifa?
You should not be persuaded kuwa hili jina halina shida, hilo jina linaelezea kilichopo ndani.
Maghimbi Mzini dhidi ya Jamhuri ni kesi nyingine imeletwa na wenzetu pia hii kesi haiwasaidii hata kidogo naomba nisome paragraph mbili kwenye ukurasa wa 21.
Amesoma hiyo kesi.
Anasema hoja hapa hatujajadili uzito wa ushahidi wa hiyo taarifa, My only contention has been hii taarifa is not admissible.
Haijakidhi matakwa ya sheria ya kupokelewa kama kielelezo, sijasema ripoti hii ni ya uongo na ina mambo yasiyo ya ukweli.
Mimi sijafika huko nimeishia kwenye suala la kwamba hayakidhi vigezo.
Kwahiyo with all due respect hii kesi ya Maghimbi Mzini haiwasaidiii kwasababu inasema tusichanganye uzito wa ushahidi na kupokelewa kwa kielelezo.
Ni hayo tu Mhe. Jaji, Mhe. Lissu amemaliza kufanya Rejoinder
Majaji wanaandika kidogo.
Mawakili wa Serikali kwa mara ya kwanza leo wapo na kahali fulani ambako ni kama hawaitaki kesi kabisa.😂
Ukiwaangalia unaona moja haikai na mbili haikai, wapo wapo kama wamerogwa.
Majaji wanamaliza kuteta hapa.
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti.
Anasema Mahakaman itatoa uamuzi kesho saa tatu asubuhi.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 134
Anaambiwa hapa Mh. Lissu kuwa GN. iliyomteua ilikuwa inasema anapaswa kuteuliwa na AG na sio DPP.
Mhe. Lissu anawaomba hapa Vijana wake wamfanyie research kama kipindi hicho sheria ilikuwa inasema hivyo.
Anaambiwa ni sahihi.
Anasema sasa nakubali hata kama Sheria inasema AG ndio alipaswa kumteua swali la msingi linabaki kuwa AG alimteua shahidi huyu kama mtaalamu wa picha na sio mtaalamu wa video.
Lakini pia shahidi ameandaa taarifa badala ya Certificate wakati CPA imetoa kwenye third schedule format ya hiyo certificate.
Pia GN. No. 823 na GN. No. 825 zimewataja wataalamu wa cyber forensic na huyu shahidi hayumo.
Kwahiyo nasisitiza vielelezo hivi visipokelewe kwa maana ya ripoti ya mtaalamu.
Naomba kuishia hapo.
Majaji wanateta kidogo pale na wanawaita upande wa Mashitaka.
Anasimama Renatus Mkude na anasema mara baada ya kupokea ile ruling ya kwanza na Mshitakiwa ameirejea sana ile ruling ya kwanza tunaomba nusu saa ya kwenda kutafakari halafu tukirudi tutakuja na msimamo wa namna ya kwenda mbele.
Majaji wanateta kidogo.
Jaji Nduguru anasema Mahakama imehairishwa mpaka saa sita mchana ili upande wa Jamhuri waende kutafakari.
Watoto wa mjini wanasema Hii Kesi ishakuwa ngumu, aliyetumwa kumpelekea chakula mtuhumiwa na yeye kakamatwa kawekwa lock.😀😀😀
Tukutane baada ya nusu saa.
Naomba Repost yako.
Viongozi wetu watano wilaya ya Bukoba na Mkoa wa Kagera.
Katibu wetu wa wilaya ya Kyerwa.
Bado wanashikiliwa na polisi kwenye eneo lisilojulikana..
Familia, marafiki na wanachama hawajaruhusiwa kuwaona..
Huu ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu, uvunjifu wa sheria zetu za Nchi… uhalifu na impunity ya hali ya juu sana.
Tunalitaka jeshi la polisi kukomesha mara moja tabia hizi, kufanya siasa dhidi ya ccm sio kosa kwa mujibu wa sheria zetu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 133
Anaendelea kusoma uamuzi Jaji Nduguru
Kilichotokea hapa Mahakamani shahidi ametender flash disk yenye hizo video na memory card.
Ingawa upande wa Mashitaka uliishawishi Mahakama kuwa hizo flash disk zimebeba picha na video na wakatumia shauri la India.
Mahakama imepitia upande wa Mashitaka na hoja zao walizoleta.
Mahakama imerejea kwenye kifungu cha 216 cha CPA kikirifaa mambo ya picha na hakisemi kuhusu video.
Hivyo vitu viwili vina maana tofauti kuhusu photograph na video na Jamhuri wameshindwa kutofautisha.
Shahidi Na. 3 alichokuwa anataka kukitoa hivyo vitu sio photographic prints wala enlargement.
Kwahiyo huyu shahidi hana uwezo wa kutoa hiyo video na Mahakama imekataa kupokea hizo video.
Wataalamu wa electronic ndio walipaswa kuja kutoa hizo video na tumeona ipo GN inayohusiana na video na mambo ya kielektroniki kwa ujumla.
Baada ya kusema hayo Mahakama inakubaliana na pingamizi la mshitakiwa.
Jaji anasema tuendelee sasa.
Kabla hatujaendelea kwa kifupi ni kwamba VIDEO AMBAYO SASA NDIO USHAHIDI WENYEWE WA KESI IMEKATALIWA. KWAHIYO HAYO WANAYOSEMA YALISEMWA NA LISSU AMBAYO NDIO UHAINI WENYEWE. MAHAKAMA IMEUKATAA. KWA KIFUPI KESI IMEISHIA LEO. HAPA TUNAPOTEZA MUDA KUSUBIRI HUKUMU.
Anasimama Thawabu Issa kuanza kumuongoza Shahidi.
Sasa shahidi ulizungumzia kuhusu taarifa ya uchunguzi.
Ukiiona utaijuaje.
Samwel Elibariki Kaaya: Nitaitambua kwa majina yangu, logo ya Polisi, signature, Muhuri na tarehe.
Thawabu Issa: Naomba Waheshimiwa Majaji naomba nimuonyeshe Nyaraka shahidi.
Jaji: Muonyeshe.
Anapewa shahidi nyaraka kadhaa.
Shahidi anasema hii ndio ripoti ya kitaalamu niliyoiandaa ina majina yangu na vyote nilivyosema awali na niliandaa mwenyewe.
Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama?
Shahidi: Ipokee kama sehemu ya kielelezo.
Jaji: Mpatieni Mshitakiwa.
Mhe. Lissu anaiangalia anasema napinga hiyo taarifa kupokelewa kwa hoja zifuatazo.
Hii inaitwa Mbwa kala Mbwa.😀
Mhe. Lissu anaanza tena.
Waheshimiwa Majaji kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Jinai shahidi anayetakiwa kuwasilisha taarifa za uchunguzi wa kitaalamu, anapaswa kuwa ni shahidi aliyetamkwa kwenye kifungu cha 216, 217, 218 na 220 vya Sheria ya Mwenendo wa Jinai.
Sasa Waheshimiwa Majaji shahidi huyu ni shahidi wa picha za mnato kwa maelezo yake yeye mwenyewe mtayaona kwenye kielelezo anachotaka kukiwasilisha.
Mimi Samweli Kaaya Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi ambae ni mtaalamu wa picha chini ya kifungu cha 202(1) cha CPA.
Sasa anaendelea Mh. Lissu.
Sasa Waheshimiwa Majaji hicho kifungu cha 202(1) cha CPA ndio kifungu cha 216 cha sheria ya sasa kinazungumzia hati za wataalamu wa picha mnato.
Wao wanakitumia kuleta kielelezo ambacho ni video.
Waheshimiwa Majaji WINO HAUJAKAUKA. toka muamue kuwa huyu shahidi hapaswi kuleta ushahidi wa video hapa Mahakamani maana yeye sio mtaalamu wa video.
Shahidi yeye mwenyewe amejisema kuwa yeye sio shahidi competent, amejisema Mwenyewe.
Tunaanzaje kumkubalia?
Na hawa Mawakili wa Serikali sijui wana akili au wamerogwa maana muda mfupi uliopita Mahakama imewaambia kuwa huyu mtu sio mtaalamu wa video ni mtaalamu wa picha, wao wanataka kutuletea hapa mtaalamu wa picha aliyechunguza video ni kituko.
Kwenye kielelezo chake mwenyewe shahidi anasema pia ameteuliwa na tangazo la serikali 799 lilitolewa na AG Adeladus Kilangi halikutolewa na DPP.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakuwa na Mamlaka na hana mamlaka ya kuteua mtaalamu yeyote aliyesemwa kifungu cha 216 hadi 220 cha CPA.
Mawakili wa Serikali wapo na ubaridi mkubwa wamekuwa wadogo sana kama Pilton.
Sect. 216 ya CPA inazungumzia Certificate ambayo ndo ripoti yenyewe ya mtaalamu na kinasema pia uteuzi wa huyo mtaalamu anapaswa kuteuliwa na DPP na sio AG.
Part 134 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 112
Anaendelea Wakili wa Serikali Thawabu Issa
Hii Meta Data ni nini hasa?
Meta Data ni Data about Data. Yaani picha mjongeo ni Data ndani ya Picha mjongeo kuna Data nyingine ambazo ni taarifa. Hzio taarifa zinaweza kuwa tarehe, jina na kadhalika. Taarifa hizo mjongeo zilizopo kwenye picha mjongeo ndio tunaita Meta Data.
Anasimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali huyu Baba ni mstaarabu kwakweli. Yeye muonekano wake hana nouma. Anaongea kistaarabu sana. Hana arrogance yoyote. Kwa kumuona tu haoneshi kuwa kisirani kama mawakili wengine wa Serikali.
Anasema kwa sasa ni saa saba naomba tupate break watu wakapate Chakula.
Majaji wanaandika kidogo.
Wanamuuliza Mshitakiwa. Anasema sina pingamizi.
Wanaandika kidogo. Wanasema sasa twendeni break tukutane baada ya lisaa limoja kutoka sasa. Tumeishia hapo kwa sasa. Tukirudi Shahidi ataendeelea kutoa ushahidi wake kwa maana ya EXAMINATION IN CHIEF ITAENDELEA.
Kumbuka jina la Shahidi ni SAMWEL ELIBARIKI KAAYA alkiongozwa na Wakili wa Serikali Thawabu Issa.
Tukutane baadae kidogo.
Naomba Repost yako