Usipochagua nini cha kulisha ubongo wako mtandaoni, litakuwa jalala (dampo) la kila, "content" unayokutana nayo.
Bahati mbaya sana, "Useless content" zina mvutano mkubwa na dopamine zetu.
Ndiyo maana makala Ndefu au thread yenye vitu vya kukuongezea ujuzi, unapata shida Sana kusoma au unaskip tu.
LAKINI, udaku, vichekesho na vitu vingine ambavyo siyo vya muhimu sana vinakula muda wako.
Unaweza ukajikuta kila ukiingia, online una-scroll tu huku na kule, unashangaa dakika, masaa au siku inakatika.
Na 'Alogarithms' zilivyo za ajabu, zinarekodi, 'behavioral patterns" yetu juu ya kontenti tunayo-consume daily kwa asilimia kubwa.
Alafu, kila ukiingia online inakusukumia mzigo wa content unaoendana na kile unachokula kila siku.
Mwisho wa siku inazaa addiction!
Choose wisely!
Unaona vile vyakula wanakula watu;
Wenye BP,
Wenye sukari,
Wenye matatizo ya figo,
Wenye cancer,
Kula hivyo vyakula na vile wasivyokula achana navyo hili hutafundishwa kokote shuleni.
Maisha ya watu wengine ni somo la kila siku kwetu ni vile tu huwa tunaamua kutokujali.