I think sahizi FOLLOWERS sio SUALA tena.
Nimejaribu kueka scrappers za TikTok,IG,X na Youtube afu nikaambia CLAUDE kila asubuhi inaangalia top performing content kwenye Niche yangu.
Nikiamka tu inadrop content,hook wametumia, kwanini imeenda viral, link kwa hiyo post etc. so unaTelezea GANDA LA NDIZI
Ni gharama ofcoz
I’m sorry CHATGPT silipii tena🤣
Naishi Building moja na UbepariPc , japo yeye hajui 😅. Hata jana tumeonana.
Ni mmoja wa influencers waliokuwa na mchango mkubwa kunifanya nije Dubai. Kabla ya hapo sikuwahi kumjua binafsi. Nilimfahamu kupitia @eddygotya .
Eddy alinambia, “Bro Gaby, unaweza kuuza PC kuliko kitu chochote.” Afu akanitumia link ya IG ya Ubepari.
Kuanzia hapo, nikaghairi mpango wangu wa kwenda China na kuamua kwenda Dubai.
Hii interview ni MASTERCLASS kweli. 🔥check 👉🏽 https://t.co/CzaUxndRUn
S/o to @amrisaly@Mike_Dastan n the TEAM
Anza Leo. Usingoje perfect moment anza na uliyonayo.
➮ Nenda Google uka-search: “𝗚𝗢𝗢𝗚𝗟𝗘 𝗗𝗜𝗚𝗜𝗧𝗔𝗟 𝗚𝗔𝗥𝗔𝗚𝗘”
↳ Ingia kwa email yako
↳ Chagua skill yoyote ya digital unayoipenda
↳ Anza course (ziko simple + step by step)
↳ Fanya assignments zote
↳ Ukimaliza unapewa cheti (certificate)
➮ Weka hicho cheti kwenye LinkedIn yako
➮ Tumia kuomba kazi au freelance gigs
Kozi zote ni 𝗕𝗨𝗥𝗘. Hakuna kisingizio.
Lakini ngoja nikuambie kitu ambacho watu wengi hawasemi…
Course peke yake haitokupa pesa.
Skill + matumizi yake ndiyo inaleta pesa.
Ndiyo maana tunafanya hii kama CHALLENGE 👇
You're not lazy – your brain is experiencing functional freeze.
You know everything you need to do, but you cannot physically start. Starting a new routine every 2 weeks, getting obsessed with a system but abandoning it overnight. If you’re struggling.
Take the 3 minute quiz
🚨 Toni Kroos tells Marca: “Luis Enrique subbed out Ousmane Dembélé, his best player, in the 65th minute of a Champions League semi-final and nobody complained. He exits the pitch, shakes his coach’s hand and sits on the bench cheering his teammates. There are some counter examples to this.”
“You look at Ousmane Dembélé, and how he's yelling at his teammates to keep fighting, from the bench. That's not what 90% of players who think they're stars would do. They start to do bad gestures on the pitch, then sit on the bench sulking.”
Usiogope kujitafuta upya, hata kama italazimu ku-relocate.
Maisha ni marathon,Using’ang’anie vitu, mazingira, au watu ambao hawakufanyi kukua, bali wanakuua taratibu ndani yako.
Wakati mwingine hatua ya kuondoka ndiyo mwanzo wa kuishi kweli.
Pumzika kwa amani James Robert Temba.
Mwanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), James Robert Temba (24), anatekwa, anapatikana baada ya siku kadhaa akiwa amekatwa kichwa, kiwiliwili/mwili wake unaelea Mto Msimbazi, Kipawa, Dar es Salaam.
Uongozi wa Institute of Finance Management (IFM) na Serikali ya Wanafunzi (IFMSO) kimya. Hakuna tamko la kulaani au kutoa pole. Uongozi wa chuo na Uongozi wa Wanafunzi kimya kama hakuna kitu kilichotokea.
Hakuna tamko kutoka Jumuiya ya Wanafunzi wa elimu ya Juu (TAHLISO). Hakuna kauli ya kuwahakikishia usalama wanafunzi au kutaka uwajibikaji kutoka Wizara ya Elimu. Nchi yetu imeanguka vibaya katika shimo refu sana.
Ukimya huu ni kielelezo ukatili na uhalifu unachukuliwa kama jambo la kawaida, na kukemea maovu ni kitendo hatari. Hii ni athari ya taasisi muhimu kufanywa kuwa matawi ya CCM. Hata taasisi za elimu zimepooza.
James Temba alikuwa mwanachama wa CCM. UVCCM wenzake wameshindwa kuona sababu za kutoa TAMKO kulaani na kutaka uchunguzi wa haraka wa mauaji ya mwanachama mwenzao? Taasisi takamwili hizi.
Pongezi CHADEMA STUDENTS ORGANIZATION (CHASO), mkoa wa Dar es Salaam kwa kuchukua wajibu rasmi wa kumkumbuka mwanafunzi mwenzenu wa elimu ya juu kutoka Institute of Finance Management (IFM).
Mazishi ya James Temba ni kesho 07/05/25, Old Moshi, Kilimanjaro. Leo 06/05/25 mwili utawasili nyumbani baadae kutakuwa na ibada, KKKT – Usharika wa Tabata kabla ya kuanza safari kuelekea Kilimanjaro.
Poleni sana familia ya James Robert Temba (2002 – 2026).
Gen Z si adui; Ni wateja wa siasa na uchumi wa kesho.
Making Africa Work: A Handbook (waandishi ni Greg Mills, Jeffrey Herbst, Olusegun Obasanjo, na Dickie Davis). Kitabu kinasisitiza kuwa Afrika inapitia ongezeko kubwa la watu kuliko bara lingine lolote.
Mmoja wa waandishi, Olusegun Obasanjo (Rais wa zamani wa Nigeria), ameandika kwamba “Making Africa Work” kunahitaji uongozi wenye maono ya mbali sana, siyo uongozi wa kuzima moto wa maandamano.
Idadi ya watu itaongezeka mara mbili hadi kufikia bilioni 2 ifikapo mwaka 2045. Zaidi ya nusu ya Waafrika wataishi mijini. Kundi hili litakuwa na vijana ambao wanaunganishwa kupitia simu na mitandao ya kijamii.
Hadi kufikia 2050, robo ya idadi ya watu duniani itakuwa Afrika. Ongezeko linaweza kuwa baraka ikiwa vijana watapata kazi na elimu, au likawa janga ikiwa serikali zitashindwa kuweka mifumo ya kiuchumi
Kitabu kinaeleza; Ikiwa (Gen Z) watapewa fursa za kiuchumi, watakuwa nguvu ya mabadiliko na ukuaji (demographic dividend). Lakini ikiwa hakuna ajira, uchumi na fursa, itakuwa janga la kisiasa na kijamii.
Waandishi wa “Making Africa Work” wanaeleza kuwa (Gen Z) wanaishi mijini zaidi na wameunganishwa na mtandao (digital connectivity). Tofauti na vizazi vilivyopita ambavyo vilikuwa vijijini na vilitawanyika
Gen Z siyo Taasisi iliyosajiliwa, ni wazo (Idea). Tofauti na vyama vya siasa ambavyo vina ofisi, viongozi wa kukamatwa, ruzuku za kuzuia, Gen Z ni kizazi chenye itikadi inayozungumza haki, ukweli, na teknolojia.
Gen Z Hawana “central command”. Wao wanakutana ‘online’ tu. Ukimkamata mmoja, wengine elfu kumi wanazaliwa mtandaoni. Huwezi kuua wazo lao ambalo halina ofisi wala msemaji mkuu mmoja. Never.
Gen Z hawana kiongozi mmoja (leaderless movement), hivyo hakuna mtu mmoja wa kumnyamazisha ili harakati zao zifariki. Decentralization haitawezekana kamwe katika Ulimwengu huu wa sasa wa kidijitali.
Habari inasafiri kwa sekunde. Ukijaribu kufunika ukweli mmoja, video 100 zinatokea TikTok au X (Twitter) au Instagram au Facebook. Information speed ni kubwa sana. Huwezi kutengeneza uongo na kuutea uongo.
Usiwaone Gen Z kama adui, waone kama mtaji katika uwekezaji wa baadaye; Wanaishi katika ulimwengu tofauti na vizazi vilivyotangulia. Wao wanafikiria digital, wanataka uwazi, haki, na fursa za kiuchumi.
Huwezi kufungia “spirit” ya watu wanaozungumza lugha moja kupitia mitandao. Washauri wa watawala wanatumia mbinu za karne ya 20 (mabavu, propaganda, na vitisho) kukabiliana na matatizo ya karne ya 21.
Mtawala anayewaona vijana kama maadui anajitenga na uhalisia. Badala ya kutumia nguvu (force), alipaswa kutumia ushawishi (influence). Vijana hawataki kupindua nchi; wanataka nchi ifanye kazi kwa ajili yao.
Kitabu hiki kimeweka msisitizo mkubwa kwamba, Viongozi wanaotaka kuendelea kubaki madarakani lazima waendelee na ukuaji wa kiuchumi wa kweli na kuunda ajira — si kupambana na raia wao wenyewe.
Fanyeni tafiti (research) halisi, si hizi tafiti zenu za uongo za kufurahisha genge; Washauri wa watawala huwaeleza watawala lugha ambayo wanadhani wanayotakiwa kusikia. Hawaelezi ukweli na uhalisia.
Mnatakiwa kutumia data halisi, surveys zisizopendelea upande, na mazungumzo ya moja kwa moja na vijana (bila kuwakamata au kuwatisha). Kuujificha nyuma ya “wanasiasa wana wachochea” ni kukimbia ukweli.
Kitabu kinakataa mifumo ya kufadhiliwa na rushwa (patronage) na kuendesha mambo tu bila mpango (muddling through). Kinasisitiza kuwa ongezeko hili la watu linafanya mifumo ya zamani isifanye kazi tena.
Kitabu hiki kimeandika kwamba, ulinzi wa kweli hautokani na silaha, bali unatokana na raia walioridhika. Kupambana na “Gen Z” ni sawa na kupambana na injini ya gari lako mwenyewe ukiwa barabarani.
Unapochagua mabavu dhidi ya raia wako, unajenga Deep-seated Resentment. Hiki ndicho kizazi chenye nguvu kazi, wabunifu, na walaji wa kesho. Ukiwavunja moyo, unaharibu uchumi wa nchi muda mrefu.
Ukiziba njia zote za kidemokrasia na mazungumzo, unawalazimisha kutafuta njia mbadala ambazo mara nyingi huwa ni za machafuko zaidi. Hapa ndipo inaibuka dhana ya ‘Radicalization’ ili wapate kupumua vizuri.
Kitabu kinaeleza huwezi kuwadhibiti watu ambao wanajua haki zao na wanaona maendeleo ya nchi zingine kwa kutumia mabavu. Gen Z hawawezi kufungwa macho kirahisi. Ulimwengu upo kiganjani.
Badala ya kupambana nao, waweke katika meza ya mazungumzo. Washirikishe katika maamuzi badala ya kuwafanyia maamuzi. Wana maoni makali kwa sababu wanaona matatizo moja kwa moja kupitia mitandao.
Kiongozi unatakiwa kujenga uaminifu mkubwa kupitia vitendo, si maneno; Punguza gharama za maisha kwa vitendo. Pambana na ufisadi bila kuchagua. Toa fursa za kiuchumi kwa vijana (ajira, mikopo, elimu bora).
Tumia mitandao kuwajibu moja kwa moja, si kuwazima ili sauti zao zisikike tena. Msiifungue hiyo mitandao. Msiifanye kama ni majukwaa haramu kuyatumia. Tumia lugha yao kupitia mitandao, memes, na uwazi.
Usiwaone Gen Z kama watu kutoka nje — ndiyo wapiga kura wengi wa baadaye. Miaka mitano ijayo, hawa walio na umri wa miaka 15 had 18 watakuwa na miaka 20 hadi 23 na ndiyo watakuwa wapiga kura wenu wengi.
Watawala mnatakiwa kuanza kufanya town halls za kidijitali na za kimwili (physical) bila kuwakamata. Wajenge uwezo — elimu bora, stadi za tech, na nafasi katika uongozi (youth quotas bunge na serikali).
Tumia Youth Councils na hizi Youth Development Forum ili kupata malalamiko ya vijana. Tumieni data halisi (si kutegemea taarifa za intelligence tu) kuelewa malalamiko halisi ya gharama ya maisha na ajira.
Kitabu kinatoa takwimu Afrika inahitaji kutengeneza mamilioni ya ajira kila mwaka ili kukidhi hitaji la vijana wanaoingia sokoni. Serikali lazima zifanye mageuzi makubwa sana ya kiuchumi (economic reforms).
Toeni mikopo ya vijana (kama SIDO au TIB) bila siasa, anzisheni digital hubs katika mikoa. Tengenezeni National Youth Dialogue Forum na hakikisheni isifanywe kuwa jukwaa la kisiasa la vijana wa mbogamboga.
Vijana si kikwazo, ni kipimo cha uongozi wako; Kiongozi mkubwa si yule anayeshindana na vijana, bali yule anayewaelewa na kuwaongoza kuelekea mustakabali bora. Gen Z wataendelea kukua na kuwa wengi zaidi.
Usipambane na kizazi chako. Kipambane na matatizo yanayowatesa. Kama utawaelewa na kuwahudumia, watakufanya uwe na urithi mkubwa. Kama utawapuuza au kuwapiga, watakuandika kama sehemu ya tatizo.
Kitabu kinathibitisha suluhisho la Afrika siyo bunduki, bali ni sera sahihi, utawala bora, na kutoa nafasi kwa Gen Z kuongoza mabadiliko ya kiuchumi. Mtawala anayewazuia, anazuia maendeleo ya nchi yake.
Watawala someni kitabu, mtaelewa Afrika iko njiapanda. Upande mmoja ni mafanikio makubwa kupitia nguvu ya vijana, na upande mwingine ni machafuko ya kudumu ikiwa mahitaji ya vijana ya kudumu yatapuuzwa.
Huwezi kushinda vita dhidi ya wakati. New generation (hawa ambao tunawaita Generation Z) ni wakati unaokuja, na kamwe, huwezi kuuzuia jua lisioneke kwa kutumia kiganja cha mkono. Msiwachukie Gen Z.
Mimi nimeshauri tu kama mwananchi wa kawaida, mkitaka chukueni ushauri, msipotaka acheni.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Makaa ya mawe Songea
Bomba la Mafuta Tanga
Mradi wa Gas Lindi
Mikoa mitatu inabeba future ya Taifa kwa next 30 years Kama una kibunda sehemu za kuwekeza hizi
Tanga kuna Bandari ambayo sasa inafanya vizuri.
Tunahitaji siasa safi tu na Haki next generation wataishi vizuri
😭 TABIA YA 6
Tabia Ya Kuogopa Kuonekana
Mjinga Au Kushindwa...
Kabla Sijaendelea Kwenye Tabia Hii
Ambayo Imekuwa Ni Ugonjwa
Sugu Kati Ya Watu Wengi.
Naomba Kama Bado Hujasoma Tabia 5
Ambazo Tayari Zipo Hapo Juu
Naomba Uzisome Na
Pengine Zikakusaidia Kujua
Wapi Inabidi Urekebishe ...
Ok... Tuendelee
Sasa Leo Tupo Kwenye Tabia Ya 6
Imagine Labda Unataka Kuanza
• Biashara Mpya.
• Project Mpya.
• Content Creation
• Au Ujifunze Skill Mpya.
Lakini Kabla Hata Haujaanza…
Akili Inaanza Kukuletea Maswali.
↳ Itakuwaje Kama Nikishindwa?
↳ Itakuwaje Kama Watu Watanicheka?
↳ Itakuwaje Kama Nitaonekana Sijui Ninachofanya?
Na Ghafla Unaamua Kitu Kimoja.
Kuacha Kabisa Kujaribu.
Si Kwa Sababu Wazo Halikuwa Zuri.
Bali Kwa Sababu Anaogopa
Kuonekana Mjinga Mwanzoni.
Hii Ni Hali Ambayo Karibu
Kila Mtu Amewahi Kupitia.
Unataka Kuanza Kitu Fulani.
Lakini Ndani Yako
Kuna Sauti Inakuambia:
"Watu Watasema Nini?"
Unaanza Kuwaza:
• Maoni Ya Watu
• Kuchekwa Na Wengi
• Kushindwa Mbele Ya Watu
Na Polepole Wazo Zuri L
inaishia Kubaki Kichwani.
Utaniuliza:
"Francis - Kivipi Hofu Hii Inazuia Watu Wengi Sana?"
Sababu Ni Moja Tu...
Watu Wengi Wanataka Kuonekana
Wako Vizuri Tangu Mwanzo.
Lakini Ukweli Wa Maisha Hauko Hivyo.
Kila Mtu Anayeanza Kitu
Kipya Hupitia Hatua Hii:
* Kufanya Makosa Mwanzoni
* Kujifunza Polepole
* Kuonekana Hajui Kila Kitu
Kwa Kifupi…
Mwanzoni Kila Mtu
Anaonekana Mjinga Kidogo.
Lakini Tofauti Ni Moja.
Wengine Wanaendelea.
Wengine Wanaacha
Kabla Hata Hawajaanza.
Kama Ukiniuliza;
"Nawezaje Kupukana Na Hali/Tabia Hii?"
Nitakwambia Kwamba -
Kama Unataka Kusonga Mbele Maishani…
Lazima Ukubali Ukweli Mmoja Rahisi.
> Hatua Za Mwanzo Hazitakuwa Perfect.
Na Hilo Ni Kawaida Kwa Watu Wote.
Badala Ya Kuogopa Kuonekana Hujui Kila Kitu…
Anza Kujifunza Kwa Vitendo.
• Jaribu
• Fanya Makosa
• Rekebisha Ukiwa Unaendelea Kusonga
Kwa Sababu Ukweli Ni Huu:
Watu Wanaofanikiwa Si Wale Ambao
Hawajawahi Kuonekana Wajinga.
Ni Wale Ambao Hawakuogopa Kuanza.
Lakini Kuna Tabia Nyingine
Moja Ambayo Imepoteza
Fursa Nyingi Sana Kwa Watu Wengi.
Tabia Ya Kuahirisha Maamuzi Muhimu.
Na Mara Nyingi Mtu Anapogundua Kosa Hilo…
Fursa Tayari Imepita.
Baadae Nitaielezea - Stay Tune
Kama Umesoma Mapaka Hapa
Follow, Like Au Toa Reaction Yoyote
-🔥-👍-💪🏾 - 🙏🏽 - 🙌 - ❤️
Soon... Tukutane Kwenye Tabia Ya 7
...
FRANCIS | ABRACADABRA 👇🏻