@godbless_lema Mmhโฆ..nilikuwa nazisoma comments za wadau hapa, nikabaki njia panda. Nashindwa kuelewa kaka, huyo Banjoo alikuwa kweli ni Business man? Au mtu wa kazi? All โn all, ajuae Mungu na Yeye ndiye Hakimu wa Mahakimu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 164
Anaendelea Mhe. Lissu na cross examination.
Mhe. Lissu: Uliporudi nyumbani kwako umesema kwamba ulimpigia ndugu yako askari?
Shahidi wa kificho: kweli.
Mhe. Lissu: ulisema anafanya kazi tabata relini?
Shahidi wa kificho: kweli.
Mhe. Lissu: Tuoneshe yako wapi kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo.
Mhe. Lissu: huyo ndugu yako askari Polisi ana jina?
Shahidi wa kificho: ndio jina analo.
Mhe.Lissu: Polisi umemtaja jina? Waeleze majaji kama kuna mahali umemtaja jina?
Shahidi wa kificho: Sijamtaja.
Mhe. Lissu: Ana cheo chochote?
Shahidi wa kificho: sijui kama ana cheo chochote.
Mhe. Lissu: ana force no?
Shahidi wa kificho; sijui hata maana yake mimi.
Mhe. Lissu: ulipoangalia ile video ukaona maneno ukapata hofu?
Shahidi wa kificho: kweli.
Mhe. Lissu: kwenye maelezo yako wapi?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo hayo.
Mhe. Lissu: Tarehe 09 siku unaandika maelezo yako Polisi ulipofika Central ulimpigia simu aliyekupigia mwanzoni?
Shahidi wa kificho: ndio.
Mhe. Lissu: uliandika wapi kwenye maelezo yako polisi?
Shahidi wa kificho: Yapo yameandikwa lakini hapa hayapo.
Mhe. Lissu: maana yake nini sikuelewi?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo.
Mhe. Lissu: Yale maneno kwamba tutakinukisha ndio yaliyotokea siku ya Uchaguzi ulisema hivyo?
Shahidi wa kificho: Ndio nimesema.
Mhe. Lissu: je uliandika maelezo ya ziada polisi ili kujumuisha kilichotokea tar. 29/10 au wamekupanga tu uje uongeze na hayo.
Shahidi wa kificho: Tar. 09/04 ndio maelezo yangu.
Mhe. Lissu: kwahiyo huna maelezo ya ziada?
Shahidi wa kificho: kwa hapa hamna na hayapo kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Mhe. Lissu: Najua akina Mafwele, Kingai na George wamekwambia tu kaseme sasa nakuuliza yapo maneno hayo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Shahidi wa kificho: Unanichanganya mimi.sijui.
Mhe. Lissu: Ulikaa ndani siku sita ukiwa na njaa. Hebu tuonyeshe kama yapo kwenye maelezo yako polisi?
Shahidi wa kificho: Kwa hapa hayapo ili niliyatolea maelezo.
Mhe. Lissu: Kwahiyi Mapolisi wamekuuza na kukupuuza, uliwaambia vitu hawakuandika?.
Shahidi wa kificho: Kimya
Mhe. Lissu: Sasa nimemaliza kukuonesha kuwa wewe ni mtu wa kupuuzwa huaminiki. Ngoja nianze kukuuliza maswali yangu sasa.
Watu wanacheka.๐๐๐
Mhe. Lissu: Huo mtandao wa Facebook ni account ya nani?
Shahihi wa kificho: ilikuwa kwenye account yangu ya faceebook.
Mhe. Lissu: unaelewa kweli unachojibu? Niambie account inaitwaje?
Shahidi wa kificho: Sikujua account inaitwaje.
Watu wanacheka.๐๐๐
Mhe. Lissu: uliona video ya Tundu Lissu. Sasa Majaji hawajaona hiyo video. Wewe umewaonyesha.
Shahidi wa kificho: Simu yangu ilipotea mwaka jana.
Mhe. Lissu: umewaonyesha.
Shahidi wa kificho: Sikuwaonyesha.
Mhe. Lissu: Umeiwasilisha hiyo video Mahakamani?
Shahidi wa kificho: sikuiwasilisha.
Mhe. Lissu: ulipompigia yule askari simu na kumuuliza kama wameyasikia ya Tundu Lissu. Hayo unakumbuka ulisema?
Shahidi wa kificho: ndio nakumbuka.
Mhe. Lissu: Je ulienda kutoa polisi taarifa?
Shahidi wa kificho: Sikwenda.
Mhe. Lissu: Huyo ndugu yako Polisi alikwambia uende kufungua RB polisi?
Shahidi wa kificho: Hakuniambia hayo.
Mhe. Lissu: Ulichosikia kwenye video kwamba kukinukisha sasa tusaidie maana ya kukinukisha ni nini?
Shahidi wa kificho: muashirio ya kuchocheo fujo au vurugu.
Mhe. Lissu: Umeyatoa wapi hayo? Mimi nina kamusi ya kiswahili. Unataka nikusomeee?
Shahidi wa kificho: sio mbaya.
Mhe. Lissu: anamsomea tokwa na harufu mbaya au vunda. Na nukia na toa harufu nzuri yakunukia kama vile marashi. Haya yakwako umetoa wapi?
Shahidi wa kificho: Mimi nimesikia mitandaoni na kupitia watu pia.
Mhe.Lissu: Kwahiyo kamusi yako ni mitandao na watu?
Shahidi wa kificho: ndio.
Mhe.Lissu: Je kuna mahali kokote Polisi uliposema maana ya kukinukisha ni kufanya fujo kwenye hayo maelezo yako?
Part 164 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 162
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali ya Dodoso
Mhe. Lissu: Una leseni ya biashara?
Shahidi wa Kificho; Leseni ya Biashara sina ila ninayo naiandaaa.
Mhe. Lissu: Una kitambulisho cha NIda?
Shahidi wa kificho; Sina ila napambana nikipate.
Mhe. Lissu: una kitu chochote cha kukutambulisha ni mfanyabiashara zaidi ya maneno yako?
Shahidi wa kificho: Kile ninachotembeza ndio ushahidi wangu.
Mhe. Lissu : Umekileta hapa?
Shahidi wa kificho; Sijaleta.
Mhe. Lissu: Watajuaje we ni mfanyabiashara.
Shahidi wa kificho: Waniamini tu.
Lissu: unakaa ubungo kibangu?
Shahidi: ndio.
Umeleta mkataba wa pango? Au umesema unakaa nyumba gani?
Shahidi: sijaleta ila labda niende nao Ubungo Kibangu wakapaone.
Mhe. Lissu: Unadhani majaji hawana kazi hadi waende kibangu?
Shahidi wa kificho : Sijui wao.
Mhe. Lissu: Unakumbuka ulitoa maelezo kule Polisi?
Shahidi wa kificho; Ndio nakumbuka.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa naomba apewe maelezo yake huyu P5 ayaone.
Wanamtafutia. Wameyapata. Wamempa huko kwenye kiboksi chake.
Shahidi wa kificho: Haya ndio maelezo yangu niliyoandika Central Polisi.
Mhe. Lissu: yana sahihi yako
Shahidi wa kificho: Ndio yana sahihi yangu.
Mhe. Lissu: Mh. Nataka nimsomee shahidi maelezo yake anamsomea hapa maelezo yake yote.
Anasema anajishughulisha na kuuza maeneo mbalimbali posta na kuosha magari.
Niliona video ya Tundu Lissu ambae ni Mwenyekiti wa Chadema aliyesema mwaka huu hakutakuwa na uchaguzi na nitakinukisha.
Baada ya kumaliza mizunguko yangu nilirudi Ubungo Riversid na nilipita kijiwe cha kahawa yupo rafiki akaonesha video ndefu sana tofauti na ile niliyoiona mimi. Wengine walimuunga mkono Lissu wengine walipinga.
Baada ya kuona video nikaona nchi inaenda kuingia kwenye vurugu na itatuathiri sisi tunaotafuta riziki mitaani.
Nikamtafuta ndugu yangu ambae ni Polisi kuhusu maneno ya Tundu Lissu na akanijibu tumeyasikia na tumeyaona.
Nikapigiwa simu na Polisi na kwenda Central kutoa ushahidi.
Mhe. Lissu anasema sasa nataka kukuhoji kuhusu.
1. Mambo ya Aina ya simu yako sijaona kwenye maelezo yako.
2. Namfahamu Lissu kutokana na vyombo vya habari. Hayapo kwenye maelezo.
3. Maskani kijiwe cha kahawa hayapo kwenye maelezo.
4. Mtu uliyempigia simu anafanyakazi Tabata Relini. Hayapo pia
5. Ulipata hofu hayo pia kwenye maelezo yako kulikuwa na hofu.
6. Ulipofika Central ulimpigia simu huyo askari hayapo kwenye maelezo.
7. kwamba ulipigwa na njaa kwelikweli siku 6 ulizokaa
Mh. Tundu Lissu anaendelea kusoma amesoma maeneo zaidi ya 14 anayotaka kumkanusha shahidi ameyasema Mahakamani lakini kwenye maelezo yake ya Polisi hakuna.
Mhe. Lissu: Je ungependa maelezo yako haya yawe sehemu ya ushahidi hapa Mahakamani.
Shahidi wa kificho: Sijakuelewa hapo.
Mhe. Lissu: Je ungependa maelezo yako yawe ushahidi Mahakamani?
Shahidi wa kificho: Ndio.
Majaji wanateta pale juu.
Mawakili wa Serikali wanaulizwa mnasemaje?
Anajibu Renatus Mkude. Sisi hatuna Objection yanaweza kupokelewa tu.
Majaji wanaandika pale.
Basi maelezo ya P5 yatakuwa ni Kielelezo D3 yaani kielelezo No. 03 cha upande wa Mshitakiwa. Kwa kifupi Mh. Lissu ameshakuwa na vielelezo vitatu upande wake kabla hajaanza kujitetea upande wake. ๐ Hadi muda huu Jamhuri hawana kielelezo hata kimoja kilichopokelewa na Mahakama maana vyote vilikataliwa.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa naomba apatiwe maelezo yake.
Shahidi wa kificho: anapatiwa maelezo yake.
Mhe. Lissu: Sasa tueleze ulisema unapatia bidhaa zako ilala boma sokoni sasa angalia maelezo yako na useme hayo maelezo kama yapo?
Shahidi wa kificho: yapo.
Mhe. Lissu: Hebu nionyeshe.
Shahidi wa kificho: Amekaa kimya huko anapatafuta.
Mhe. Lissu: Waonyeshe Majaji mimi siruhusiwi kukuona.
Shahidi wa kificho: yuko kimya huko.
Mhe. Lissu: hayo maneno yapo au hayapo Kaka, natumaini we ni mwanaume.
Part 163 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Video showing Electoral Commission officials ticking all ballot papers in favor of Museveni at a polling station in western Uganda. This is what Museveni and his criminal system call an election! We campaigned. We voted. We tried to protect our vote but the criminals arrested or abducted many of our agents and officials. The only recourse is for the PEOPLE OF UGANDA to reclaim their voice. That is why we called this a PROTEST VOTE.
Please keep those videos coming in - and all other evidence of the theft that took place on the 15th.
#FreeUgandaNow
Cameroonian ๐จ๐ฒ football superstar and President of the Cameroonian Football Federation Samuel Etoโo met his longtime teammate, now working as a security guard, at an Ecobank seminar in Douala, Cameroon in 2025.